Tafuta

Vatican News
kile kinachoendelea nchini Siria ni cha ulimwengu mzima katika ngazi mbalimbali kile kinachoendelea nchini Siria ni cha ulimwengu mzima katika ngazi mbalimbali  (AFP or licensors)

UN:Tunashindwa kuhesabu vifo nchi za mashariki!

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa nchini Lebanon, ni nchi ndogo zaidi ya Mkoa wa Calabria wa nchi ya Italia, lakini ni mahali ambapo kuna matatizo yanayozidi kuongezeka ya wakimbizi na wahamiaji

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa kuhitimishia Mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyi mjini Torino nchini Italia hivi karibuni, ukiongozwa na na kauli mbiu Mwisho wa nchi za mashariki na hatima ya watu walio wachache, ripoti yao inasema kuwa nchini Lebanon, ni nchi ndogo zaidi ya Mkoa wa Calabria nchini Italia, lakini mahali ambapo kuna matatizo yanayozidi kuongezeka ya wakimbizi na wahamiaji.  Nchi ya Libanon ni ndogo zaidi lakini inapokea kwa miaka sasa  milioni moja na laki mbili za wakimbizi kutoka Siria.

Zaidi ya milioni 7 ya watu wanarundikana nchini Siria

Ni hali ambayo inafanana na ile ya nchi ya Yordan na nchini Uturuki na zaidi ya milioni 7 ya watu wanamekusanyika nchini Siria. Hiyo ni mifano tu midogo ambayo imeweza kuripotiwa na  kulezea hali halisi ya nchi za Mashariki kutokana na wakimbizi na wahamiaji ambapo ripoti pia inasema, wanashindwa tena kuhesabu watu waliokufa nchini Siria, wakati huo huo watoto wengi hawajuhi hata kusoma wala kuandika  katika lugha yao ya kiarabu, wanachokitambua ni mauti inatokea sehemu gani.

Hadi sasa makundi 98  bado yanaendelea na mapigano

Na hili kuweza kuwafanya watambue zaidi ya vurugu hizi zinazoendelea, wamekumbusha kuwa yapo kwa sasa makundi 98 ambayo yanaendelea na mapigano. Katika mantiki hiyo, nafasi ya Umoja wa Mataifa inakazama kutafuta namna ya kuzungumza na ili kuweza kutazamia kusiitshwa kwa hali ya migogoto na ili kuwezesha maisha kweli endelevu ya nchi ya Siria. Lakini hata hivyo ripoti inabainisha kuwa kile kinachoendelea nchini Siria ni cha ulimwengu mzima kwa ngazi mbalimbali.

13 November 2018, 14:36