TOPSHOT-FRANCE-WWI-POLITICS-HISTORY-CENTENARY-DIPLOMACY TOPSHOT-FRANCE-WWI-POLITICS-HISTORY-CENTENARY-DIPLOMACY 

Paris:kumbukumbu ya miaka 100 tangu Vita ya Kuu ya Kwanza ya Dunia

“Kongamano la kimataifa kwa ajili ya miradi ya utawala". Ndiyo mada inayoongoza Kongamano la Amani mjini Paris,Ufaransa kuanzia 11- 13 Novemba 2018. Hili ni tukio linalijika katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuisha kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 11 Novemba imezinduliwa Kongamano la Amani mjini Paris nchini Ufaransa  kwa ajili ya kufanya kumbukumbu ya miaka 100 tangu kuisha Vita Kuu ya kwanza ya dunia ilipokoma. Kongamano hili la Amani mjini Paris  ni la kwanza na  la aina yake  ambalo ni mkakati ulioandaliwa na serikali ya Ufaransa ukiongozwa na Rais Emmanuel Macron, ambalo limatalizika tarehe 13 Novemba 2018, likiongozwa na kauli mbiu “Kongamano la kimataifa kwa ajili ya miradi ya utawala.” Ni kongamano linalowaleta pamoja karibia viongozi 60 wakuu wa nchi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kwa ajili ya mijadala mbalimbali na kusisitiza ahadi za kukabiliana na changamoto kubwa zionazoikumba dunia hivi sasa.

Umoja wa Ulaya ni hakikisho la amani

Kati ya wageni pia waalikwa yupo, Rais wa Tume ya Ulaya Bwana Jean-Claude Junker, ambaye anakumbukwa wakati wa kutoa hotuba yake mwezi Septemba, 2018, mara baada ya kutaja suala la Vita ya kwanza ya dunia, kuwa alisema kwamba: “Umoja wa Ulaya ni hakikisho la amani. Na hivyo tutafute kuwa wenye furaha kwa sababu ya kuishi katika bara ambalo linatambua amani na hiyo ni shukrani kwa  bara la Ulaya”. Kadhalika ushauri wake ulikuwa kwamba: “ni lazima kuheshimu zaidi Umoja wa Ulaya na si kuchafua sura yake , kwa maana  ni kuilinda kwa namna ya kuwa na pia namna ya kuishi. Bwana Junker alikuwa amekumbusha pia  kwamba: “Mkataba msingi  ya Umoja wa Ulaya ulikuwa ya kwamba pasiwepo kamwe na  vita, na alikuwa amethibitisha kwamba “ sasa ni wakati wa dharura msingi ya amani ambayo leo hii inahitajika na lazima kukesha kwa ajili  yetu na sehemu zote zinazotuzunguka”.

Miaka 100 iliyopita dhamira ya kutokomeza migogoro na vita kwa njia ya amani

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Gueteres  wakati wa thotuba yake mekumbusha kwamba  “Katika miaka 100 iliyopita dhamira ya kutokomeza migogoro na vita kwa njia ya amani kwa mantiki ya sheria na misingi ya pamoja imebadilishwa na kuwa mfumo wa kimataifa wa taasisi katika nyanja za kisiasa,kiuchumi, kijamii na kimazingira.” Akendelea na hotuba  yake ya ufunguzi wa kongamano la Amani la Paris, amesema kwamba “Jinamizi la vita hivyo vikubwa vya kimataifa halitosahaulika , lakini jinamizi halipwaswi kughubika matumaini, kwani ni matumaini kama hayo ndio yaliyoleta kuibuka kwa maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa katika karne ya 20” akimaanisha kuundwa kwa jumuiya ya madola mwaka 1919 na Umoja wa Mataifa baada ya vita kuu ya pili ya dunia 1945.

Kuyumba kwa watu wa kipato cha kati na wengine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiendelea na hotuba yake  amesema, kuna tofauti kubwa iliyokuwepo duniani katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 na leo akiongeza kuwa “hii inatupa mazingira ya hofu kwamba matukio yasiyotabirika yanaweza kutokea. Kwa mfano kudora kwa kiuchumi wa mwaka 2008 sawa na ule wa mwaka 1929, ingawa umedhibitiwa na kubadilishwa mwelekeo, asante kwa vyombo na taasisi za fedha, umesababisha kuyumba kwa watu wa kipato cha kati na wengine kuwa tegemezi wa wale wa daraja la juu. Mfano mwingine alioutoa ni ule wa kuzuka kwa utawala wa kiimla au udikteta miaka ya 1930, “ingawa hatuko tena katika zama hizo amesema lakini tunachokishuhudia hii leo ni ukandamizaji wa maisha ya kisiasa na kijamii ambayo yamesababisha kumomonyoka kwa misingi ya haki za binadamu na uhuru, demokrasia na utawala wa sharia”.

Sumu ya Ushirikiano wa Kimataifa

Kudhoofika kwa msimamo wa demokrasia na tofauti katika misingi ya pamoja ni sababu mbili ambazo ni sumu ya ushirikiano wa kimataifa, amesema Bwana Guterres, akinyonyeshea kidole juu ya mgawanyiko  ya ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Siria, na ongezeko la mivutano ya kibiashara na changamoto ya kujiamini inayoghubika Muungano wa Ulaya ikiwa ndiyo baadhi ya mifano.

Akifafanua kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa Kimataifa Katibu Mkuu amesema “umekuwa ni wa lazima, kwani nchi kwa kushirikiana na kufanya kazi pampoja kumezaa matunda yasiyopingika  ikiwemo kupunguza vifo vya watoto wachanga na umasikini uliokithiri katika karne chache zilizopita , kushinda vita vikubwa dhidi ya tishio la afya ya umma kama vile ndui, polio, na ukimwi. Lakini pia mafanikio mengi ya kuzuia vita na juhudi za ujenzi wa amani.

Mafanikio ya mipango ya ulinzi wa amani kwa miaka 70 iliyopita

Baba Guterres akiendelea amesema,“zaidi ya wanaume na wanawake milioni moja kutoka nchi 125 wamehudumu katika mipango mbalimbali ya ulinzi wa amani katika miaka 70 iliyopita ili kuzuia kusambaa kwa machafuko , kulinda raia na kusaidia mchakato wa kisiasa na kuongezea kwamba operesheni hizo ni za gharama nafuu. Pia amesema ushirikiano wa kimataiofa umedhihirisha kuwa unahitajika hasa katika kutatua mgogoro wa uzalishaji wa silaha za nyuklia akitoa mfano wa mshikamano kwenye Baraza la Usalama katika kukabiliana na nyuklia za Iran na hali ya Korea ya Kaskazini au DPRK, uliowezesha majadiliano ya suluhu mara zote 2015 na 2018!

12 November 2018, 14:13