Mtume Muhammad (S.A.W) alipohamia Madina akajenga Msikiti ili watu wamwabudu Mungu na pili akajenga soko ili watu washiriki shughuli za kiuchumi! Mtume Muhammad (S.A.W) alipohamia Madina akajenga Msikiti ili watu wamwabudu Mungu na pili akajenga soko ili watu washiriki shughuli za kiuchumi! 

Msikitiki utumike kumwabudu Mungu, Soko watu washiriki shughuli za kiuchumi!

“Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kutoka katika mji wa Makka na kuhamia Madina kitu cha kwanza alijenga msikiti ili watu waweze kumwabudu Mwenyezi Mungu, alijenga soko ili watu washiriki shughuli za kiuchumi na alifanya upatanishi kwa makabila mawili kwa lengo la kuonesha kuwa kuishi kwa amani ni kitu bora.”

Na Ofisi ya Waziri Mkuu – Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua msikiti wa Nandagala na amewataka waamini wa dini ya Kiislamu katika Kata ya Nandagala wilayani Ruangwa wautumie vizuri msikiti huo kwa kufanya ibada na kuhamasisha amani na si vinginevyo. “Msikiti huu ninauzindua leo naomba tuutunze vizuri na tuutumie kwa kufanya ibada na si ibada za kiuanaharakati. Watakaokuja msikitini na kufanya mambo ya hovyo Mwenyezi Mungu atawalaani.” Waziri Mkuu alizindua msikiti huo Jumatatu, Novemba 19, 2018, ambapo alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waaamini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha muda wa kufanya swala unapofika waende msikitini hapo kufanya ibada.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka waamini hao waanzishe madrasa na kuwafundisha watoto Quran lengo likiwa ni kuwafundisha misingi ya dini na kuwaandaa vizuri na kuwawezesha kukua kiimani ili waje kuwa waja wema. Hata hivyo, Waziri Mkuu alimshukuru Mzee Suleiman na familia yake kwa uamuzi wao wa kujitolea kujenga msikiti huo ambao utawawezesha waamini katika kijiji cha Nandagala kufanya ibada zao. “Namshukuru na Mzee Mamboleo na mkewe kwa kutoa eneo lao bure ili litumike kujengea msikiti.”

Kwa upande wake, Sheikh Hilal Kipozeo ambaye alihudhuria uzinduzi wa msikiti huo aliwasisitiza waamini wa dini ya Kiislam watumie muda mwingi kwa ajili ya kufanya ibada na wajiepushe na vitendo vyenye kumuasi Mwenyezi Mungu na wadumishe amani. “Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kutoka katika mji wa Makka na kuhamia Madina kitu cha kwanza alijenga msikiti ili watu waweze kumwabudu Mwenyezi Mungu, alijenga soko ili watu washiriki shughuli za kiuchumi na alifanya upatanishi kwa makabila mawili kwa lengo la kuonesha kuwa kuishi kwa amani ni kitu bora.” Wananchi na waamini wa dini ya Kiislamu katika kijiji cha Nandagala walimshukuru mfadhili aliyejenga msikiti huo kwa sababu utawawezesha kuwa na eneo la kufanyia ibada baada ya lile la awali kubomolewa kwa kuwa walijenga katika hifadhi ya barabara.

20 November 2018, 12:05