Rais Magufuli aahairisha maadhimisho ya Sherehe za Uhuru kwa mwaka 2018 na fedha ya sherehe hizi kutumika kujenga Hospitali ya Uhuru, Dodoma! Rais Magufuli aahairisha maadhimisho ya Sherehe za Uhuru kwa mwaka 2018 na fedha ya sherehe hizi kutumika kujenga Hospitali ya Uhuru, Dodoma! 

Rais Magufuli aahirisha maadhimisho ya sherehe za uhuru, 2018 na fedha sasa kujenga Hospitali ya Uhuru, Dodoma!

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne, Novemba 20, 2018 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru, Desemba 9, 2018 na fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha shamrashamra hizo ameelekeza zitumike kujenga hospitali mkoani Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne, Novemba 20, 2018 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais Dkt. Magufuli ameagiza kiasi cha shilingi milioni 995.182 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo zitumike kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa mkoa wa Lindi pamoja na wilaya zake katika kikao cha maandalizi ya shughuli za kuzima Mwenge kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Amesema hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam itakuwa inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wananchi wengine watakaokuwa  mkoani humo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya waandae matukio watakayoyatekeleza katika maeneo yao yatakayoashiria maadhimisho ya siku ya Uhuru. “Wanaweza kutumia siku hiyo kwa kufanya usafi maeneo ya wazi au kwenye hospitali.” Kufuatia maagizo hayo, Waziri Mkuu amewataka wananchi katika maeneo yote nchini wajiandae kufanya shughuli mbalimbali za kijamii zitakazopangwa na wakuu wao wa mikoa na wilaya kufanyika katika maeneo yao.

21 November 2018, 07:46