Cerca

Vatican News
Maandamano makubwa yamefanyika pande zote duniani,  hata mamia elfu ya wanawake nchini Italia waliungana mjini Roma katika kupinga kila aina ya ukatili dhidi yao Maandamano makubwa yamefanyika pande zote duniani, hata mamia elfu ya wanawake nchini Italia waliungana mjini Roma katika kupinga kila aina ya ukatili dhidi yao   (ANSA)

25 Novemba ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake!

Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 25 Novemba 2018 na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, (UNODC) inasema nyumbani ni mahali hatari zaidi kwa wanawake na hususan kwa mauaji na ukatili wengi wakipoteza maisha mikononi mwa wenzi wao au familia. Ni ripoti kufuatia na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake 25 Novemba

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Migogoro inaongezeka na vurugu katika dunia, wakati huo hata idadi ya mauaji, nyanyaso za kijinsia ukatili na ubaguzi dhidi ya  wanawake. Ni mambo ambayo yameweze kutolewa katika Jukwaa la dunia juu ya hali za binadamu, liloandaliwa katika siku hizi huko Strasburgh katika Baraza Kuu la Ulaya, sambamba na maadhimisho ya Kimatifa siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, ambayo inafanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 mwezi Novemba.

Taarifa zaidi juu ya vurugu hizo lakini hata aina mbalimbali za vurugu 

Mwanamke mmoja kati ya watatu duniani anapata moja ya mtindo wa ukatili ikiwa ni kimwili au kijinsia, lakini kwa sasa upo hata ujasiri wa kutoa taarifa juu ya suala hili. Naye Rais wa Baraza La Ulaya juu ya kupinga  na kupambana na dhidi ya vurugu na nguvu za nyumbani wa  (kitengo cha Instambul) amesema: “ upo uelezwa zaidi juu ya vurugu dhidi ya wanawake sasa kulinganana na miaka kumi iliyopita, kwa maana wapo watu wengi wanatoa taarifa juu ya suala hili. Na zaidi hata takwimu za mabadiliko hayo, zimefanya kuelezea zaidi na kwa haraka juu ya aina mbalimbali za ukatili ambao ulikuwa haujulikani kabisa, anathibithisha.

Nyumbani ndiyo mahali penye hatari zaidi katika uhai wa wanawake

Na wakati huo huo Ripoti mpya iliyotolewa tarehe 25 Novemba 2018 na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu, (UNODC) inasema nyumbani ni mahali hatari zaidi kwa wanawake na hususan kwa mauaji na ukatili wengi wakipoteza maisha mikononi mwa wenzi wao au familia. Ripoti hiyo imetaja kuwa ni  wanawake 87,000 waliuawa mwaka jana , huku 50,000 au asilimia 58 ikiwa ni mikoni mwa wenzi wao au jamaa watu wa familia. Hii ina maanisha wanawake 6 huuawa kila saa moja na watu wanaowafahamu umesema utafiti wa ripoti hiyo. Matokeo ya utafiti huo yalitolewa metolewa yanaangazia takwimu zilizopo za mauaji na kutathimini mauaji yanayohusiana na masuala ya jinsia kwa wanawake na wasichana yakijikita zaidi kwa mauaji kutoka kwa wapenzi na watu wa familia na jinsi gani yanahusiana na hali na jukumu la mwanamke katika jamii kwa ujumla.

Wanawake wanalipa gharama kubwa kutokana na kutokuwepo usawa wa kijinsia

Akifafanua kuhusu ripoti hiyo mkurugenzi mtendaji wa UNODC, Yury Fedotov amesema “Wakati wengi wa waathirika wa mauaji ni wanaume, wanawake wanaendelea kulipa gharama kubwa kutokana na kutokuwepo usawa wa kijinsia, ubaguzi na tabia mbaya. Pia wana uwezekano mkubwa wa kuuawa na wapenzi wao  na ndugu wa karibu katika familia, "

Ameongeza kuwa ili kukabiliana na uhalifu huo "Hatua madhubuti za haki dhidi ya uwahalifu zinahitajika ili kuzuia na kumaliza mauaji yanayohusiana na jinsia na pia ili kuongeza uelewa na kuwajulisha kuhusu hatua. " Utafouti huo umebaini kwamba kiwango cha kimataifa cha mauaji ya wanawake na wasichana yanayofanywa na wenzi wao au wanafamilia ni mwathirika 1.3 kwa kila wanawake 100,000. Katika kuangalia wapi kulikoathirika zaidi utafiti umegundua kwamba Afrika na ukanda wa Amerika ndiko wanawake waliko hatarini zaidi kuuawa na wenzi wao au wanafamilia. Na kwa Afrika kiwango ni wanawake 3.1 kwa kila wanawake 100,000, wakati nchi za Amerika ni wanawake 1.6 Ocenia 1.3 na asia 0.9. Eneo lililo na kiwango kidogo kabisa kwa mujibu utafiti huo ni Ulaya ambako kiwango ni 0.7 kwa kila wanawake 100,000.

Uratibu mzuri na ushirikiano miongoni mwa polisi na mifumo ya haki na sheria

Ripoti hiyo imehitimisha kwa wito wa kuhimiza hatua za kuzuia uhalifu  na adhabu  kwa ukatili dhidi ya wanawake ambazo zitachagiza usalama wa waathirika na kuwawezesha , lakini wakati huohuo kuhakikisha uwajibikaji wa hali ya juu kwa watekelezaji wa uhalifu huo. Pia imetaka kuwe na uratibu mzuri na ushirikiano miongoni mwa polisi na mifumo ya haki na sheria, mifumo ya afya, na huduma za jamii na pia kuwahusisha wanaume katika kupata suluhu ya jinamizi hili ikiwemo katika elimu ya mapema.

Hata hivyo Kufuatia na maadhimisho ya siku hiyo ambayo yalianzishwa na umoja wa mataifa, ili kuleta uwazi wa uelewa wa matukio hayo na ili  kuyaondoa kabisa hata katika jamii zilizoendelea. Kwa mujibu wa Polis inchini Italia, takwimu zinaonesha vifo vya wanawake 32 kwa miezi tisa ya mwaka 2018. Kutokana na hiyo naye Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarellia amesema kuwa tukio hili na la juu. Kwa Mkuu wa Nchi, anasema taarifa za matukio ya unyanyasaji na unyanyaswaji bado hazikubaliki kwa maana ya  ubaguzi na maoni dhidi ya majukumu na mitazamo ya msingi ya jinsia, lazima yashinde, kuanzia utotoni na ulimwengu wa shule.

Wanawake nchini Italia waandamanama kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Pamoja na hayo nchini Italia Jumamosi 24 Novemba 2018, yalifanyika maandamano makubwa mjini Roma ya wanawake kwa ajili ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, hiyo pia ni pamoja na maandamano mengi yaliyofanyika katika nchi mbalimbali duniani kote kwa ajili ya kuhamasisha uelewa huo wa vurugu na ukatili. Hata baadhi ya wanamichezo wa mpira pia walitelemka uwanjani wakiwa wamechorwa usoni mwao  rangi nyekundu ishara ya ishirikiano ulioanzishwa wa kupinga kila aina ya manyanyaso, vurugu na ukatili dhidi ya wanawake. Na Chama cha (Di. Re) kinachohusika na kufuatiala nyanyaso za wanawake kwa njia ya mtandao, wanathibitisha kuwa uwepo wa  mshambuliaji  kwa wastani wa  asilimia 65% ni wa Kiitaliano. Takwimu za hivi karibuni za (ISTAT) pia zinatoa taarifa kwamba wanawake ambao walikwenda kwenye vituo vya kupambana na unyanyasaji mwaka 2017 walikuwa zaidi ya 49 elfu, ambapo zaidi ya elfu 29 wameanza mchakato wa  njia ya kuondoka kwa vurugu hizo. Je ni akina nani wanawasiliana na vituo? Katika asilimia 27% ya kesi ni wageni na wakati huo asilimia 63.7% sehemu kubwa ni kesi za watoto wadogo .

26 November 2018, 15:57