Tafuta

Vatican News
Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania 

Tanzania:maendeleo ya wanawake katika biashara ya viwanda!

Kongamano kuhusu“Maendeleo ya Wanawake katika Biashara ya viwanda,limefanyika Jijini Dar Ess Salam,Tanzania tarehe 27 Oktoba 2018. Ni Kongamano la nne lililoandaliwa na sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania (VoWET) na kuhudhuriwa na asasi nyingine kama,TWCC, Purple Planet, TAFOPA na NABW

Na Natujwa Sengoka - Dar es Salaam,  Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wanawake wajasiriamali Tanzania, wametakiwa kuungananisha mitaji ili kuweza kuzalisha bidhaa na huduma zitakazowawezesha kushiriki kwenye uchumi wakati wa Tanzania ya Viwanda. Hayo yameelezwa kwa washiriki wa mdahalo kutoka asasi mbalimbali zinazowahudumia wanawake wajasiriamali, katika Kongamano lililofanyika tarehe 27 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ni kongamano lililoongozwa na kauli mbiu, “Maendeleo ya Wanawake Katika Biashara.” Na ni Kongamano la nne lililoandaliwa na sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania (VoWET) na kuhudhuriwa na wanawake zaidi ya 500.

Katika jopo liliunganishwa na  washiriki kutoka asasi za sauti ya wanawake wajasiriliamali Tanzania (VoWET), TWCC, (Purple Planet), Chama cha wasindikaji (TAFOPA) na Chama cha Taifa cha Biashara cha Wanawake (NABW)  na kwa pamoja wamewataka wanawake kuacha ubinafsi kwani uchumi wa viwanda unataka uwekezaji mkubwa.

 Lengo la VoWET ni  kukuza biashara za wanawake Tanzania

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Rais wa VoWET, Bi. Maida Waziri alisema, VoWET imedhamiria kukuza biashara za wanawake wa Tanzania kwa njia ya kuwajengea uwezo, kuwawezesha kuwa na mitandao na wigo mpana wa mawasiliano kwa lengo la kupata masoko na kushirikishana fursa pamoja na kufanya utetezi juu ya sheria na sera zisizoweka mazingira rafiki kuwezesha kukuza biashara za wanawake.

Naye mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliyekuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo Bi. Sara Msafiri amesema, serikali ya Tanzania inafanya mchakato wa kuunganisha huduma zote zinazotolewa na mamlaka za udhibiti, ili kupunguza urasimu kwenye upatikanaji wa vibali na hati muhimu katika shughuli za uzalishaji wa viwandani. Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni aliweza kukabidhi hata cheti kwa wadhamini wao wa muda mrefu, Chama cha Vodacom, hata kuweza kutembelea maonyesho ya ujasiriamali kwa  walioshiriki kongamano hilo. Akihitimisha mjadala kuhusu ujasiriamali na changamoto zake, muendesha mdahalo huo Bibi Vida Nasari, amewataka wanawake kote nchini Tanzania kuhakikisha wanarasimisha biashara zao na kuziongezea thamani ili waweze kumudu ushindani wa kibiashara na pia kuweza kushinda zabuni kubwa za serikali.

Wanawake waelimike na wajue nini wanatakiwa kufanya katika kuingia Tanzania ya viwanda

Naye Bi Happy Seiph Rwechungura  mjumbe wa bodi ya Sauti ya wanawake wajasiriamali Tanzania  (VoWET), akihojiana na vyombo vya habari kuhusiana na suala la kongamano la wanawake wajasiriamalia: “ tumefika hapa, wahakikishe kukutana na watu na kusalimiana, waangalie biashara zao, wajue wanafanya kitu gani, lakini kikubwa zaidi wapate elimu, na tunawashauri waendelee kuudhuria makongamano kama haya kwa sababu sisi nia  yetu ni kuwaelimisha wanawake wenzetu wajue ni nini wanatikiwa kufanya katika  kuingia Tanzania ya viwanda”. Bi Rwechungura amethibitisha!

Tujue malengo ya asasi za sauti ya wanawake wajasiriamali

 Licha  asasi za sauti ya wanawake wajasiriamali zilizopo Tanzania,  VoWET ni asasi isiyo ya kiserikali, iliyoanzishwa kunako 2014 ili kusaidia kupaza sauti za wanawake wajasiriamali na kukuza biashara zao. Tangu kuanzishwa kwake, VoWET imefanikiwa kuwafikia wanawake zaidi ya 500 na vikundi zaidi ya 23 vya ujasiriamali  na kuwajengea uwezo kwa njia ya mafunzo ya usimamizi wa biashara, ziara za mafunzo na maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Pia VoWET imefanikiwa kununua shamba la ekari 50  katika kijiji cha Kifuru wilayani Kisarawe Tanzania, kwa lengo la kujenga chuo cha ujasiriamali. Pamoja na mafanikio hayo kwa miaka mine, sasa VOWET imekuwa ikiendesha Kongamano la kuwasaidia wanawake kuwa mahiri kibiashara ambapo pia hupata fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zao.

Asasi ya Planet Purple Tanzania

Kadhalika hata asasi ya Planet Purple  Tanzaniani mashirika yasiyo ya kiserikali  ambayo yaliingia nchi ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujihusisha na Mipango ya Uwezeshaji wa Wanawake na Majadiliano ya Wanawake katika chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania. Lengo  msingi ni kuweka, upyaisho katika vijiji  na makao ya jiji nchini Tanzania, kwa maana hiyo Planet Purple inalenga katika maendeleo ya wanawake na wajasiriamali, haki za wanawake na mazingira, maendeleo ya jamii na utamaduni.

Vilevile lengo jingine pia  ni kusaidia, kuhamasisha wanawake wa kipato cha chini kuwa na kujitegemea kiuchumi na kuwa washiriki wenye nguvu katika maisha yao na jamii kwa ujumla. Wanatafuta kuimarisha mabadiliko ya wanawake walioachwa nyuma na ili kupanua upatikanaji wao kwa rasilimali zilizopo za kiuchumi na za asili. Na hatimaye wanatarajia kuwa wanaweza kuwa na  uwezo wa kutumia sauti yao, kufanya maamuzi yao mwenyewe, na kushiriki kikamilifu katika fursa za kiuchumi.

 Sera nzuri na mipango juu ya usawa wa kijinsia

 Tangu mwanzo wa Malengo ya Maendeleo Endelevu mwezi Desemba 2015, na kuanzishwa kwa Jopo la Uwezeshaji wa Uwezeshaji wa Wanawake mwaka 2016 na kulingana na Muktadha wa Kiafrika hasa Tanzania juu ya hali ya wanawake, Planet Purple iliweka kipaumbele juu ya kuendeleza kuunganisha mpango wote wa miaka 12 unaoitwa Mpango wa Uwezeshaji wa Wanawake nchini Tanzania na ambao  unazingatia kufungua wanawake macho na upeo kutokana na uwezo wa kufanya kazi na kufikia uhuru wao wa kifedha kupitia maendeleo ya biashara ya kilimo, kuongeza ufikiaji wa fedha, kukuza viwanda vya ubunifu uchumi na kujenga uwezo wa wanawake katika vijijini hadi mijini.

WANAWAKE TANZANIA
30 October 2018, 10:34