Tafuta

Tarehe 2 Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya kutotumia nguvu Tarehe 2 Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya kutotumia nguvu 

Siku ya kupinga kutumia nguvu katika wazo la Gandhi na Papa!

Kutotumia nguvu ndiyo matumaini yaliyo makubwa. Kwa mujibu wa Gandhi ndiyo silaha yenye nguvu zaidi ambayo haijawahi kuvumbuliwa na mtu. Kwa upande wa Papa Francisko ni mtindo wa siasa ya amani

Sr. Angela Rwezaula na  Frt. Frank Gilagiza – Vatican

Kueneza ujumbe wa kutotumia nguvu hata kwa njia ya mafundisho na uhamasishaji wa jumuiya na ili kuweza kuhakikisha kunakuwepo utamaduni wa amani, uvumilivu na uelewa. Ndiyo lengo la Siku ya Kimataifa ya kutotumia nguvu ambayo inaadhimishwa katika siku ya kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi, tarehe 2 Oktoba, ili kuweza kusikika sauti ya maneno yake ya amani duniani!

Wazo la Gandhi

Kwa mujibu wa maneno ya Gandhi anathibitisha: "Ninapinga kutumia nguvu, kwa sababu unapodhani kuwa umezaliwa wema, huo ni wema wa muda tu; wakati ubaya unaofanyika unabaki”. “Kutotumia nguvu, anaongeza Gandhu kuwa, ndiyo nguvu zaidi iliyowekwa katika maisha ya binadamu. Ni nguvu zaidi ya silaha ya uharibifu ambao kwa binadamu anaweza kuuelewa”.

Wazo la Gandhi leo hii, bado ni kisima cha kuchota na kuigwa mfano kwa  vyama mbalimbali vinavyopinga nguvu na vinaongeze sauti katika kikundi cha kwaya nzima ya kutafuta amani ya kweli. Kati ya watu muhimu wasio weza kusahaulika ni Martin Luther King. Katika wito wake alisema, “silaha yenye nguvu zaidi ni ile ya upendo”. “Katika msingi wa imani yetu ya kutotumia nguvu, kuna kukubali kwamba,  yapo mambo mazuri, ambayo ni tunu na kweli daima  ambayo ni vema hata kufia. Na mtu anakufa pale tu anaposhindwa kupambania kile ambacho ni chenye haki”.

Papa Francisko: Siasa za kutotumia nguvu, zinanapaswa kuanzia kati ya kuta za nyumba

Kwa upande wa Baba Mtakatifu Francisko, wa kutokutumia nguvu, hasa yeye anathibitisha kuwa: "ni mtindo wa kisiasa wa amani". Katika Ujumbe wake kwenye fursa ya Siku ya Amani duniani mwaka 2017  anaadika kuwa: “ Siasa za kutotumia nguvu, zinapaswa kuanzia kati ya kuta za nyumbani na ili kuweze kuenea ndani ya familia nzima ya kibinadamu. "Upendo na kutotumia nguvu  viwe ndiyo kiongozi kwa namna tunavyo kaa na wenzetu katika mahusiano: binafsi, kijamii na yale ya kimataifa".

Kadhalika kwa mujibu wa Papa Francisko: “kushuhudia kutotumia nguvu maana yake ni kufungua njia ya mapatano, kwani : “Unapoweza kuvumilia kishawishi ya kutolipiza kisasi , waathirika wa nguvu wanaweza kuwa mstari wa mbele na kuaminika katika mchakato wa kutotumia nguvu kwenye ujenzi wa amani”. Ujumbe wake, unatoa matashi mema kwa  namna ya pekee kuanzia ngazi ya chini ya kila siku hadi kufikia ile ya sasa ya dunia na ili kutotumia nguvu iwe ndiyo mtindo na tabia ya maamuzi yetu, katika mahusiano yetu, katika matendo yetu na katika sera zote za kisiasa".

Siku ya Kimataifa ya kutotumia nguvu, kwa maana ya amani

Mnamo mwaka 2007, Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, uliiweka kila tarehe 2 Oktoba ya kila mwaka kuwa ni siku ya kimataifa ya kutokutumia nguvu na hivyo ni amani, ambayo inakwenda sambaba na siku ya kuzaliwa Mahatma Gandhi, Baba wa Taifa la India. Naye Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutaka ulimwengu kufuata mtizamo endelevu na busara za Mahatma Gandhi ambaye aliishi kwa namna  ya kutokuwa na vurugu ambayo ndiyo mwafaka wa kutengeneza njia ya amani na maendeleo.

Dunia isiyokuwa na vurugu

Amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kutokutumia nguvu duniani iliyofanyika tarehe 2 Oktoba , katika sikukuu ya kuzaliwa kwa kiongozi shujaa na jasiri, Baba wa Taifa, kiongozi wa falsafa na mkakati wa amani, mpigania uhuru wa nchi ya India. Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa anaeleza,“ katika nyakati za migogoro ya muda mrefu na changamoto ngumu, tunabaki kuhuishwa na falsafa ya Gandhi”.

Katika umoja wa mataifa, Bwana Guterres anasema “tunalo jukumu msingi la kuunda Ulimwengu usio na vurugu na kutafuta suluhu la changamoto zilizopo bila umwagaji damu”. Bwana Guterres amekuwa nchini India toka tarehe 1 hadi 4 Oktoba, kushiriki matukio kadhaa yanayopamba maadhimisho ya miaka mia moja na hamsini tangu  kufariki kwake Mahatma Gandhi. Siku ya jumanne 2 Oktoba alitembelea makumbusho ya Gandhi ya Raj Ghat mjini Delhi, na kuweka shada la maua kwa Heshma ya Gandhi.

Haki za kijamii

Bwana Guterres amekumbusha jinsi Gandhi alivyojitolea kupambania haki na usawa katika jamii, amesema ni wakati mwafaka sasa kwa utandawazi kujikita katika mizizi ya hadhi ya mwanadamu, katika nyakati  hizi  ambapo dunia inakuwa na malengo ya kimaendeleo na kusisitize usawa wa kijinsia na bila kumuacha yeyote nyuma.

Amani na maendeleo

Hati ya umoja wa mataifa, anasema Katibu mkuu, Ibara ya Sita, kwa kutumia  maneno “kabla ya yote” mazungumzo, ushauri upatanisho na kusuruhisha, maamuzi ya kimahakama na njia yoyote ile ya kupambana na kiashiria  cha amani. Kadhalika ameongeza kusema,  “tunapata mwangwi wa Gandhi anayeeleza kinagaubaga: “ Njia ya amani ni kubwa kabisa aliyopewa mwanadamu”. Gandhi aliamini, njia ya amani inaweza kubadili historia, kwa maana hiyo Bwana Guterres anautaka ulimwengu uhuishwe na mtizamo wa Gandhi anayesema:“ujasiri unakufanya uwe na uhakika na unaloamini, kadiri tunavyoendelea kutafuta amani, maendeleo endelevu na haki za binadamu kwa wote”.

05 October 2018, 09:50