Cerca

Vatican News
Ni zaidi ya miezi miwili tangu kuanza kwa ugonjwa wa Ebola huko Kaskazini ya Kivu , DRC (AFP or licensors)

CONGO: Ebola bado ni changamoto katika kanda husika!

Pamoja na migogoro inayo endelea katika kanda ya Congo (DRC) na kuwakilisha matatizo makubwa ya kuweza kuingilia kati, jibu la haraka la utoaji wa huduma katika maadhi ya vituo mbalimbali vya afya kwa Madaktari wasio kuwa na Mipaka, wanaendelea kugawa vifaa na huduma muhimu katika dharura hiyo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni zaidi ya miezi miwili tangu kuanza kwa ugonjwa wa Ebola huko Kaskazini ya Kivu( DRC). Mwaka huu hali bado siyo nzuri na haijathibitiwa, ambapo kesi mpya zaidi zimejitokeza katika kilimeta  100 kuelekea kanda ya kati ya nchi. Mara baada ya uthibitisho wa ugonjwa huo tarehe Mosi Agosti,  Madaktari wasio na Mipaka, walianza mara moja shuguhuli yao kwa ushirikianoa na mantiki ya mpango wa Ofisi ya Waziri wa Afya nchini DRC. Pamoja na migogoro inayoendelea katika kanda hiyo na kuwakilisha matatizo makubwa ya kuingilia kati, lakini jibu la haraka katika maadhi ya vituo mbalimbali vya afya wanaendelea kugawa vifaa na huduma muhimu katika dharura hiyo.

Kadhalika kuna badhi ya tiba mpya ambayo inaweza kuchukua nafasi muhimu kutoa jibu la haraka na mwafaka wa virus vya Ebola. Vipimo vya damu vinavyo chukuliwa katika maabara kwenye vituo vya kutibu, vinasaidia madaktari kuanza kwa haraka na kutoa matibabu kwa wagonjwa. Kwanza wanatumia madawa ya aina tano katika mwendelezo wa matibabu ya mgonjwa na uwezekano wa kufanyia majaribio ya maana katika tiba hizi mpya kati ya wagonjwa wa Ebola kwa masaa 24, baada ya kuthibitisha uchanya wa virus.  Vifo kati ya wagojwa wa Ebola ni kubwa ambayo ni  sawa na asilimia karibu 50%. Madawa mapya yana nguvu  ya kuongeza uwezekano wa kuishi, kwa mujibu wa utafiti wa madaktari.

Kadhalika maafisa wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamethibitisha watu 24 zaidi wamefariki dunia kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo katika kipindi cha wiki iliyopita. Maafisa hao wa Afya wametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuchukua hatua za kujikinga dhidi ugonjwa huo hatari. Makundi ya waasi yamekuwa yakiendeleza uhalifu mpakani mwa Rwanda na Uganda hali ambayo imefanya kuwa ngumu jitihada za kutoa huduma za kimatibabu. Hadi sasa kesi 216 zimegunduliwa  na kati ya hizo kesi 181zimethibitiwa watu  104 wamekufa na 57 wamepona.

Maeneo mengine yenye virus vya Ebola pia  ni karibu na mpaka wa Uganda

Hata hivyo kwa mujibu wa wataalam hao wanasema hali ya Ebola siyo kwamba inazidi kuongezeka sana, lakini hali inabaki ya kutia wasiwasi. Wapo wangonjwa waliothibitiwa wa Beni na Butembo, lakini pia hata maeneo mengine ya ndani zaidi yanayopakana na Uganda. Hayo yamethibitiwa na Laurence Sailly mratibu wa dharura wa Madaktari wasio kuwa na mipaka. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ameonya kuwa ghasia za hivi karibuni nchini humo zinakwamisha juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo.

Mmoja miongoni mwa waathirika ni fundi bomba ambaye anafanyakazi na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika ukanda huo, amepata maambukizo ya virusi vya Ebola alipokuwa akienda kwa mganga wa kienyeji ambaye anadaiwa kumhudumia mmoja wa waathirika wa ugonjwa huo. Mapema mwezi huu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya ziara ya dharura kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano makali nchini humo ambayo yametatiza jitihada za kudhibiti kuzuka kwa virusi vya Ebola. Mapigano makali kati ya makundi yaliyojihami katika mji wa Beni Mashariki mwa nchi yamewalenga pia wahudumu wa afya wa Umoja wa Mataifa na kupunguza kasi ya vita kuzuia kuenea kwa Ebola nchini DRC

17 October 2018, 15:09