Tafuta

Tarehe 15 Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya  wanawake vijijini Tarehe 15 Oktoba ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya wanawake vijijini 

15 Oktoba ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake vijijini

Katika siku ya Kimataifa ya wanawake vijijini, inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 15 Oktoba, ujumbe unasema,“kuwawezesha wanawake na wasichana wa vijijini ni jambo muhimu kwa ajili ya kujenga mstakabali bora kwa kila mtu duniani”

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa vijini tarehe 15 Oktoba, ni siku inayo mulika kwa nguvu zote kutazama masuala ya wanawake vijijini duniani kote. Wao ni taa lakini inayo ng’aa katika giza nene, kwa kukanyagwa bila kuonekana. Mara nyingi vyombo husika vimekuwa vikitaka wamulikwe wanawake na wasichana wa vijijini na kutekeleza ipasavyo malengo ya maendeleo endelevu, (SDGs), ambayo kwa wingi yanalenga hali ya wanawake vijijini.

Kutetea wanawake: Vyombo husika vya utetezi wa wanawake vimekuwa  vikisisitiza juu ya haja ya kulinda na kuendeleza haki za wanawake na wasichana vijijini, na kusema kuwa wanawake hao ambao ni robo ya idadi ya watu duniani, hukumbana na changamoto za kimfumo na vizuizi katika kufurahia haki zao kikamilifu. Kadhalika katika nchi nyingi, mahitaji ya aina yake ya wanawake hao hayashughulikiwi katika sheria, katika sera za kitaifa na mikoa, na katika bajeti.

Hata hivyo hata  Baba Mtakatifu katika kutazama sura ya mwanamke akimtazama kwanza Mama Maria ambaye ni mfano na kielelezo cha wanawawake wote duniani  amesema kuwa wanawake kweli kama tabernakulo ya Injili ya uhai, ili kuwaheshimu na kutambua dhamana, wito na utume wao kwa Kanisa na jamii katika ujumla wake. Na kwamba hata katika ukimya wao, wanawake ni nguvu ya matumaini.

Changamoto: Na hiyo ni changamoto kubwa ya kuwasilimamia na kuwalinda dhidi ya ukandamizwaji na pamoja na ukatili wanaofanyiwa wanawake wengi katika dunia hasa kutokana na kuendekezwa kwa mfumo dume, ambao kwa sasa umepitwa na wakati. Amethibitisha kwamba  umefika wakati wa kutunga sheria zinazolinda utu na heshima ya wanawake dhidi ya ghasia na vipigo. Inabidi kutafuta njia na mbinu ya kupambana na utandawazi usioguswa na shida na mahangaiko ya wengine.

Ushuhuda wa Kanisa kwa upande wa wanawake: Kanisa mara nyingi limekuwa likihimiza mshikamano na mkamilishano kati ya wanawake na wanaume walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Kwa ujumla wake, kupitia masharika mengi ya upendo, hasa yanayofanya toa hduma katika vijiji na pembezno mwa jamii, likuwa msaada mkubwa katika kuwainua wanawake vijijini. Kutokana na hiyo wote wanawajibika  kukuza na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya utandawazi na utamaduni wa kifo.

Katibu wa Umoja wa Mataifa: Katika kilele cha kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya wanawake vijijini, naye  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema, “Wanawake wa vijijini ni msingi kwa maendeleo ya wote”, Amesisitiza  hayo tarehe  15 Oktoba 2018, siku inayokumbuka kweli wanawake wote vijijini. Hata hivyo amesema ili kuwajengea uwezo makundi hayo ni lazima nchi zichukue hatua ya kuhakikisha kuwa wanawake wa vijijini na wasichana wanafurahia kwa hakika haki zao za binadamu. Ametaja haki hizo kuwa ni pamoja na uwezo wa kumiliki ardhi, kupata chakula cha kutosha na chenye lishe, maisha yasiyo na aina yoyote ya vurugu, na waweze pia kupata huduma bora ya afya ikiwemo afya ya uzazi bila kusahau elimu bora na nafuu.

Ujumbe wa Bwana Guterres kwa siku ya wanawake vijijini umesema, “ili kufikia hayo ni lazima uwekezaji, maboresho ya sheria na sera na kuwahusisha wanawake wa vijijini katika maamuzi yanayoathiri maisha yao na kwamba kwa kuwekeza katika ustawi, maisha na uimara wa wanawake na wasichana wa vijijini dunia itafikia maendeleo ya wote. Kuwawezesha wanawake na wasichana wa vijijini ni jambo muhimu kwa ajili ya kujenga mstakabali bora kwa kila mtu duniani.

15 October 2018, 15:15