Cerca

Vatican News
SAUDI ARABIA ETHIOPIA ERITREA PEACE ACCORD Makubaliano ya amani kati ya Eritrea na Ethiopia  (ANSA)

Viongozi wa Ethiopia na Eritrea wasaini mkataba wa amani

Mkataba wa amani umetiwa saini kati ya Ethiopia na Eritrea, shukrani kwa msaada wa Umoja wa Matafia ambao wamejitahidi na kwa nguvu ya makubaliano ya tarehe 9 Julai mwaka huu. Tukio lililoshuhudiwa na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz katika mji wa Jeddah na Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Viongozi wa Ethiopia na Eritrea wametia saini mkataba wa amani tukio lililoshuhudiwa na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz katika mji wa Jeddah. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres na maafisa wa umoja wa Afrika pia walikuwemo katika tukio hilo muhimu tarehe 16 Septemba 2018, lakini Mambo muhimu yaliyoainishwa kwenye mkataba huo bado hayajawekwa wazi. Mkataba huo umetiwa saini, shukrani kwa msaada wa Umoja wa Matafia ambao wamejitahidi na kwa nguvu ya makubaliano ya tarehe 9 Julai mwaka huu.

Hii inakuja miezi miwili baada ya Rais wa Eritrea Isaias Afewerki na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kusaini mkataba mwingine wa amani wa kumaliza uhasama uliodumu kwa takriban miongo miwili na kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili jirani.

Hata hivyo Maandamano ya kupinga vita vya kikabila yafanyika Addis Ababa Ethiopia.Waandamanaji wenye hasira kali wameuzingira mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa baada ya kuuawa kwa watu 23 wakati wa mapigano ya kikabila yaliyoibuka mwishoni mwa juma lililopita.

Wamezuia barabara kuu za jiji hilo, sambamba na kufunga biashara mbalimbali wakiitaka serikali ichukue hatua muhimu kuzuia mauaji hayo. Wakaazi wa jiji hilo wanawalaumu vijana wa kabila la Oromo kuwa walianzisha fujo katika mitaa ya mji wa Burayu ambapo walitumia visu, mawe na vyuma.

Polisi inasema zaidi ya watu 200 wamekamatwa kufuatia mapigano hayo. Migogoro ya kikabila imeogezeka nchini Ethiopia tokea waziri mkuu anayetajwa kuleta mageuzi makubwa nchini humo Abiy Ahmed Ali kuingia madarakani mwezi April.

17 September 2018, 09:39