Tafuta

Vatican News
Migogoro ya vita inasababisha kiwango cha elimu kuwa chini katika chi ya Lebano na Siria Migogoro ya vita inasababisha kiwango cha elimu kuwa chini katika chi ya Lebano na Siria  (ANSA)

Kipeo cha elimu katoliki nchini Lebanon!

Katika Mkuntano wa mwaka huu utajikita katika masuala ambayo yanaweka hatari mwendelezo wa uwepo wa shule za kikatoliki katika muktadha wa sasa nchini Lebanon

Frt Titus Kimario - Vatican

Mwanzoni  wa mwaka mpya wa masomo, kwa mwaka wa pili mfululizo, shule za Kikatoliki na taasisi zote za elimu zisizo za serikali zinaanza  masomo katika hali ya mgogoro mkubwa, ambayo imekuwa katikati ya kazi ya mkutano wa mwaka wa XXV wa Shule za Kikatoliki, ambao ulianza Jumanne, Septemba 4 katika shule ya masista wa Antoniane huko Ghazir.

Mwaka huu mkutano utajikita  katika  masuala ambayo yanaweka katika hatari mwendelezo wa uwepo wa shule za kikatoliki katika muktadha wa sasa nchini Lebanon. 2005-2018 angalau taasisi 24 za elimu za Kikatoliki zilifungwa, na miaka miwili iliyopita kunaonekana matarajio ya kufilisika kwa  hali ya baadaye ya kuongezeka kwa idadi ya shule zinazoendeshwa na mashirika ya dini.

Ni hali inayofanya uchumi usiwe endelevu kwa mwendelezo wa huduma za elimu zinazotolewa na shule nyingi za  Kikatoliki kama ilivyothibitishwa na washiriki wote wa mkutano. Ilikuwa sheria ya mwaka  2017 kisha serikali kuamuru mzunguko wa mishahara "kwa wafanyakazi katika sekta ya umma, ambayo ni pamoja na sekta ya elimu. ongezeko la mshahara lililowekwa na kanuni mpya za serikali, ambazo mara moja zilianza kutumika kwa walimu wa shule za serikali, ambapo zimeonesha tatizo kubwa ambalo bado halijapata kutatuliwa kwa ustawi wa kifedha wa hali halisi ya shule binafsi za Lebanon.

11 September 2018, 09:18