Cerca

Vatican News
Tutunze mazingira kwa ajili nyumba yetu na hata kwa ajili ya wanyama wetu wazuri Tutunze mazingira kwa ajili nyumba yetu na hata kwa ajili ya wanyama wetu wazuri  (AFP or licensors)

COP24, juu ya mabadiliko ya hali ya hewa Desemba 2018, Poland!

Katika Baraza la COP 21 huko Paris Ufaransa yaliwekwa mapendekezo kadhaa kuhusu mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira, lakini hata mwaka huu kuna mapendekezo mengine ambayo nchi zitaleta na kuweka kwenye meza katika Baraza la COP24 mwezi Desemba mwaka huu huko Katowicze nchini Poland

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Hata hivyo katika kusubiri Mkutano wa COP24, Baraza kuhusu kukabiliana mabadiliko ya tabianchi utakao fanyika huko Katowicze nchini Poland mwezi Desemba 2018, Maaskofu wa Italia wanahimiza kuwa na uwajibikaji wa Italia ili kwa mantiki hiyo wanaweza kuchukua nafasi halisi na ya kudumu katika ujenzi wa jamii isiyo kuwa na hewa ya ukaa. Naye Monsinyo Fabiano Longoni, Mkurugenzi wa Ofisi ya Baraza la Maaskofu Katoliki Italia katika kitengo cha matatizo ya kijamii na kazi anasema kuna matendo hai ya kisiasa kwa ngazi ya juu ambao walikuwa wameamua katika Baraza la COP 21 huko Paris Ufaransa, pia  kuna hata mapendekezo mengine ambayo nchi zitaleta na kuweka kwenye meza katika Baraza la COP24 mwezi Desemba mwaka huu.

Sala ya kiekumene: Aidha amesema kuwa ni lazima kusali kwa ajili ya huduma ya viumbe , ndiyo mwaliko kwa wote na hivyo anawaalikwa watu wenye mapenzi mema , waamini wa madhehebu mengine ya kidini na wasio amini,  kuungana kwa pamoja katika suala hili la pamoja , kwa sababu hata maombi ni fursa ya mabadiliko ya kiroho ambayo yanasaidia uongofu wa moyo na hata katika matendo mengine na kutambua kuwa sisi ni viumbe na siyo wamiliki na wala watawala wa lolote, zaidi ya kuwa wahudumu na walinzi wa kazi ya muumba. Kwa maana hiyo fursa hii nzuri ya Siku ya kuombea huduma ya viumbe iwe kwa manufa ya wote na kuanza kwa upya.

Sheria nyingi katika mabara yote duniani kwa ajili ya utunzaji wa mazingira: Kwa kuzingatia sheria nyingi za mazingira, kanuni na viwango vilivyopo na  vinavyoandaliwa katika nchi nyingi katika mabara na hususani za kiafrika, ni busara kufikiria kuingiza vifungu muhimu vya mazingira ndani ya katiba ili kuhifadhi na kusimamia mazingira kwa dhati . Kwa kuzingatia mwamko wa ufahamu wa mazingira katika miongo ya hivi karibuni, mazingira yamekuwa ni suala la kipaumbele katika siasa na katiba nyingi sasa zinatoa hakikisho la “haki ya mazingira bora” pamoja na haki za taratibu zinazohitajika katika utekelezaji na uhimizaji wa haki muhimu zilizotolewa.  Katika nchi nyingi vifungu vya Katiba zao vinavyoainisha haki za msingi za raia, siyo marazote vimekuwa moja kwa moja chini ya uwezo wa raia kuhakiki utekelezaji wake na siyo mara zote vimejenga thibitisho la haki. Hata hivyo mwelekeo wa kimataifa ni katika kuimarisha upatikanaji wa haki zilizoainishwa katika vifungu vyote vyenye mwelekeo huo.

Miji, mitaa, bahari, maziwa kujazwa takataka:  Uzalishaji wa taka upunguzwe, pale inapowezekana taka lazima,kwa kuzingatia kipaumbele, zitumike tena, zizungushwe, zipatikane tena na ziondolewe kwa usalama kwa namna ambayo haitaleta athari kubwa au kama hii haiwezekani kuepukwa, kwa hali ambayo ina uwezekano mdogo wa kuleta athari kubwa. Kwa maana hiyo.

Ni Jukumu la raia kulinda, kuhifadhi, kutunza na kusimamia mazingira na inataka kwamba kila  kila mtu ana wajibu wa kushirikiana na vyombo vya dola na watu wengine kulinda na kuhifadhi mazingira na kuhakikisha maendeleo endelevu ya kiekolojia na matumizi endelevu ya maliasili. Hata hivyo kila nchi pia inapaswa kuchukua hatua stahiki zinazohitajika kuhifadhi na kulinda mazingira ya taifa kwa ajili ya ustawi; na kutafuta ushirikiano na nchi zingine na vyombo vingine kwa ajili ya kulinda uwanda mpana wa kimataifa wa mazingira kwa ajili ya binadamu, kwa maana ni kuhufadhi nyumba ya pamoja. Siku ya kuombea huduma ya viumbe ambayo imewekwa na Kanisa katoliki kila ifikia tarehe 1 Septemba inataka kukumbusha, na kuonesha udhati huo  kwa maana hiyo ni kutaka kweli kuona thamani kuu ya Muumba inatunzwa ipasavyo kwa wema wa wote, yaani nyumba yetu ya pamoja tunamoishi.

Wajibu mkuu wa kutunza mazingira kwa jamii nzima: Hii ni changamoto kubwa kwa wana wa Afrika na haiwezi kuipuuza kwa maana hiy lazima kupania kutimiza wajibu huu wa kutetea na kutunza mazingira kupitia mipango mbalimbali inayotekelezwa na taasisi na mashirika yake yote ya nchi yakiwemo ya kidini ambayo yako mstari wa mbele kuhamasisha kwa dhati kwa kushirikiana na tume na taasis inyingine  na katika kutengeneza mpango ya muda mrefu, katika mtazamo wa kichungaji kwa ajili ya utetezi wa viumbe vya Mungu, katika ubia na Mwavuli unaoungnisha dini na hifadhi.

Ni mwaliko kwa wote  kutoa kipaumbele katika shunguli zao za kila siku , nia au kazi za kutunza mazingira na viumbe katika mtazamo kwamba, hayo ni maagizo na kazi ya Mungu Mwenyewe aliye viumbe vitu vyote vilivyomo duniani na mbinguni. Kwa maana hiyo, kazi hii inafanikishwa kupitia huduma na utoaji wa elimu mashuleni parokiani, vituo vya kiroho na huduma za kijamii kama mipango ya kilimo, ufugaji. Yote hayo yalenge  katika mpango huu, wa kurejesha mazingira bora kwa kila kiumbe, Mazingira Bora hufanikisha afya bora kwa mtu binafsi na hivyo jamii kwa ujumla. Ili kuifanikisha ndoto hii, kila mmoja anapaswa kuwajibika kikamilifu, katika kuhudumia uumbaji wa Mungu.

 

 

01 September 2018, 09:22