Tafuta

Ustawi wa kila nchi  yoyote kama ilivyo Somalia unategemea uwepo wa imani na hatua za pamoja kutoka kwa serikali kuu na wajumbe wa serikali hiyo Ustawi wa kila nchi yoyote kama ilivyo Somalia unategemea uwepo wa imani na hatua za pamoja kutoka kwa serikali kuu na wajumbe wa serikali hiyo 

Amani ya Somalia inahitaji ushirikiano kutoka pande zote!

Somalia, au maeneo yaliyo na uhusiano, uwezo wake wa kuvutia wawekezaji na kutatua migogoro unategemea sana viongozi wa kisiasa nchini humo kuweza kuaminiana na kukubali ajenda moja. Hayo yamesemwa na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Bwana Michael Keating, mjini Kismayo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Somalia, au maeneo yaliyo na uhusiano na umaskani au mabadiliko ya hali ya hewa, uwezo wake wa  kuvutia wawekezaji na kutatua migogoro unategemea sana viongozi wa kisiasa nchini humo  kuweza kuaminiana na kukubali ajenda moja.  Viongozi wa majimbo mbalimbali nchini Somalia wamehimizwa kuimarisha ushirikiano baina ya serikali zao na serikali kuu kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kuweka mazingira ambayo yatakuwa ya manufaa kwa wasomali wote.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Bwana Michael Keating, mjini Kismayo wakati wa mkutano wa Baraza la ushirikiano wa majimbo (CIC) ambao umewaleta pamoja  viongozi wa majimbo ya Puntland, HirShabelle, Galmudgud, na yale ya Kusini Magharibi.

Katika lengo kuu la mkutano huo ni kujadili mbinu za kuendeleza ushirika miongoni mwa majimbo tofauti nchini humo. Bwana Keating akihimiza ushirika huo kwa ajili ya maendeleo  amesema: “Kwa maoni yangu matatizo ya Somalia, au yanao uhusiano na umaskani au mabadiliko ya hali ya hewa, uwezo wake wa  kuvutia wawekezaji na kutatua migogoro unategemea sana viongozi wa kisiasa nchini humo  kuweza kuaminiana na kukubali ajenda moja”. Akiendelea ameongeza kusema:  “kwa hivyo hii ni sehemu moja muhimu ya hali halisi.” Kwa kukazia zaidi amesema “ bila ya Somalia kuna mashakani ikiwepo pia  ni ushindi kwa pande zote  pamoja na mamilioni ya watu ambao wanastahili kuwa na maisha bora, kwani mafanikio na ustawi wa kila nchi  yoyote kama ilivyo Somalia unategemea uwepo wa imani na hatua za pamoja kutoka kwa serikali kuu na wajumbe wa serikali hiyo”.

Mjumbe maalum amekariri kuwa  mkutano wa Kismayo unatoa nafasi ya mambo kusogea mbele katika njia sahihi. Pamoja na hayo , masuala mengine yaliyojadiliwa na viongozi hao ni  mabadiliko ya katiba ya nchi, mfumo wa sheria, upitishwaji wa sheria za uchaguzi na pia makubaliano ya kugawana mapato.

Mjini Kismayo pia kuna kituo cha wakimbizi wanao rudi nyumbani kwao ambacho kinafadhiliwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kwa ushirikiano na asasi ya kiraia kama ilie ya  Mercy Corps.  Kituo hicho kinapokea wakimbizi wa Somalia wanaorejea kutokea Kenya, hususan kutoka kambi ya Dadaab iliyo na wakimbizi na wanaotafuta hifadhi,ambao wamesajiliwa takriban watu  200,000.

07 September 2018, 09:03