Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maaarifa ili kuboresha maisha yao. Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maaarifa ili kuboresha maisha yao. 

Vijana fanyeni kazi kwa bidii, juhudi na maarifa, acheni kulalama!

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kama kuna changamoto zinazowakabili vijana katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasiliana na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao. Vijana wajenge utamaduni wa kufa kazi kwa juhudi, bidii na maarifa.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar- Es Salaam.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka vijana wa kitanzania wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika. Amesema kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasiliana na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao. Aliyasema hayo Jumatano, Agosti 8, 2018 wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.

Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii. Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama. Pia Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

 

09 August 2018, 08:40