Upo utaalam wa kutengeneza ramani kwa kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani au Drones. Upo utaalam wa kutengeneza ramani kwa kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani au Drones.  

Mkutano ujulikanao kanzi data FOSS4G2018, unafanyika Tazania

Mkutano ulioandaliwa na kanzi data FOSS4G, Bank ya Dunia, Umoja wa Mataifa na wadau wengine, unatoa fursa kwa washiriki kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu na faida ya kutumia teknolojia katika kuleta maendeleo na kuboresha kanzi data. Mkutano huo mwaka huu unafanyika jijini Dar Es Salaam -Tanzania

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkutano ujulikanao kama kanzi data FOSS4G 2018, unafanyika nchini Tanzania, ambao unajumuisha wataalamu wa ramani mtandaoni, wawakilishi wa serikali mbalimbali, sekta binafsi, vyuo, vijana, na taasisi zisizokuwa za kiserikali.

Mkutano ulioandaliwa na kanzi data FOSS4G, Bank ya Dunia, Umoja wa Mataifa na wadau wengine, unatoa fursa kwa washiriki  kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu na faida ya kutumia teknolojia katika  kuleta maendeleo na kuboresha kanzi data. Miongoni mwa washiriki kutoka Tanzania, ni Khadija Abdullah Ali maarufu kama Malkia wa Drone kutoka Zanzibar, yeye ni mtaalam wa kutengeneza ramani kwa kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani au Drones.

Yeye ameeleza kwa nini ni muhimu kutumia teknolojia hizo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika jamii na kwamba “Teknolojia yaweza kuwa mkombozi wa maendeleo duniani”. Kwa mujibu wa wanaoudhuria mkutano huo kanzi data ni tatizo kubwa nchi nyingi barani Afrika na duniani kote, hivyo uwezo wa kupata taarifa za msingi utasaidia kupima maendeleo kwa siku zijazo.

Ikumbukwe: Hii ni mara ya pili mkutano huu wa kimataifa unafanyika barani Afrika, mara ya kwanza ulifanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2016, na mwaka huu Tanzania. Mkutano ujulikanao kama kanzi data (FOSS4G) 2018, ni Mkutano wa kimataifa wa kutumia ubunifu wa ramani mtandaoni kufuatia picha zilizopigwa na ndege zisizokuwa na rubani au drones, unaendelea jijini Dar es Salaam, ukiwaleta pamoja wadau zaidi ya1000 kutoka nchi mbalimbali duniani na  mkutano huo  wa siku sitautamalizika tarehe 3 Septemba 2018.

31 August 2018, 16:29