Tafuta

Vatican News
Calissita L. Giungrich ameteuliwa kuwa Balozi wa USA mjini Vatican. Calissita L. Giungrich ameteuliwa kuwa Balozi wa USA mjini Vatican.  (ANSA)

Calissita L. Giungrich ameteuliwa kuwa Balozi wa USA mjini Vatican.

MS. Calissita L. Giungrich amethibitishiwa uteuzi wake na Senate ya Marekani kuwa ni Balozi wa Marekani mjini Vatican. Balozi mteule ataanza kutekeleza shughuli na utume wake mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa viongozi wakuu wa Vatican akiwemo Baba Mtakatifu Francisko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. - Vatican.

Senate ya Marekani imeridhia uteuzi wa Calissita L. Gingrich kutoka McLean kuwa Balozi mpya wa Marekani mjini Vatican. Balozi mteule amewahi kuwa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa shughuli za uzalishaji za Kampuni ya Kimataifa ya Gingrich pamoja na kuwa mshauri wa Kampuni ya Arlington, yenye makao yake makuu mjini Virginia, nchini Marekani. Ni mwandishi maarufu sana wa vitabu na mtengenezaji wa sinema. Kwa muda wa miaka ishirini amekuwa ni mwanakwaya maarufu sana katika Madhabahu ya Kitaifa ya Kanisa kuu la “Immaculate Conception” Jimbo kuu la Washington DC. Ms. Calissta L. Gingrich amewahi kuwa msaidizi kwenye Bunge la Wawakilishi na Rais wa Mfuko wa Gingrich unaotoa msaada kwa ajili ya huduma ya upendo!

 

17 October 2017, 15:44