Sr Brambilla:Maisha ya kitawa ni maabara yetu“sisi”
Na Simona Brambilla, MC
Hati ya Mwisho ya kisinodi kuhusu Sinodi inasema kwamba: "Maisha ya kuwekwa wakfu yanaitwa kulihoji Kanisa na jamii kwa sauti yake ya kinabii. Katika uzoefu wao wa karne nyingi, familia za kitawa zimekomaa mazoea yaliyothibitishwa ya maisha ya kisinodi na utambuzi wa jumuiya, kujifunza kuoanisha karama za mtu binafsi na utume wa pamoja. Baraza la Kipapa la Masharika ya kitawa na Vyama vya Maisha ya Kitume, Taasisi za Kidunia, pamoja na Mashirika mengine, Harakati na Jumuiya Mpya zina mchango wa kipekee katika ukuaji wa kisinodi katika Kanisa. Leo hii, jumuiya nyingi za maisha ya wakfu ni maabara ya tamaduni mbalimbali ambazo ni unabii kwa ajili ya Kanisa na kwa ulimwengu”(DF, 65).
Papa Francisko amezungumza mara kadhaa juu ya wito wa kuhama kutoka katika “mimi”hadi ya kufika “sisi” na juu ya hitaji la kukutana "sisi" ambayo ina nguvu kuliko watu walio wachache na (Fratelli tutti, 78) kwamba ni "changamoto ya kugundua na kusambaza "fumbo" la kuishi pamoja" (Evangelii Gaudium, 87), la uzoefu wa ukombozi na uwajibikaji wa kuishi kama Kanisa ambalo ni "fumbo letu " ( Veritatis gaudium kuhusu Vyuo Vikuu vya Kikanisa na Vitivo, 4). Mchakato wa Sinodi umechukua, miongoni mwa mambo mengine, sura ya Mtume Paulo juu ya mwili mmoja (DF, 16, 21, 26, 27, 36, 57, 88) na imetufanya tupate ladha ya kiroh" (EG 268) ya kuwa Watu wa Mungu, waliokusanywa pamoja kutoka katika kila kabila, lugha, watu na taifa, wanaoishi katika mazingira na tamaduni tofauti. Siyo rahisi hata hivyo kwa wabatizawa, fundisho la kijumuiya na historia ya kisinodi na utume (DF, 17.).
Kila kitu kinahusiana, kila kitu kimeunganishwa, kila kitu kimesukana: hiki ndicho kiitikio kinachopatika katika Waraka wa ’ Laudato si’ wa Papa Francisko. Taswira ya mwili inadhihirisha kwa njia iliyo wazi ya uhusiano uliopo kati yetu: sisi viumbe, sisi wanadamu, sisi Wakristo, sisi washiriki wa Mwili wa Kristo ambao ni Kanisa, sisi washiriki wa Mashirika ya Kitawa, Jumuiya ya Maisha ya Kitume, kwa Familia ya kiroho inayohuishwa na karama ya pekee na asilia. Kama vile katika mwili, kila sehemu, kila kiungo, kila seli ya mwili na karama yake ina ushawishi kwa wengine.
Kinachotokea katika sehemu moja ya mwili kina athari kwa ujumla wa mwili wote. Na kile kinachotokea katika mwili wote kama hivyo, kina athari kwa njia fulani kwa kila sehemu yake. Katika karama kwa kile ambacho washiriki huweka ndani yake huzunguka. Kila tendo na neno letu, kila wazo na hisia zetu ni nguvu inayopitia wavu( au mtandao)mnene wa mahusiano yetu, na kumfikia kila mtu, kwa sababu sisi sote tumeunganishwa katika mwili mmoja, kuoshwa kwa damu ile ile ya uzuri hai. Hakuna neno, hakuna ishara, hakuna wazo au hisia isiyoegemea upande wowote: kila usemi muhimu una matokeo, ambayo yanaweza kuwa kuwa bora au mabaya.
Ni ajabu, kwa sababu ya ukweli kwamba sisi sote tumeunganishwa, kwa kiwango kikubwa sana, cha roho, na karama, kile ninachohisiwa, nadhani, kusema, kutenda, shauku, hutolewa kwenye mzunguko wa mwili na huleta matokeo yake, kwa manufaa au madhara. Kusindikizana na mwili, ambao ni kiumbe hai, kuelezea uzalishaji wake, uzazi wake, madhumuni ambayo yalikuja ulimwenguni, inamaanisha kwanza kabisa kusindikizana nayo kuungana tena kwa kuendelea na kile kinachohuisha na uzuri wake. Na inamaanisha kutunza kile kinachozunguka ndani ya miunganisho muhimu.
Karama si mali ya Taasisi, Jumuiya, au Familia yenye upendo. Ni zawadi ya Mungu kwa ulimwengu, ni Roho, na ni Uzima. Taasisi (au Jumuiya, au Familia) na kila dada na kaka ambaye ni mshiriki wake, huipokea kama zawadi ya bure, nguvu muhimu ya kuruhusiwa kutiririka ndani yake yenyewe kwa ubunifu, kwa uhuru, bila shaka kuhifadhiwa au ilipakwa rangi kama kipande cha makumbusho. Kwa maneno ya Papa Francisko: “Kila karama ni ubunifu, siyo sanamu ya makumbusho, hapana, ni ubunifu.” Hii inahusu kubaki mwaminifu katika chanzo asili huku tukijitahidi kukitafakari upya na kueleza katika mazungumzo na hali mpya za kijamii na kiutamaduni. Ina mizizi iliyoimarishwa, lakini mti hukua katika mazungumzo na ukweli. Kazi hii ya kusasisha inazaa matunda zaidi kadiri inavyopatikana kwa kuoanisha ubunifu, hekima, usikivu kwa wote na uaminifu kwa Kanisa” (Hotuba kwa Harakati ya Focolare 6 Februari 2021).
Nguvu ya karama hupitia kila seli ya mwili: kwa kila dada/kaka ni mbebaji na ushuhuda wake. Si hivyo tu. Mwili wa Karamam kama kiumbe hai, una hisia zake, na kati yake hisia ya karama, kuna pua, kwa kutumia maneno ya Papa Francisko tena, kwamba pua inaruhusu kutofautisha harufu ya karama, ya kusikia mdundo wake, kutazama nuru yake, kuonja ladha yake, kutambua mguso wake. Na unapogusana nayo, kuvutiwa nayo na kuifuata, kama mwili, kama kiumbe ni muhimu jinsi gani basi kwamba kiongozi wa Familia yenye sifa kama mchungaji mwema, atembee na kundi wakati fulani mbele, wakati mwingine katikati na wakati mwingine nyuma: mbele, kwa ajili ya kuongoza jumuiya; katikati, kwa kultia moyo na kuunga mkono; kuwa nyuma, ili kuiweka umoja kiasi kwamba pasiwepo mtu aliyeachwa pia, nyuma sana, ili kuiweka umoja, na pia kwa sababu nyingine: kwa sababu watu wana "pua"! (hotuba Assisi, Oktoba 4, 2013).
Mitetemo ya Karama na mwendo wa kiumbe kwa kuitikia kile ambacho ananusa kwake na hisi zake zote huona sio tu jumla ya mitetemo na mienendo ya kila sehemu yake; ni mengi zaidi. Ni kidogo kama kile kinachotokea wakati kwaya nzima na vifaa vyake vinafanya kazi: sio tu kwa jumla wa sauti mbalimbali za ala; bali kuna mengi zaidi. Akizungumza na Makardinali wapya wakati wa Baraza la Makardinali tarehe 30 Septemba 2023, Baba Mtakatifu alipendekeza picha hii kwa usahihi, akiiunganisha na sinodi: “Baraza la Makardinali linaitwa kufanana na okestra ya symphony, ambayo inawakilisha ulinganifu na sinodi ya Kanisa. Pia ninasema kisinodi si kwa sababu tuko kwenye mkesha wa Mkutano wa kwanza wa Sinodi ambayo ina mada hii hasatu, lakini kwa sababu inaonekana kwangu kwamba umoja wa kwaya ambao unaweza kuakisi vizuri tabia ya sinodi ya Kanisa. Maelewano ya kwaya huishi juu ya muundo wa ustadi wa midundo ya vyombo tofauti: kila mmoja hutoa mchango wake, wakati mwingine peke yake, wakati mwingine pamoja na mtu mwingine, wakati mwingine na kusanyiko zima.” Alisema Papa Francisko
Tofauti ni muhimu, ni ya lazima. Lakini kila sauti lazima ichangie katika muundo wa kawaida. Na kwa sababu hiyo, kusikilizana ni jambo la msingi: kila mwanamuziki lazima awasikilize wengine. Ikiwa mtu anajisikiliza yeye mwenyewe, hata sauti yake inaweza kuwa ya hali ya juu, haitafaidika na maelewano; na vivyo hivyo ingetokea ikiwa sehemu moja ya okestra haikusikiliza wengine, lakini ilicheza kana kwamba iko peke yake, licha ya kwamba ilikuwa nzima. Na anayeongoza kwaya au bendi yuko kwenye huduma ya aina hiyo ya miujiza ambayo kila wakati ni ufuatiliaji wa mdundo na kwaya. Lazima asikilize zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, na wakati huo huo kazi yake ni kusaidia kila mmoja wa kwaya au bendi kukuza uaminifu wa ubunifu hadi kiwango cha juu, uaminifu kwa kazi inayofanywa, lakini ubunifu, inayoweza kutoa roho. . kwa alama hiyo, ili kuifanya isikike hapa na sasa kwa njia ya kipekee."
Kiumbe hai ni lazima na daima katika mwendo, kukabiliana na kufanya upya. Wakati harakati, ya marekebisho na upya vinakoma, kifo hutokea. Kwa kumnukuu tena Papa Francisko: "Wale wanaosimama tuli, huishia kuwa wafisadi. Kama maji: wakati maji yapo yametulia, mbu huja, na kuzaa mayai, na kila kitu kinakwenda vibaya. "Kila kitu" (mahubiri katika nyumba ya Mtakatifu Marta, 2 Oktoba 2018). Kiongozi wa Familia ya Watawa anaitwa kurudi na kuzamishwa tena katika uzuri, katika nguvu muhimu inayohuisha "mwili wa uzuri", katika muziki unaouunga mkono, katika asili hai na ya kusisimua ambayo hutoke na huwezekana kuanza tena, ili kuanzishwa tena kwa sasa na uzazi usio na mwisho wa msukumo ambao mtu alizaliwa. Kwa hivyo, kwaya inaweza kujieleza leo kwenye orchestra, ikitoa uhai na roho kwa alama hapa na sasa. Kisha, tukiwa huru kutoka katika miundo, kihisabati na kijiografia ambazo pengine zililemea, mtiririko muhimu wa uzuri unaweza kuachiliwa katika ngoma inayosonga mbele na kuwasha na kuhuisha mwili mzima ambao ni Kanisa na ulimwengu.
*Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Taasisi ya Maisha ya Kitawa na Vyama vya Kitume.