Tafuta

2025.02.02 Mons. Joseph Bato’ora Ballong-Wen-Mewuda, aliwahi kuwa Mhusika wa Idhaa ya Kifaransa-Afrika ya Radio Vatican0(1986-2013). 2025.02.02 Mons. Joseph Bato’ora Ballong-Wen-Mewuda, aliwahi kuwa Mhusika wa Idhaa ya Kifaransa-Afrika ya Radio Vatican0(1986-2013). 

Mons.Joseph Ballong,afariki dunia na alihudumu kwa miaka 34 katika Radio Vatican

Mhusika wa kwanza wa Afrika katika idhaa ya Kifaransa Afrika ya Radio Vatican aliaga dunia tarehe 1 Februari 2025 jijini Roma akiwa na umri wa miaka 76.Sauti yake ilijulikana kupitia kipindi cha “Rendez-vous avec l'Afrique”-"Kukutana na Afrika."

Na Stanislas Kambashi, SJ – Vatican.


Monsinyo Joseph Ballong-Wen-Mewuda, Padre wa Jimbo la Kara nchini Togo, alijitolea miaka mingi ya maisha yake katika huduma ya Kanisa, kama padre na katika Radio Vatican. Kwa muda wa miaka 34, kupitia masafa ya Radio, aliufahamisha ulimwengu kuhusu Papa, Vatican, Kanisa zima na la Afrika, jamii na mengine mengi. Kuanzia 1986 hadi 2013 alikuwa na jukumu Idhaa ya Kifaransa-, ya Radio Vatican, ambayo toleo lake la kila siku lilianzishwa kwa wimbo wa mada 'Rendez-vous avec l'Afrique', 'kukutana na Afrika' kwa sauti yake. Kwa wasikilizaji wengi, “alikuwa mojawapo ya vyanzo vikubwa vya habari zenye kutegemeka.” Mnamo mwaka 2021, katika kuadhimisha miaka 60 ya matangazo ya kila siku ya Radio Vatican barani Afrika, Mons. Ballong alionesha kwamba, katika tasnia kubwa ya habari ya leo, kusambaza habari za kuaminika, sahihi na kuthibitishwa ndiko kulikoifanya Radio Vatican kuwa ya kipekee.

Umaalum wa Kiafrika katika Radio Vatican

Vipindi vya Radio Vatican kwa Afrika vilianza mnmamo mwaka 1950. Lakini hadi mwaka 1961 nchi zilianza kupokea habari za mara kwa mara kutoka kwa Papa na Kanisa la Ulimwengu, makanisa ya mahalia pamoja na vyanzo vingine vya kijamii na kisiasa. Matangazo ya kila siku kwa Afrika yalikuwa ya kawaida kwa Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kiarabu na Kiswahili. Miaka kadhaa baadaye, Kiamhari, Kitigrinya na lugha zingine za Kiafrika ziliongezwa. Matangazo hayo kwa lugha ya Kifaransa hadi Afrika na Madagascar yalianza kipindi cha baada ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, kwa ombi la Maaskofu wa Afrika waliotaka kipindi maalum kwa ajili ya Afrika, kama vile Monsinyo Ballong alivyoeleza mara kadhaa. Mpango huo, kama alivyokumbuka mnamo 2021, ulirekebishwa "ili kuyapa matangazo haya sura ya Kiafrika," ambayo ilikuwa moja ya sababu kwa nini kipindi cha Kifaransa- Afrika kiliitwa "Rendez-vous avec l'Afrique, Kukutana na Afrika.

Padre Bodjoko:Ballong,mtangulizi wa kipindi cha Afrika katika Radio Vatican

Kazi ya “mtangulizi huyo wa Kiafrika” ndani ya tasnia ya habari ya Vatican “itabaki kuwa kumbukumbu katika kumbukizi zetu,” alisema Mjesuti Jean-Pierre Bodjoko, ambaye alimrithi Monsinyo Ballong kama mkuu wa huduma ya Kipindi cha idhaa ya “Kifaransa Afrika” ya Radio Vatican. "Alijumuisha lugha za Kiafrika - Ewondo, Kikongo, Kinyarwanda, Kirundi, Lingala, Malagasi, Tshiluba - katika vipindi vinavyotangazwa na Radio Vatican", alisisitiza Mjesuit wa Congo, akielezea jinsi ambavyo "mtu huyo aliacha alama muhimu na uwepo wake wa Kiafrika kwenye Radio Vatican. Niliweza kuendelea na kazi yake kwa kuendelea kutoa nafasi ya kutosha kwa habari kutoka katika Makanisa ya ndani ya Kiafrika,” aliendelea Padre Bodjoko, ambaye alihusika na huduma ya Idhaa ya ‘kifaransa Afrika’ kuanzia 2013 hadi 2021.

Albert Mianzoukouta,kwa miaka 25 karibu na Monsinyo Ballong

Albert Mianzoukouta, mwandishi wa habari kutoka Congo-Brazzaville, ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa “Semaine Africaine,”Gazeti la Baraza la Maaskofu wa kila Juma la pili la nchi hiyo, alikuwa mmoja wa watu waliofanya kazi kwa muda mrefu na Padre Ballon katika Radio Vatican. "Kwa sisi sote, aliiruhusu Radio Vatican kuashiria umoja wake na uwepo wa Waafrika wenye uthubutu zaidi. Wanaume na wanawake wa Kiafrika walikuja kutumikia Neno la Mungu kwenye masafa ya radio yetu kubwa zaidi ya Kikatoliki, kwa kujitolea kwa uthabiti wa Padre Joseph Ballong. Aliwakilisha bara letu na Kanisa letu kupitia hali ya Kiafrika ya kujitolea kwake kitaaluma.
 

04 Februari 2025, 09:13