Tafuta

2025.02.03 Kardinali Parolin akisalimiana na viongozi walioshiriki katika Mkutano wa kilele wa watoto mjini Vatican. 2025.02.03 Kardinali Parolin akisalimiana na viongozi walioshiriki katika Mkutano wa kilele wa watoto mjini Vatican. 

Kard.Parolin:Sikilizeni wito wa watoto wanaoomba haki!

Makumbusho ya Vatican yaliandaa Dominika jioni tarehe 2 Februari 2025 mkutano kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Haki za Watoto,uliofanyika mjini Vatican.Kardinali Parolin katika hotuba yake alielezea kuwa mkutano huo ni wakati wa kutafakari na kusikilizaji kwa kuheshimiana.Historia imeonesha mara kwa mara kwamba watoto ni miongoni mwa watu walio hatarini zaidi katika jamii.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, tarehe 2 Februari 2025 aliwakaribisha viongozi wa kimataifa na washiriki wengine katika hafla ya mkesha wa Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Haki za Watoto, uliofanyika mjini Vatican. Kuanzia kwa watu mashuhuri wa kisiasa na kiuchumi hadi viongozi wa kitamaduni na raia wa kawaida, sauti za watoto wanaolia dhidi ya njaa, vita, ghasia, ukosefu wa usawa na uharibifu wa mazingira haupaswi kusikika. Ndiyo hakika yalisikika katika ujumbe wa hotuba ya Kardinali Pietro Parolin kwa washiriki. Katika Tukio lililopewa kauli mbiu: “Wapende na Walinde” lilianza rasmi Jumatatu, tarehe 3 Februari 2025, mjini Vatican, kwa uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko asubuhi na wakati wa kufunga jioni. Washindi wa Tuzo ya Nobel, wasomi, waandishi, wachumi, viongozi wa kidini na kisiasa na viongozi wa mashirika ya kimataifa walikusanyika kwa ajili ya tukio hilo linalohimizwa na Kamati ya Kipapa ya Siku ya Watoto Duniani. Mpango ulioanzishwa na Papa Francisko tarehe 20 Novemba 2024, sanjari na kutangazwa kwa mkutano huo.


“Wapende na uwalinde”

Kardinali Parolin alielezea mkutano huo kama wakati wa kutafakari na husikilizaji wa kuheshimiana. Ukigawanywa katika vikao viwili, tukio hilo lilijumuisha hotuba ya ufunguzi na hotuba ya kufunga ya Baba Mtakatifu  Francisko, pamoja na mijadala saba iliyoshirikishwa na wazungumzaji hamsini. Akiakisi mada ya mkutano huo: "Wapende na Uwalinde," alisema kwamba hatua hizi mbili sio tu mapendekezo lakini ya lazima na msingi ambayyo ni kuamuru makubaliano ya ulimwengu wote na kuhamasisha hatua madhubuti na ya pamoja.

Waathiriwa ni watoto zaidi wa vita na uhamiaji

Historia imeonesha mara kwa mara kwamba watoto ni miongoni mwa watu walio hatarini zaidi katika jamii. Licha ya maendeleo ya mawasiliano mamboleo, dunia ya leo hii  bado inakabiliwa na ukosefu wa upendo na ulinzi kwa wanachama wake wachanga zaidi, Kardinali Parolin alibainisha, kuomboleza ukweli wa kusikitisha wa vita vinavyogharimu maelfu ya maisha ya vijana na wasio na ulinzi na machafuko ya kibinadamu yanayoendelea baharini, ambapo wahamiaji - ikiwa ni pamoja na watoto wengi - wanakabiliwa na hatari na kifo.

Uwepo wa wawakilishi wa Kiyahudi na Waislamu

Akirejea Injili, Kardinali Parolin alikumbuka kwamba Yesu aliwaomba wanafunzi wake wahifadhi usafi wa mtazamo mkubwa wa  mtoto na akawaonya dhidi ya kuwadhuru. Kanisa linaendelea kuwa kidete katika utume wake wa kutetea na kudumisha haki za watoto, japokuwa linatambua mapungufu yake yenyewe, akikariri umuhimu wa kuwasikiliza wataalam wa sayansi ya jamii, saikolojia na ualimu, pamoja na mashirika ya kimataifa na wafanyakazi wa nyanja hizo. Pia aliakisi thamani ya mazungumzo ya dini tofauti, na kutoa shukrani kwa uwepo wa wawakilishi kutoka jamii ya Wayahudi na Waislamu, ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Kiyahudi David Rosen na Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb wa Al-Azhar.

Haki ya kucheza kwa amani na uhuru

Tunapotazamia Siku ya Pili ya Dunia ya Watoto, iliyopangwa kufanyika Septemba 2026 kufuatia sherehe ya uzinduzi wake kwa mara ya kwanza mnamo Mei 2024, Kardinali Parolin alihimiza ulimwengu kusikiliza sauti za watoto - hasa kukataa kwao njaa, ukosefu wa usawa, vurugu, vita na uharibifu wa mazingira. Aliomba hatua zichukuliwe ili kushughulikia masuala muhimu yanayowahusu watoto yakiwemo upatikanaji wa rasilimali, elimu, lishe, afya, familia na burudani. "Kila mtoto ana haki ya kucheza kwa amani na uhuru," Kardinali alithibitisha.

Kusonga mbele

Ingawa changamoto ni kubwa, Kardinali Parolin alibainisha kuwa hatua muhimu zaidi ni kuanza kuanzisha michakato ambayo inaweza kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu. Aliwahimiza wale wote wanaohusika kusonga mbele kwa ujasiri na azma, wakiunganishwa na lengo kuu: kuhakikisha kwamba watoto wote wanakaribishwa, wanapendwa na kulindwa.

Kard. Parolin
04 Februari 2025, 10:44