Ask.Mkuu Gallagher:Diplomasia ya tumaini ni muhimu kwa amani!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jubilei ya 2025 na diplomasia ya Vatican vina sababu moja inayoitwa "tumaini" ndivyo alianza kujieleza Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, ambaye tarehe 27 Januari 2025 akiwa huko Ufalme wa Monaco, alikutana na mapadre, wanaohusika na huduma za majimbo, na watawa wa kike na kiume. Mkutano huo ulifanyika katika kikanisa cha Huruma cha Askofu Mkuu mahalia, katika hitimisho la ziara ya siku mbili ya Askofu Mkuu,huyo kwa mwaliko wa Mfalme Albert II katika maadhimisho ya mtakatifu Devota anayeheshima huko. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu baadaye aliongoza adhimisho la Ekaristi katika Kanisa Kuu Bikira Maria hasiye na doa. Kisha, alikutana na mapadre huku akikumbuka kaulimbiu ya Jubilei ya matumaini, na kuakisi jinsi wakati wa vita vinavyoendelea na tishio linaloongezeka la vita vya ulimwengu ambavyo Papa Francisko mara nyingi hurejea katika Mwaka Mtakatifu wa sasa unaotaka kuwa jibu la kiroho kwa maovu ya muda ambayo yanakumba nchi nyingi. Na ni katika mtazamo huo ambapo Vatican, pamoja na hatua zake ya kidiplomasia, inatazama kwa huruma mateso ya ulimwengu, inakabiliana nayo kwa huruma, inasikiliza mahitaji na kupendekeza suluhisho za kibunifu za kutatua migogoro, iwe Ukraine, Mashariki ya Kati au Mashariki ya Caucasus au Yemen."
Maneno askofu Mkuu hayakukosa kurejea majanga yanayoshuhudiwa katika bara la Afrika, hususan katika nchi za Sudan, Sahel, Pembe ya Afrika, Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Maeneo yote yaliyoathiriwa na dharura kubwa za kibinadamu, shida ya hali ya hewa na, wakati mwingine, na tauni ya ugaidi. Lakini zaidi ya usimamizi wa migogoro, kazi ya diplomasia ya upapa inalenga katika kanuni za msingi kama vile amani, udugu, ushirikiano wa pande nyingi, ulinzi wa Uumbaji, udhibiti wa mtiririko wa watu wanaohama, uchumi wa haki, mapambano dhidi ya biashara haramu na utetezi wa haki za binadamu. Kiini cha hotuba ya Askofu Mkuu Gallagher pia kilikuwa rejea ya dhamana ya uhuru wa kidini, mojawapo ya masharti ya chini ya kuishi kwa heshima" na bila ambayo "amani ya kweli inabakia nje ya kufikiwa. Askofu Mkuu kisha akakumbuka maombi mengi na ya kuendelea, pamoja na mipango ya Papa Francisko kukomesha migogoro duniani: "Jambo la msingi sio ufanisi wa haraka wa miito hii lakini ni kitendo cha kuzipa jina vita na migogoro, ili zisizame katika usahaulifu na wahanga kuweza kufaidika na umakini na mshikamano wa kimataifa.”
Kwa sababu nyuma ya takwimu kuna maisha na hatima ya binadamu iliyoharibiwa. Vita havitakwisha kamwe, lakini ukweli rahisi kwamba vinatajwa, kwamba macho ya ulimwengu yanakazia kwao, hata ikiwa ni kwa muda mfupi tu, husaidia kuzipa mwelekeo wa kibinadamu.” Katibu wa Mahusiano na Mataifa alitoa tafakari maalum kuhusu suala la uhamiaji na akisisitiza ombi la Papa la kutobadilisha bahari ya Mediterania , bahari yetu Askofu Mkuu Gallagher alihimiza kukaribishwa kwa kaka na dada hao katika ubinadamu wanaobisha hodi milango yetu, mara nyingi huleta talanta na nguvu. Ukarimu"unaozingatia kuheshimu sheria na usawa wa kijamii na kiutamaduni, aliongeza Askofu Mkuu,na lazima pia kuangalia ushirikiano na nchi za asili za wahamiaji ili kuruhusu wakazi wao kuishi kwa heshima katika ardhi yao wenyewe, kama raia huru na waliotimilika.
Kwa hivyo basi, wito wa Askofu Mkuu kulinda hadhi ya binadamu ya kila mtu, kufungua njia ya kuelekea kwenye hatima ya baadaye iliyo salama na kwamba “Hakuna mwanadamu anayepaswa kuhisi hatia kwa ajili ya maisha yaliyopo na hakuna mzee au mgonjwa anayepaswa kunyimwa tumaini au kukataliwa.” Katika muktadha huu diplomasia ya Vatican inayooneshwa na matumaini na huruma, inakuwa kioo cha mshikamano, nguvu ya hatua ya maadili, na dira inayoongoza dhamiri. Na ikiwa inaendeshwa na utetezi wa manufaa ya wote, kiukweli, inatafuta kukuza maadili, badala ya kulinda maslahi fulani. Na malengo haya yanaweza kutafsiriwa katika vitendo madhubuti, kama vile: "Kusaidia kufutwa kwa deni la nje la nchi masikini zaidi, kukuza mabadiliko ya haki ya kiikolojia, kusaidia maendeleo fungamani yanayoweza kufikiwa na wote, kutekeleza sera ya kimataifa ya upokonyaji silaha na kutafuta suluhisho la kudumu kwa migogoro.
Askofu Mkuu Gallagher alisema kuwa “Msingi wa mbinu hii, ni utamaduni wa kukutana ambao hutengeneza mitandao, huhimiza mazungumzo hata kati ya wapiganaji, hata wawe nani, na hujitahidi kutatua migogoro bila kuwadhalilisha walioshindwa, kuweka misingi, kwa amani ya kweli ya haki na ya kudumu. Kwa hiyo, matumaini ya Katibu wa Mahusiano na Mataifa yalikuwa kwamba mkakati huu, muhimu katika ulimwengu unaozidi kuvunjika, ungeweza kupitishwa na kuimarishwa kwa kiwango kikubwa zaidi, pia kwa ushirikiano na Kanisa la mahali na kupitia diplomasia ya matumaini kwa kuzingatia nguzo nne: kweli, msamaha, uhuru na haki.