Tafuta

Maadhimisho ya miaka 80 ya ukombozi wa kambi ya kifo ya Auschwitz-Birkenau nchini Poland. Maadhimisho ya miaka 80 ya ukombozi wa kambi ya kifo ya Auschwitz-Birkenau nchini Poland.  (Copyright (c) 2025 Shutterstock. No use without permission.)

Ask.Mkuu Gyhra,OSCE:Kuelimisha amani ni ufunguo wa kutokomeza ubaguzi

Vatican inapenda kueleza matumaini kwamba Siku ya Kumbukizi ya Maangamizi ya Wayahudi kwa 2025 inaweza kutoa mchango katika kufundisha vizazi vya sasa na vijavyo umuhimu na yenye ufanisi kwa ajili ya kukuza amani na heshima ya kweli ya binadamy.Alisema hayo Mwalikishi wa Kudumu wa Vatican wa OSCE katika Mkutano wa Baraza la Kudumu katika kumbukizi la miaka 80 ya kukombolewa kwa Kambi ya Auschwitz-Birkenau na vifo vya Wahahudi kunako 27 Januari 1945.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican alitoa hotuba yake katika kikao cha  1506 cha Baraza la Kudumu la Usalama wa Nchi za Umoja wa Ulaya (OSCE ) tarehe 30 Januari 2025 kufuatia na hotuba ya Mwenyekiti wa Muungano wa Kimataifa wa Ukumbusho wa Maangamizi ya Wayahudi (HRA) katika kumbukumbu ya miaka 80 ya ukombozi wa kambi ya maangamizi ya Auschwitz-Birkenau, yaliyotendekea kunako tarehe 27 Januari 1945. Katika hotuba Askofu Mkuu Richard Gyhra, alimshukuru Mwenyekiti wa Muungano wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi kwa hotuba yake kwenye Maadhimisho hayo. Siku hii ya ukumbusho inatimiza dhumuni mazuri la kuhakikisha kwamba mateso ya kutisha na ya kinyama na uangamizaji ulioratibiwa dhidi ya Wayahudi na utawala wa kinazi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia hautasahaulika.

Mamilioni ya Wahahudi waliangamizwa

Kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosisitiza: "kumbukumbu na kulaaniwa kwa maangamizi hayo ya kutisha ya mamilioni ya Wayahudi na wale wa imani nyingine yaliyotokea katika nusu ya kwanza ya karne iliyopita, itusaidie sote kutosahau kwamba mantiki ya chuki na vurugu kamwe isihesabiwe haki, kwa sababu inakanusha ubinadamu wetu wenyewe.” Kwa hakika, kukumbuka matukio yaliyopita sio tu kwamba husaidia kuzuia makosa yale yale yasijirudie, bali pia huwezesha kumbukumbu, kama tunda la uzoefu, kuwa msingi na msukumo wa maamuzi ya sasa na yajayo yanayoelekezwa kwenye amani. Mnamo 2014, OSCE ilitambua ukumbusho na elimu ya Maangamizi ya Wayahudi kama hatua muhimu za kuimarisha juhudi za pamoja za kupambana na kuzuia chuki dhidi ya Wayahudi katika maeneo yetu yote. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba maonyesho ya chuki dhidi ya Wayahudi yanaendelea kuongezeka mashariki na magharibi mwa Vienna.

Lazima kupinga aina zote za zamani na mpya juu ya chuki dhidi ya Wayahudi

Vatican kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kudumu anaibisha kuwa,  inasikitishwa sana na mwenendo huu na inasisitiza msimamo wake usio na shaka dhidi ya aina za zamani na mpya za chuki dhidi ya Wayahudi. Kuhusiana na hili, Papa Francisko anaendelea kulaani vikali matamshi haya yanayokua ya chuki dhidi ya Wayahudi, ambayo yanaathiri ongezeko la idadi ya jumuiya za Wayahudi duniani kote. "Kuelimisha kwa ajili ya amani" ni ufunguo wa kimsingi wa kutokomeza janga hili, pamoja na kujitolea kwa jamii ya "udugu na kukubalika kwa wengine", kwa kukumbuka siku za nyuma kwa ufahamu mkubwa wa kihistoria. Kuvielimisha vizazi vya sasa na vijavyo kwa uelewa mzuri wa sababu zilizopelekea Shoah na ukatili mwingine usiohesabika ni dawa ya lazima katika wimbi hili la chuki ambalo bado tunalishuhudia. Kwa kuzingatia hayo, Vatican inapenda kueleza matumaini yake kwamba Siku ya Kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi mwaka huu inaweza kutoa mchango mkubwa katika kufundisha vizazi vya sasa na vijavyo masomo muhimu na yenye ufanisi kwa ajili ya kukuza amani na heshima ya kweli kwa utu wa kila mtu.


Uchaguzi wa Katibu Mkuu wa Baraza la OSCE, Mhes Feridun Sinirlioğlu

Na wakati huo huo, Askofu Mkuu Richard Gyhra, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya(OSCE),katika kikao hicho hicho, kufuatia na matamshi ya Uzinduzi ya Katibu Mkuu mpya wa OSCE, alitoa hotuba fupi akiomba aruhusiwe kuongeza sauti yake “kwa wale wazungumzaji waliotangulia katika kumkaribisha kwa moyo mkunjufu katika Baraza la Kudumu la Usalama Barani Ulaya (OECE), Katibu Mkuu mteule wa Shirika letu, Mheshimiwa Feridun Sinirlioğlu, na kumshukuru kwa matamshi yake mwanzoni mwa mamlaka yake. Askofu Mkuu alisema anashika usukani wa Ofisi hiyo muhimu katika kipindi ambacho kinaweza kuchukuliwa kuwa mojawapo ya vipindi vyenye changamoto nyingi katika historia ya Shirika lao. Eneo la OSCE bado limezama katika migogoro ya wazi kati ya Mataifa yanayoshiriki. Zaidi ya hayo, licha ya kuwa na zana mbalimbali zinazoweza kutumika, Shirika linaendelea kukabiliwa na changamoto katika kukabiliana na migogoro na kutafuta ufumbuzi na maamuzi yanayotokana na mamlaka, maridhiano. Changamoto hizi zinachangiwa zaidi na kutokuwepo kwa Bajeti Iliyokubaliwa, ambayo inahitajika haraka ili kuhakikisha utendakazi mzuri wa OSCE.

Wasiwasi wa Vatican kuhusu migawanyiko inayokua 

Vatican inatazama kwa wasiwasi mgawanyiko unaokua na migawanyiko ambayo inaficha mizizi ya OSCE na kuathiri kazi yake ya kila siku." Kwa hakika, mgawanyiko na migawanyiko hiyo sio tu kwamba inahatarisha kudhoofisha uaminifu na mamlaka ya Shirika letu, lakini pia ni tishio la kweli kwa uwepo wake. Hata hivyo, mafanikio ya hivi majuzi ya OSCE katika kufikia maafikiano kuhusu nafasi 4 za Juu na Uenyekiti-katika Ofisi ya 2026 yanaonyesha uwezo wake wa kudumu wa kushinda migawanyiko.” Hii inathibitisha kwamba maendeleo yanaweza kufikiwa wakati kuna dhamira ya kweli ya ushirikiano na maelewano. Katika mwaka huu ambao tunasherehekea Maadhimisho ya Miaka 50 ya Sheria ya Mwisho ya Helsinki, ni wakati mwafaka kwa Mataifa yanayoshiriki "kurejesha 'roho ya Helsinki.'" Tunahitaji kukua katika maelewano na azimio la kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi na kujenga OSCE imara zaidi. Hii itahitaji uvumilivu na nia ya kushirikiana na wote. Kwa kumalizia, ningependa kumhakikishia Mheshimiwa wa Kiti Kitakatifu msaada wa kujenga kwa kazi yako, kama Katibu Mkuu, na kutoa matashi  yake mema anapochukua majukumu yake mapya.

 

31 Januari 2025, 10:26