Papa Francisko amekutana na Rais wa Congo,Bwana Denis Sassou-N’Guesso
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya Habari mjini Vatican, Jumatatu tarehe 25 Novemba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana katika Jumba la kitume na Raisi wa Jamhuri ya Congo, Bwana Denis Sassou-N’Guesso, ambapo mara baada ya mkutano huo, vile vile amekutana na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizwa na Askofu Mkuu Miroslaw Stanislaw Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Masuala ya kisiasa , kijamii na kiuchumi
Wakati wa Mkutano wao, na Sekretarieti ya Vatican, wameibua uhusiano mwema uliopo kati ya Vatican na Jamhuri ya Congo na kujikita juu ya baadhi ya mantiki ya hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi, hasa juu ya ushirikano na Kanisa mahalia katika muktadha wa Elimu, Afya na Utunzaji wa mazingira. Katika mazungumza yakiendelea aidha walibadilishana maoni juu ya mada zenye tabia ya kikanda na kimataifa, huku wakisisitiza umuhimu wa kuhamasisha mazungumzo na maridhiano kati ya nchi.