Tafuta

2024.11.22:Kardinali  Pietro Parolin akiwa chuo Kikuu "Lumsa" (22-11-2024). 2024.11.22:Kardinali Pietro Parolin akiwa chuo Kikuu "Lumsa" (22-11-2024). 

Kard.Parolin:Kuna wasiwasi wa kuongezeka vita nchini Ukraine

Akiwa pembezoni mwa uwasilishaji wa kitabu huko Lumsa,Katibu wa Vatican hakutoa maoni juu ya hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Netanyahu:“Tuna nia ya kumalizika kwa vita hivi karibuni.”Kuhusu maneno ya Papa Juu ya “mauaji ya kimbari huko Gaza:“Papa alisisitiza msimamo wa Vatican,kuna vigezo vya kiufundi vya kufafanua dhana hii."Na suala la chuki dhidi ya Wayahudi:“Sisi daima tuko wazi juu ya jambo hilo tumelilaani na tutaendelea kulaani.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican. 

Hakuna maoni kutoka Vatican kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kutoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu kwa uhalifu wa kivita, badala yake wito wa nguvu umetolewa kwa kuzingatia kuongezeka kwa mvutano katika mzozo wa Ukraine, ili kuacha kabla ya kufika mahali ambapo siyo rahisi  kurekebishwa. Kisha ilikuwa ni kutoa maoni juu ya maneno ya Papa ya kuweza  kuchunguza ikiwa tendo la Gaza, ambapo idadi ya waathiriwa ilizidi elfu 44, inaweza kusadikiwa kama “mauaji ya ya Kimbari. Kwa njia hiyo Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican aliibu maswali juu ya umuhimu wa sasa wa migogoro inayotikisa ulimwengu kwa waandishi wa habari aliokutana nao tarehe 22 Novemba 2024, kando ya uwasilishaji wa kitabu katika Chuo Kikuu cha LUMSA chenye kichwa: “Utunzaji wa kichungaji wa upweke. Pendekezo jipya” kilichoandikwa na  Profesa Matthew Forde.

Hofu kuhusu Ukraine

Kuhusu hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, Kardinali alieleza kwamba Vatican “imezingatia kile kilichotokea” na kwamba “kinachotutia wasiwasi na kinachotuvutia ni kwamba vita vikomeshwe hivi karibuni.”  Wasiwasi huo pia unatumika kwa Ukraine baada ya kurusha makombora ya masafa marefu yaliyotengenezwa na Uingereza na Marekani katika ardhi ya Urusi na vitisho vya Rais Vladimir Putin kuhusu mzozo ambao unaweza kuenea duniani kote. “Hebu tuache sasa kwa kuwa tuna wakati, kwa sababu hatujui ni wapi ongezeko hili litasababisha!” alishangaa Kardinali Parolin, akifanya kama “mfasiri wa mawazo na wasiwasi wa Papa.” Wakati fulani hatutajua tena jinsi ya kudhibiti uwezekano wa maendeleo ya hali hii, na hivyo akatoa wito “kwa wale walio na jukumu waache kabla ya kufikia yasiyoweza kurekebishwa.”

Hatua ya kubadilishana wafungwa na kurudi kwa watoto inaendelea

Alipoulizwa kama huu ni wakati mbaya zaidi wa mzozo nchini Ukraine, Katibu wa Vatican alibainisha:  “sidhani kama kumekuwa na wakati mzuri zaidi, hakika matukio haya yanatia wasiwasi sana, kwa sababu hatufanyi na sijui yanaweza kutuongoza wapi. Vatican, inaendelea kuwa karibu na nchi "iliyoteswa" kwa kuendelea kuchukua hatua za kidiplomasia kwa kubadilishana wafungwa na kurudi kwa watoto wa Ukraine waliopelekwa Urusi kwa nguvu. Hakuna sasisho juu ya hatua hii, lakini “kwa upande wetu kuna hamu ya kuendelea” alisema Kardinali Parolin na kwamba “Siku zote imekuwa ikifanywa sio tu kwa faida yenyewe ya mpango huu lakini pia kuandaa msingi kidogo wa kufikia mazungumzo.”

Kulaani chuki dhidi ya Wayahudi

Hata juu ya suala la chuki dhidi ya Wayahudi, Kardinali alikumbusha kwamba “msimamo wa Vatican daima  uko wazi": “Hakuna haja ya kufanya mazingatio zaidi. Daima tumekuwa tukilaani na tutaendelea kulaani na tutajaribu kuweka masharti hayo, kwa kadiri tunavyohusika, ili kweli kuwe na laana kali na mapambano makali dhidi ya jambo hili.”

Tafakari 2 kuhusu Papa Benedikto na Papa Francisko

Wakati wa kutoa tafakari Kardinali  Parolin alijikita na  mitazamo fulani juu ya mada hiyo, akinukuu mafundisho ya Mapapa wawili wa mwisho. Papa Benedikto wa XVI kwanza kabisa, ambaye aliona “kuwa katika nchi zilizo na maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa asili ya aina mpya za ugonjwa wa akili, wataalam pia wanatambua athari mbaya ya shida ya maadili. Hii huongeza hisia za upweke, kudhoofisha na hata kuvunja aina za jadi za mshikamano wa kijamii, kuanzia na taasisi ya familia,” alisema Papa wa Bavaria Kwa upande wa Papa Francisko, Kardinali alisema “katika Bunge la Ulaya mnamo 2014: “Moja ya magonjwa ambayo ninaona kuwa yameenea sana Ulaya leo hii ni upweke, mfano wa wale wasio na uhusiano. Inaonekana hasa kwa wazee, mara nyingi ambao huachwa hatima yao na vile vile kwa vijana.” Kwa  njia hiyo uzinduzi wa huduma ya kichungaji ya upweke, ulisisitizwa na Kardinali Parolin, kwamba “unaendana kikamilifu na mafundisho ya Papa Francisko yenye sifa ya msisitizo mkubwa wa 'huruma'. Na kuwasaidia walio peke yao ni tendo la huruma, kama vile kuleta msaada kwenye vitongoji.” Lakini “Je, si watu wangapi wapweke, kwa maana ya walio pembezoni;  je, huduma ya kichungaji ya upweke haiwezi kuwajumuisha? Kwa hiyo ni tumaini la Papa Francisko kwa Kanisa linalitoka nje kwenda kukutana nao, na ndiyo  utimilifu wa tumaini.”

22 November 2024, 17:27