Tafuta

2024.11.23:Mkutano wa Kitaifa wa Vyombo vya habari katoliki huko Bangalore nchini India. 2024.11.23:Mkutano wa Kitaifa wa Vyombo vya habari katoliki huko Bangalore nchini India. 

Dk.Ruffini:jinsi gani maendeleo ya AI katika mawasiliano yanaweza kutusaidia kuwa wanadamu zaidi?

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Dk Ruffini ametoa hotuba yake katika mkutano wa Kitaifa wa Vyombo vya Habari kuhusu “Mwangaza.Kukuza Uwakili wa kidijitali huko Bangalore tarehe 23 hadi 24 Novemba 2024.“Mawasiliano yanaweza kuwa njia ya kujenga ulimwengu bora au yanaweza kuendeleakuchochea kutokuelewana, chuki,uadui.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mawasiliano yanaweza kuwa njia ya kujenga ulimwengu bora; au yanaweza kuendelea kuchochea kutoelewana, chuki na uadui ndivyo alisisitiza Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano akiwa katika Mkutano wa kitaifa wa Vyombo vya Habari Katoliki nchini India kuhusu  “kuangaza. Kukuza Uwakili wa Dijitali” huko Bangalore”tarehe 23-24 Novemba 2024 kwa ajili ya Makleri, Watawa Kike na Kiume na Waliowekwa wakfu tu. Katika hotuba yake Dk. Ruffini alionesha furaha kubwa kuwa pamoja nao. Alisema kwamba “Katika mkutano huu wa mabadiliko, ambao umeundwa kwa uangalifu sana ni jinsi gani: “Tunavyoishi katika kipindi cha wakati. Mapinduzi yanafanyika katika ulimwengu wa mawasiliano. Hivyo tunahitaji kushiriki wazo lolote na juhudi zozote ili kuunda wakati wetu. Huu ni wakati wetu.” Kama Papa Francisko alivyoandika, akiwanukuu wanafalsafa wa Kiitaliano na mtaalimungu Romano Guardini, Dk. Ruffini aliongeza “kuwa hatuishi katika wakati. Sisi ni wakati wetu. Tunautengeneza. Kwa hiyo  “kupitia kile tunachofanya na kupitia kile tunachoshindwa kufanya.” Sio tu suala la kupiga mbizi katika bahari ya kidijitali. Bahari ya kidijitali isingekuwepo bila sisi. Mitandao ya kijamii isingekuwepo bila watu. Akili ya mnemba isingekuwepo bila takwimu(data). Na sisi, maisha yetu, ni data. Ukweli haupo ikiwa haujaambiwa, au kukataliwa.”

Dk. Ruffini alisisitiza kwamba ni “Ni juu yetu kuunda ulimwengu. Na kufanya hivyo kushiriki ukweli, nzuri na bora. Kushiriki ni neno kuu. Sisi, pamoja tukiwa tumetengena, sisi wanachama tunaweza kuwa mtandao mkubwa zaidi wa kushirikisha historia na vitendo, ukweli na uhusiano unaotegemea ukweli.? Je, tunaweza kusimulia historia za siku hizi? Je, tunawezaje kukabili ukuaji huu wa kifafanuzi na muhimu sana - lakini wakati huo huo kwa njia ya kutisha ambayo inaweza hata kudhuru - ukuaji wa mifumo ya akili mnemba bila kupoteza ubinadamu wetu, lakini badala yake kuwa watu wazima zaidi kama wanadamu? “Dk Ruffini aliendelea kusema “Swali ni kwa jinsi gani Akili Mnemba katika mawasiliano inaweza kutusaidia kuwa wanadamu zaidi au inaweza kutusukuma kudhalilisha ubinadamu wetu? Ni kwa njia zipi chombo hiki kitafanya uhusiano kati ya watu binafsi kuwa imara zaidi, na wa kweli, na jamii kuwa na mshikamano zaidi... na kwa njia gani nyingine, itaongeza upweke wa walio tayari kuwa wapweke, na kumnyima kila mmoja wetu uchangamfu kwamba mawasiliano ya kweli pekee yanaweza kutoa. Swali ni ikiwa lengo kuu bado ni kuwezesha maisha kamili zaidi kwa kila mwanadamu au badala yake imekuwa madai ya kusanifisha, kuhalalisha na udhibiti wa kutoweza kurudiwa kwa kila historia.”

Kwa njia hiyo Mkuu wa Baraza la Kiupapa alisema kwamba “Swali   liko katika uwezekano au kutowezekana kwa kufanya kazi ili akili Mnemba ilete usawa zaidi na sio badala yeke kujenga tabaka mpya; matabaka mapya kulingana na utawala wa habari; kukubali kama aina mpya zisizoepukika za unyonyaji na ukosefu wa usawa, kulingana na umiliki wa midundo yake (algorithms) na uchambuzi wa data kutoka katika mgodi usio na mwisho wa maisha yetu. Ipo katika kuweka au kutoweka sheria na mipaka; kwa mfano, kwenye uwekaji takwimu za Injini ya utafutaji na uwekaji data   algorithms zenye uwezo wa kuinua au kufuta watu na maoni, historia na tamaduni; kulingana na vigezo visivyohusiana na ukweli. Kwa hivyo swali la msingi ni juu ya wanadamu sio mashine, uhusiano kati ya wanadamu sio algorithms.” “Na sio swali la kufikirika tu” alisisitiza. “Inahusu maisha yetu, uhuru wetu, hiari yetu. Inahusu uwezo wa wale wanaodhibiti mifumo ya kukokotoa, inahusu uhusiano kati ya wale wanaohesabu na wale ambao licha ya wao wenyewe wamehesabiwa, inahusu vigezo vya kuhesabu, inahusu kikomo kati ya kile kinachoweza kuhesabiwa na kisichoweza; kwa sababu sio idadi: kwa sababu ni ya kipekee, na kwa sababu haina kikomo. Je, tuko tayari kukabiliana na changamoto hii? Sote tunajua umuhimu wa njia za mawasiliano ili kupata yaliyo bora kutoka kwa kila mtu. Mawasiliano yanaweza kuwa njia ya kujenga ulimwengu bora; au yanaweza kuendelea kuchochea kutokuelewana, chuki, uadui. Hakuna uwekezaji ni mkubwa sana kwa kueneza ukweli na kuchochea mienendo ya wema katika hadithi yetu.”

Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aidha alieleza anavyofahamu baadhi ya changamoto nyingi ambazo wanakabiliana nazo kama Wawasilianaji wa Kanisa nchini India. Kwa njia hiyo alirudia kusema kwao maneno ambayo Baba Mtakatifu anatuambia kila siku kwa: Msife moyo. Sote tuko kwenye mtumbwi mmoja.” Katika makaazi ya mageuzi ya vyombo vya habari yaliyomfanya Baba Mtakatifu kuunda Baraza la Mawasiliano la Kipapa  ni hitaji la harambee na ushirikiano. Kwa hiyo Dk. Ruffini alisema “Na leo niko hapa kuunga mkono na kuhimiza harambee na ushirikiano huu. Mfano mmoja kama huo, ni mkutano huu wa leo.” Kwa hiyo aliwahimiza kwamba ni juu yao kujitolea kwa dhati katika kujenga mawasiliano yenye msingi wa uhusiano na ubinadamu ili kupambana na virusi vya mgawanyiko. Mawasiliano kulingana na mtandao ambao ni wa kimataifa na wa ndani wa  Kidijitali  na halisi. Katika wakati ambapo wengi wanajaribiwa kujenga mnara mpya wa Babeli, tumeitwa kutumikia muujiza huu wa umoja katika utofauti. Tunahitaji kusaidiana ili kuifanya ifanye kazi. Wakati umefika wa kuyafanya. Mawasiliano ya kidijitali huturuhusu kuunganishwa kwa njia ambayo haikujulikana hapo awali. Kuwa na vijana  kama wahusika wakuu. Ni uhakika wa Dk. Fuffini kwamba kutoka katika Mkutano huo utatoa njia zinazofaa za kuunda jumuiya, jukwaa, la kushirikiana na kushirikishana. Mkutano huo ni uwanja wa ushuhuda wao, kama wawasilishaji, kama mtandao wa wawasiliani wa kidini, na Ndiyo maana  yeye alikuwa hapo pamoja nao, Alihitimisha.

23 November 2024, 16:42