Mons.Samuele Sangalli ni Katibu Mwambata,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji!
Vatican News
Jumanne tarehe Mosi Okotba 2024, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Samuel Sangalli kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji katika dhamana ya Mkuu wa Utawala wa Baraza hilo la Uinjilishaji, katika Sehemu ya Uinjilishaji wa Makanisa ya Kwanza mahalia.
Mons. Sangalli alizaliwa huko Lecco nchini Italia tarehe 10 Septemba 1967. Baada ya kujiunga na Seminari ya Askofu Mkuu wa Milano akiwa na umri wa miaka 14, alipewa daraja la Upadre Jimbo kuu la Milano mnamo tarehe 8 Juni 1996 na Kardinali Carlo Maria Martini.
Mafunzo
Alipata: shahada ya Sayansi ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Roma Tre; Shahada ya Uzamivu ya Falsafa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian; Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Kiroho katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Kitaalimungu na Taasisi ya Kipapa ya Kiroho Teresianum huko Roma. Ni Profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na Chuo Kikuu Huria cha Kimataifa cha Mafunzo ya Jamii Guido Carli jijini Roma. Tarehe 25 Aprili 2023, Papa Francisko alimteua Monsinyo Sangalli (hadi wakati huo kuwa afisa katika Baraza la Kipapa la Maaskofu) kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya.