Tafuta

Sinodi ya Maaskofu Sinodi ya Maaskofu 

Sinodi,Kard.Grech:Mhusika Kkuu wa Sinodi ni Roho Mtakatifu!

Kiukweli,Sinodi inaweza kuwa sala tu,liturujia,ambayo muhusika mkuu sio sisi,lakini Roho Mtakatifu.”Alisema hayo Katibu Mkuu wa Sinodi tarehe 30 Septemba wakati wa kuanza Mafungo kwa washiriki wa Sinodi. Kwa upande wake kardinali alisema “lazima tuwe tayari kuvua nguo, kwani kusikiliza ni hatua kali ya kuvua nguo mbele ya wengine na mbele za Mungu”.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Hatimaye Mchakato wa maandalizi ya Sinodi umefikia hatua muhimu sana hasa kuwanza na Mafungo, ambapo washiriki wote kutoka Duniani kote wako mjini Vatican. “Ingawa tunatoka katika Makanisa mbalimbali ya mahali pamoja, wote wakiwa na utajiri wao, wote pamoja na changamoto zao, wote wamejitolea kujipyaisha na kutafuta njia mpya na lugha mpya ya kuzungumza juu ya Yesu kwa wanaume na wanawake wa siku hizi, ‘tumeketi pamoja’ kuhifadhi mali za Kanisa kwa njia ya urithi usiogawanyika na kugawiwa watu wote, bila ubaguzi.” Hivyo ndivyo alisema Kardinali Mario Grech, Katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, katika hotuba ya salamu za mafungo kwa ajili ya maandalizi ya Kikao cha Pili cha Mkutano Mkuu wa XVI unaoendelea katika Ukumbi Mpya wa Sinodi, Jumatatu tarehe 30 Septemba 2024.

“Mkutano wa Sinodi ni 'mahali patakatifu' pa kukutana na Bwana ambaye yuko pale ambapo 'wawili au watatu' wamekusanyika kwa jina lake. Ama tunaingia katika mtazamo huu wa maombi, imani, kukutana na Mungu, au hatuchukui mtindo halisi wa sinodi, hatuishi uzoefu wa sinodi. Kiukweli, Sinodi inaweza tu kuwa sala, liturujia, ambayo mhusika mkuu sio sisi, lakini Roho Mtakatifu,"Kardinali alisema. 

Washiriki wa Sinodi wakiwa katika mafungo ya kiroho
Washiriki wa Sinodi wakiwa katika mafungo ya kiroho

Baba Mtakatifu Francisko anatukumbusha kuwa: “Mabadiliko ya Kanisa bila maombi sio mabadiliko ya Kanisa, ni mabadiliko ya kikundi. Bila maombi sisi siyo kusanyiko la Sinodi bali ni kundi la wajasiriamali wa imani. Maria ni mwanamke wa maombi. Bikira wa Nazareti ni kielelezo cha Kanisa linalosali, linaloshukuru na kuimba utukufu wa Bwana wake. Katika Matendo tunaona Maria akiomba pamoja na Mitume waliokusanyika katika Karamu Kuu wakisubiri zawadi ya Roho Mtakatifu (Mdo 1:14). Maria ni kielelezo cha sala kwetu leo ​​katika kuishi siku hizi kali za Mkutano wa Sinodi. Maria pia ni mwanamke wa Sinodi kwa sababu ya maisha yake anatufundisha kwamba Kanisa,  kama linavyojitokeza kutokana na mafundisho na tafakari ya kitaalimungu ya Papa  Benedikto XVI – si kazi ya mikono yetu, bali ni kazi ya Mungu: Kanisa si zao la matendo yetu, ya kujitolea kwetu, lakini ni kiumbe hai ambacho hukua na kuongezeka kwa njia ya ajabu kwa nguvu ya neema ya Mungu."

Kardinali Grech alisisitiza tena kuwa "Maria ni mwanamke maskini wa Bwana, ambaye anajua jinsi ya kukaribisha kila kitu kutoka kwake kama zawadi na neema. Katika ujauzito wake akiwa bikira tunaona ishara fasaha zaidi ya ukuu wa Mungu katika maisha yake na kwa ajili ya kuzaa kwake. Kanisa pia huzaa matunda ikiwa linajua jinsi ya kuweka utendaji wa Roho Mtakatifu ndani yake kwanza. Tunaomba maombezi ya Maria ili nasi leo hii katika Mkutano wa  Sinodi tunao uzinduauwe mzuri mahali ambamo Neno la Mungu linaweza kuzaa matunda tele." Aidha Kardinali aliongeza: "Ningependa kuwaalika wote, katika mwezi huu wa Oktoba uliowekwa wakfu kwa Maria, kusali pamoja na Rozari Takatifu wakati wa Sinodi. Nyote mtapokea rozari, ili sala hii iweze kutusindikiza katika safari ya siku hizi. Rozari ni uvumi usiokoma wa Neno la Mungu, maombi ambayo hayachoshi kubisha mlangoni. Kwa njia ya Rozari sisi pia hatumgeukii Maria kwa sala tu, bali pamoja naye tunalilinda Neno la Mungu: “Maria aliyaweka hayo yote akiyatafakari moyoni mwake”(Lk 2:19).

Sinodi ya Maaskofu
Sinodi ya Maaskofu

"Tukipitia mafumbo ya Rozari Takatifu, tunayarudia maisha ya Yesu, umwilisho wake na Pasaka yake. Sala  ambaye ni yenye mwelekeo dhahiri wa Kikristo. Rozari inatualika kumweka Kristo katikati, ili kujifungua Yeye ulimwenguni, kwa kufuata mfano wa Maria. Kwa kusali Rozari tunajifunza, kama Maria, kuwa wanafunzi wa Bwana." Kwa kuhitimisha Kardinali alisema: “Tumuombe pamoja katika mwezi huu Bikira Maria, kielelezo cha Kanisa, ili Mkutano wa Sinodi ulianza  safari yake leo hiii uwe Pentekoste iliyofanywa upya, ili Injili ya Yesu iendelee kuyarutubisha maisha ya wanadamu wote na sisi. inaweza kuwa sinodi moja ya Kanisa na mmisionari.”

30 September 2024, 18:18