Tafuta

Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican imeanza na Mafungo. Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican imeanza na Mafungo.  (ANSA)

Mafungo ya Kiroho kwa washiriki wa Sinodi mjini Vatican:ukimya na lugha mpya

Katika tafakari ya Mafungo ya Kiroho kwa washiriki wa Sinodi,Mama Angelini,alisema:“Tamaduni zetu zipo kwa ajili kutuelekeza makao ya Mungu,”na kwa upande wa Padre Radcliffe,alisisitizia juu ya njia za kuzungumza na kukumbatia lugha mpya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sanaa ya mazungumzo ilianzishwa tena hapa, katika Kanisa la sinodi ni ya kuamua, mbadala kwa mazungumzo yote ambayo tunabeba mioyoni mwetu kwa uangalifu. Sanaa inayozaliwa tunaielewa kutoka katika Injili hii kutoka katika kiwango cha ukweli, ambacho Mungu anafikiria, na kutoka katika uchungu wa uziwi unaoonekana. Haya yalisemwa na Mama Maria Ignazia Angelini  katika tafakari yake ya masifu ya Asubuhi tarehe 30 Septemba 2024, wakati wa kuanza Mafungo ya Kiroho ikiwa ni maandalizi ya Sinodi mjini Vatican kwa washiriki kutoka duniani kote waliotumwa na Makanisa mahalia. “Tamaduni tunazotoka zinasita kujiweka wazi kwa kiu hii ya Mungu, ya kuiunganisha katika mifumo yao ya mfano,  na wanajitahidi japokuwa wanaathiriwa sana na mantiki ya biashara, nguvu, soko, usawa au kwa mantiki ya kukwepa ambao hufuata ndoto za uhuru kama kujiamulia." Mtawa huyo aliongeza kusema "lakini zaburi tuliyo nayo inaamsha tena kiu ya Mungu aliye hai. Yeye, Aliye Hai, ana kiu ya kiu hii, kama mtawa wa kale anavyothibitisha: 'Mungu ana kiu kwa ajili ya wale wanaomwonea kiu."

Mfano wa unyenyekevu

Mtakatifu Teresa wa Calcutta alituita tena kwa nguvu ya unyenyekevu. Kujianika kwa nuru yake kwa muda mrefu, kukaa katika Injili 'kama ilivyo katika mwili wa Kristo' huku ni kurudi nyuma, kuwa kweli. Jinsi ya kumkaribisha mtoto karibu na wewe, ndani yako mwenyewe." Mama Angellini akiendelea kutafakari juu ya kutafuta simulizi mpya zinazofungua upeo wa matumaini, alikumbuka maneno ya Papa Francisko, ambaye anatuonesha baadhi ya njia za kujaribu kufuatilia masimulizi yanayoshinda upweke na machafuko.

Padre Redcliffe: wengine wanakuja kwa woga

Changamoto kwetu ni kusaidiana kupumua kwa undani ndani ya Roho Mtakatifu anayehuisha!" Alisema Padre Timotheo Peter Joseph Radcliffe katika tafakari yake ya pili kwa ajili ya masifu ya asubuhi baada ya tafakari ya kwanza. “Kazi ya kwanza ya uongozi ni kuongoza kundi kutoka kwenye zizi ndogo hadi kwenye hewa safi ya Roho Mtakatifu. Uongozi hufungua milango iliyofungwa kwa vyumba vilivyojaa. Wanafunzi wamefungwa kwa hofu. Hebu basi na tufikirie juu ya hofu zinazoweza kutuzuia kuwa hai katika Mungu na kwa hiyo wahubiri wa Injili ya uzima kwa wingi. Wakizingatia woga wa kuumizwa. Baadhi yetu wanakuja kwenye Mkutano  kwa woga kwa sababu ya kufikiri kwamba hatutapata kutambuliwa na kukubalika.

Matumaini yetu ya thamani kwa Kanisa

Padre Redclieffe alieleza kuwa: "Matumaini yetu ya thamani kwa Kanisa yanaweza kudharauliwa. Tunaweza kuhisi hatuonekani. Je, tunathubutu kusema na kujihatarisha kukataliwa? Ikiwa haujazoea ulimwengu huu wa Vatican, wenye vyeo vyake vya ajabu na nguo za ajabu, inaweza kutisha. Tunathubutu kukimbia hatari ya kupata madhara, kwa sababu Bwana Mfufuka ameumizwa. Waoneshe mikono yako na ubavu wako.” Na baadaye alisema: “Upendo wetu mkali kwa Kanisa unaweza pia, kwa njia ya kushangaza, kutufanya tuwe na mawazo yaliyofungwa: woga kwamba litaharibiwa na mageuzi yenye uharibifu ambayo yanadhoofisha mapokeo tunayopenda. Au hofu kwamba Kanisa halitakuwa nyumba ya wazi tunayotamani. Inasikitisha sana kuona kwamba Kanisa mara nyingi linaumizwa na wale wanaolipenda, lakini kwa njia tofauti!”.   Hatimaye, kulikuwa na taalimungu nzuri, ambayo ni ilie kufungua milango ya vyumba vilivyofungwa: “Ni kama Tommasi, ambaye ana shauku na hana woga. Kubali njia mpya za kuzungumza, lugha mpya. Kanisa la sinodi kwenye.

30 September 2024, 17:36