Tafuta

Wanawake wa Kiafghanistan. Wanawake wa Kiafghanistan.  (AFP or licensors)

Afghanistan,tupaze sauti zetu kwa wale ambao sasa hawana sauti tena!

Wataliban wanakataza wanawake kuzungumza na kuimba hadharani.Huu ni uamuzi mwingine wa serikali ya Kabul ambao unakiuka haki za kimsingi za wanawake wa Afghanistan,katika miaka mitatu hasa baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka nchi hiyo ya kiasia.

Na Alessandro Gisotti

Hebu wazia  jambo la kuondoka nyumbani kesho asubuhi wakati ukielekea kazini, huku ukisikia sauti za kiume mitaani tu. Uzoefu huo ni wa kipekee zaidi kwa sababu unakutana na wanawake, kama iinavyotokea, lakini hakuna hata mmoja wao anayezungumza. Zaidi sana ananong'ona. Kisha wazia ukipita kwenye bustani ambapo unamkta mama anambembeleza mtoto wake kwa kumtikisa ili alale. Lakini anafanya hivyo kwa ukimya, bila kuimba wimbo kama ilivyokuwa zamani ya kila asubuhi. Na kama ambavyo tungetarajia kutokea kila mahali ulimwenguni. Hali hii inayostahili filamu ya dystopian au historia ya Orwellian ndiyo inayotokea huko Afghanistan ambapo, kupitia sheria, Wataliban wameamua, mara moja, kwamba sio tu nyuso na miili ya wanawake kufunikwa, hawana tena haki ya uraia katika maisha ya kijamii, bali hata sauti zao.

Habari hiyo ilichukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa, lakini kwa bahati mbaya haikuwa na habari iliyostahili na - hadi leo hii - haijazua maandamano ya kushtua na vuguvugu kubwa kama inavyotokea, sawa, kwa masuala mengine mengi na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hata hivyo sote tunapaswa kushtuka na kughadhibika mbele ya uamuzi wa namna hii, kwa sababu kukeketa sauti ya mwanamke ni kitendo cha ukatili usio wa kawaida ambao hauwezi kushindwa kuumiza jamii nzima ya binadamu kwa ujumla, zaidi ya uhusiano wowote wa kidini au kikabila au kiutamaduni. Ikiwa kweli sisi ni wanachama wa kila mmoja, kama Papa Francisko anavyoshuhudia na kutukumbusha kila siku, basi hatuwezi kubaki kutojali, kwa sababu vijakazi hao, wasichana hao wa Afghanistan ni wetu pia. Na lazima tupaze sauti zetu kwa wale ambao sasa hawana tena sauti hiyo.

Tarehe 31 Agosti 2024 ni miaka 3 sasa imepita tangu wanajeshi wa Marekani walipokamilisha haraka kujiondoa kutoka nchini Afghanistan na Wataliban wakapata tena madaraka. Tangu wakati huo, ndoto mbaya ilianza kwa wanawake wa nchi ya Asia ambayo inaonekana haina mwisho, lakini ambayo wakati huo huo ilikuwa ya kutabirika kabisa ambapo kwanza kabisa kutengwa kwa wasichana zaidi ya umri wa miaka 12 kutoka shuleni(ni nini kinachoweza kudharauliwa zaidi kuliko kuibia mustakabali wa kizazi?), kisha kupokonywa haki zao zote za kimsingi. Na sasa hata kufutwa kwa sauti hadharani. Katika mfumo wa vyombo vya habari wakati mwingine unaovurugwa na habari zinazochukua muda wake, sote tunapaswa kukumbuka kwamba kuna mamilioni ya wanawake ambao wamekatazwa kuzungumza, hata kupigwa marufuku kuimba. Wanawake ambao, mwaka 2024, sauti zao zimeondolewa na matumaini ya kuweza kuishi katika ulimwengu bora.

31 August 2024, 09:38