Tafuta

2023.05.24 Dk.Massimiliano Menichetti akiwa katika afla ya zawadi kwa Tangazo la I la Mashindano ya Kikanda 2022 Mwaka wa Perosia - Campobasso. 2023.05.24 Dk.Massimiliano Menichetti akiwa katika afla ya zawadi kwa Tangazo la I la Mashindano ya Kikanda 2022 Mwaka wa Perosia - Campobasso. 

Papa amemteua Dk.Menichetti kuwa Makamu mhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano

Alhamisi 18 Julai 2024,Papa Francisko amemteua Dk.Menichetti,kuwa Makamu Mhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na wakati huo huo akamteua Dk.Francesco Vale kuwa Makamu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Masuala ya Jumla ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano.Hadi uteuzi alikuwa Afisa wa Baraza hilo la Mawasiliano.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, alhamisi tarehe 18 Julai 2024 amefanya uteuzi kwa baadhi ya wahusika katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Awali ya yote amemteua Dk.MassimilianoMenichetti, kuwa Makamu Mhariri Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambapo hadi utuzi huo alikuwa ni Mratibu Mkuu wa Matangazo ya Radio Vatican-Vatican News.

Wasifu wake

Dk. Massimiliano Menichetti alizaliwa jijini Roma mnamo tarehe 27 Aprili 1971. Anayo digrii ya Sheria na Mwandishi wa habari kitaaluma. Kwa zaidi ya miaka 20 yupo Radio Vatican. Amefanya kazi kama Mhariri, Makamu Mratibu, Mkuu wa Kituo cha Wahariri wa Vyombo vya Habari na Mratibu wa Radio Vatican - Vatican News. Kwa njia hiyo ameshirikiana pia na vyombo mbalimbali vya habari vya Italia. Amefundisha uandishi wa habari katika vyuo vikuu mbalimbali.

Uteuzi wa Dk. Francesco Valle

Baba Mtakatifu tarehe 18 Julai 2024 pia amemteua Dk. Francesco Valle, kuwa Makamu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Masuala ya Jumla ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambapo hadi uteuzi huo alikuwa Afisa wa Baraza hilo la Mawasiliano.

Wasifu wake

Dk. Francesco Valle alizaliwa jijini Roma mnamo tarehe 27 Mei 1972. Alihitimu katika Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha La Sapienza Roma. Amefanya kazi kwa zaidi ya miaka ishirini kama mtangazaji mkuu runinga ya Italia, pamoja na Mkurugenzi wa Utayarishaji katika Vipindi vya Televishen (TV,) Mkuu wa kuripoti Kitaasisi katika Televisheni ya Sky Italia na Mkuu wa usimamizi wa Mapato na Usimamizi wa Haki za Televisheni ya LA7. Tangu 2023 amekuwa akiwajibika kwa shughuli za kibiashara zinazohusiana na Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Papa amewateua baadhi ya viongozi wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano

 

18 Julai 2024, 15:58