Papa apokea Barua na Hati za Utambulisho wa Balozi wa Timor Mashariki
Baba Mtakatifu Francisko amepokea hati na barua za utambulisho wa Balozi wa Timor ya Mashariki Bi Chloé Silvia TILMAN DINDO.Alizaliwa mnamo tarehe 19 Aprili 1989.
Vatican News
Ijumaa tarehe 19 Januari 2024, Baba Mtakatiu Francisko amepokea barua na hati za utambulisho wa Balozi wa Tomer ya Mashariki, Bi Chloé Silvia TILMAN DINDO.
Alizaliwa mnamo tarehe 19 Aprili 1989. Alipata digrii ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nova huko Lisbon (Ureno), mnamo 2013, na Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Neuchâtel (Uswiss), mnamo 2018.
Ametekeleza shughuli zinyine kama:
Mshauri wa Kisheria katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Timor Mashariki(2013 – 2014), Afisa wa Sera katika Kituo cha Ulaya cha G7+ (2018 – 2020), mshauri wa Kisheria na kidiplomasia. Katibu wa Jumuiya ya Nchi zinazozungumza Kireno- CPLP(2021 - 2022), Mkuu wa Wafanyakazi wa Katibu Mtendaji wa Nchi zinazozungumza KirenoCPLP (2022 - 2023).
19 January 2024, 17:33