Vatican,mkutano kuhusu changamoto za Kanisa katika shughuli za kitaaluma
Vatican News
Jedwali hili la kazi ni kwa lengo la kuendeleza pamoja mtindo mpya wa ushirikiano na harambee, wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo za Kanisa katika Nyanja ya shughuli zao za kitaaluma. Ni mpango uliozinduliwa hivi karibuni, ulioratibiwa kwa mamlaka ya Baba Mtakatifu na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Utamaduni na Elimu, ambalo linahusisha taasisi nyingine za Kipapa za kitaaluma, Mabaraza ya Kipapa na Ofisi za Curia romana.
Kwa undani zaidi, kwa mujibu wa ujumbe kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, walibanisha kuwa waliodhuria jedwali la kazi hiyo ni Gambera na wakuu wa taasisi sita zinazoegemea kiutawala Vatican kuanzia na(Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Taasisi ya Kipapa ya Akiolojia ya Kikristo, Taasisi ya Kipapa ya Muziki Mtakatifu),Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kiarabu na Kiislamu, Taasisi ya Kipapa ya Yohane Paulo II ya Ndoa na Sayansi ya Familia), pamoja na wawakilishi wa Sekretarieti ya Vatican, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji/Kitengeo cha Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya maalum, Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Sekretarieti ya Uchumi, ya Utawala wa Urithi wa Makao makuu ya Kitume, Avepro (Wakala wa Kiti kitakatifu kwa ajili ya Tathmini na Kukuza Ubora wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vya Kikanisa) na baadhi ya wataalam. Kwa njia hiyo tunasoma barua ya maelezo kuwa, "Kwa kutiwa moyo na uchanganuzi wa pamoja wa kitambulisho ambacho kina sifa za kitaasisi tofauti meza ya kufanya kazi ilikutana mnamo 12 Septemba 2023 na 8 Novemba 2023."