Papa ameteua maaskofu wa Kamina na Basankusu,Congo DRC
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Jumamosi tarehe 11 Novemba 2023 amemteua Padre Léonard Kakudji Muzinga, wa Lubumbashi, kuwa Askofu mpya wa Kamina Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cong DRC. Hadi uteuzi huo alikuwa ni Paroko wa Mtakatifu Paulo huko Lubumbashi.
Wasifu
Padre Léonard Kakudji Muzinga alizaliwa tarehe 13 Machi 1970 huko Kalemie. Baada ya kusoma falsafa na taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo ya Kambikila (Lubumbashi), alipewa daraja la Upadre tarehe 31 Julai 2005 kwa ajili ya Jimbo kuu la Lubumbashi.
Ameshikilia nyadhifa zifuatazo: Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Joseph na Mkurugenzi wa Mbinu ya Taasisi Mtakatifu Francis Xavier huko Likasi (2005-2012); Mkuu Idara ya Kichungaji ya vijana katika sekta ya Likasi (2007-2011); paroko wa Mtakatifu Paulo huko Lubumbashi (tangu 2012); Padre na Mwakilishi wa Masista wa Familia ya Bakhita (tangu 2013); Padre wa Maaskofu wa Kazi ya Jimbo Kuu la Lubumbashi (2019-2021). Tangu 2023 amekuwa mjumbe wa Baraza la Jimbo kwa Masuala ya Uchumi.
Askofu Mteule Jimbo katolili la Basankusu, DRC
Baba Mtakatifu Francisko vile vile amemteua Askofu wa Jimbo la Basankusu huko DRC, Padre Libère Pwongo Bope, wa Jimbo Kuu la Kinshasa, ambaye hadi uteuzi alikuwa ni Katibu- Kansela wa Jimbo Kuu la Kinshasa
Wasifu
Padre Libère Pwongo Bope alizaliwa tarehe 21 Mei 1964 huko Mweka. Baada ya kusoma falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu André Kaggwa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane XXIII huko Kinshasa, alipewa daraja la Upadre tarehe 4 Januari 1992 kwa ajili ya Jimbo kuu la Kinshasa.
Ameshika nyadhifa zifuatazo na masomo zaidi: Leseni ya Falsafa huko Kinshasa (1991-1993); Mkufunzi na Profesa katika Seminari Kuu ya Falsafa ya Mtakatifu André Kaggwa (1993-1996); Katibu wa Taaluma katika Seminari hiyo hiyo (1996-1999); katibu binafsi wa Askofu Mkuu wa Kinshasa (1993-1999); Katibu-Kansela wa Jimbo Kuu la Kinshasa (1999-2006); Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Paulo huko Evry, Ufaransa (2007-2012); Shahada ya Uzamivu katika Falsafa katika Taasisi Katoliki huko Paris (2007-2013); Mkuu wa Seminari Kuu ya Mtakatifu André Kaggwa ya Falsafa na Profesa katika Chuo Kikuu Katoliki cha Congo (2013-2020); paroko wa Mtakatifu Albert huko Kinshasa (2020-2021); Fidei donum, mmisionari katika Afrika ya Kati na paroko wa Jimbo kuu la Bangui (2021-2023). Tangu 2023 amekuwa Katibu - Kansela wa Jimbo Kuu la Kinshasa.