Papa alikutana na Rais wa Shirikisho la Uswiss
Vatican News.
Lazima haikuwa mguso wa kawaida wa rangi tu lakini hata fahari katika dhamana ya kipekee ambayo imedumu kwa zaidi ya karne tano ambayo iliibuka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss Alain Berset mbele ya Walinzi wa Uswiss aliokutana nao mapema asubuhi tarehe 9 Novemba 2023 , wakati msafara wa magari kuingia mjini Vatican ukipitia katika Arco delle Campane. Na huduma ya uaminifu na ya kitaaluma iliyotolewa kwa Papa na Walinzi wa Kipapa wa Uswiss ilikuwa moja ya mada ya Mkutano uliyofanyika kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Mkuu wa Nchi ya Uswiss, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican.
Afrika na matukio ya vita
Kwa takriban dakika 20 za mkutano, pamoja na kuridhishwa na uhusiano mzuri kati ya Vatican na Shirikisho la Uswiss, Baba Mtakatifu Francisko na Rais Berset walizingatia, juu ya shida kadhaa za kimataifa, na marejeo maalum ya hali katika baadhi ya nchi za Kiafrika, migogoro ya Ukraine, Israel na Palestina na matokeo yake kujitolea kwa pande nyingi na amani kati ya watu. Baada ya mkutano hu ona Papa, rais wa Uswiss alifanya mazungumzo na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa na mashirika ya kimataifa.
Kubadilishana zawadi
Mwishoni mwa mkutano huo Papa alitoa zawadi ya kazi ya shaba iliyoitwa "Upendo wa Kijamii", ikionesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na maandishi "Usaidizi wa Upendo", nakala ya ujumbe wa mwaka 2023 wa Amani, moja ya Hati juu ya Binadamu. Udugu na kitabu Statio Orbis cha Njia ya Msalaba cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na Lev. Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Uswiss alimzawadia nakala ya taarifa ya hali ya tabianchi Uswiss ya tarehe 29 Julai1921, siku ya joto isiyo ya kawaida huko Geneva na chenye kichwa,"Presence de la mort" kilichoandikwa na C.F. Ramuz.