Tafuta

2023.11.09  Matamasha kuelekea Jubilei 2025 2023.11.09 Matamasha kuelekea Jubilei 2025 

"Matamasha ya Jubilei,"mipango ya kwanza na wahusika wa Kiev

Kutakuwa na maonesho manane ya muziki yaliyoratibiwa kwa mojawapo ya mipango mipya ya kiutamaduni inayohusishwa na maandalizi ya Mwaka Mtakatifu.Mnamo Novemba 26,katika Ukumbi wa Conciliazione,Bendi ya Kiukraine itacheza kazi bora ya Antonín Dvořák,wimbo,"Kutoka Ulimwengu Mpya"

Vatican News

Sio kiroho tu, bali pia utamaduni. Dhana iliyosisitizwa mara kadhaa na Baraza la kipapa la Uinjilishaji katika kushughulikia mchakato wa safari ya kuelekea Mwaka Mtakatifu wa 2025, ambao maandalizi yake yameboreshwa kutokana na mtazamo huu na mfululizo wa matukio ya muziki. "Matamasha ya Jubilei Harmonies of Hope  yaani Maelewano ya matumani, yataanza Dominika tarehe 26 Novemba saa 12.00 jioni kwenye Ukumbi mkubwa wa njia ya Conciliazione Roma, pamoja na tukio la kwanza la mada ya muziki  la toleo la  tisa la Antonín Dvořák kutoka Ulimwengu Mpya ambalo litashirikisha Bandi ya "The Virtuosi of Kiev", inayoongozwa na mwalilimu Dmitry Yablonsky, maarufu duniani na  mtunzi.

Askofu Mkuu Fisichella: kutoka katika muziki tumaini la ulimwengu mpya

Kwa mujibu wa maelezo  kuhusu mwanamuziki huyo ni kwamba  "Dvořák, mwanamuziki wa Bohemian, anajitenga na kazi zake za awali za uimbaji na kupata safu ya uandishi isiyo makini lakini kali na  huru zaidi na yenye ubunifu". Kwahiyo, “Inaonekana ni jambo la kimantiki kwangu kufungua msimu wa matamasha haya ya Jubilei kwa sauti ya pamoja ya Dvořák, alisema Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa  kwa ajili ya Uinjilishaji, aliyeteuliwa na Papa kwa ajili ya maandalizi ya  Jubile ijayo, katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Kutoka katika upya. Ulimwengu unakumbushwa mada ya matumaini, ambayo tunaitwa na kauli mbiu ya Jubilei hii ya 2025. Bendi ya  Kiev, pamoja na kuwa wanamuziki wa maalum, wanatupatia fursa ya kutoa ishara ndogo ya kuunga mkono Ukraine, na aina ya ushiriki kupitia lugha ya ulimwengu wa muziki. Kwa matumaini ya ulimwengu mpya wa kweli alisisitiza tena Askofu Mkuu

Tamasha la bure

Tamasha ni bure na upatikanaji wa tikiti umehakikishwa wakati viti vinaendelea. Ili kushiriki, ni lazima uhifadhi nafasi mtandaoni kupitia sehemu ifaayo kwenye tovuti rasmi ya Jubilee 2025 kwenye kiungo: https://events.iubilaeum2025.va/registration. Msimbo wa kipekee wa QR, ambao utatolewa wakati wa kuhifadhi tiketi mtandaoni, lazima ipakuliwe na kuwasilishwa kwenye mlango wa ukumbi wa michezo, katika toleo la kidigitali au karatasi.

10 November 2023, 17:07