2023.11.19 CEPACS Jubilei, Nigeria: Dr. Paolo Ruffini akiwa na baadhi ya maaskofu wa Afrika wanaohusika na Mawasiliano . 2023.11.19 CEPACS Jubilei, Nigeria: Dr. Paolo Ruffini akiwa na baadhi ya maaskofu wa Afrika wanaohusika na Mawasiliano . 

Dk.Ruffini,Cepacs:Kuwasiliana kwa moyo na kushirikisha ujumbe kwa watu wa Mungu

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alizungumza jijini Lagos,Nigeria, tarehe 19 Novemba 2023 katika kumbukizi ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Kamati ya Mawasiliano ya Maaskofu Barani Afrika(Cepacs).Kuwasiliana kwa mtindo wa Kikristo ni kutoa ujumbe wa uzuri. kwa Watu wa Mungu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kuwasiliana na Ushirika ni maneno mawili ambayo yana mzizi mmoja. Ni ufahamu huu kwamba kwa wale wanaofanya kazi katika vyombo vya habari vya Kanisa, na hasa katika vyombo vya habari vya Vatican, ni dira inayoongoza kazi zao za kila siku. Kwa sababu mawasiliano sio habari tu bali ni mengi zaidi ya hayo. Ni kifungu cha  Hotu ya Dk. Paolo Ruffini Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, akiwa katikati ya  jiji la Lagos nchini Nigeria ambaye Dominika tarehe 19 Novemba 2023 alihutubia uwakilishi wa  Kamati ya Mawasiliano ya Maaskofu Barani Afrika(CEPACS) ili kusisitizia jambo lisiloweza kuepukika kwa wale wanaofanya kazi katika sekta hiyo.  Mawasiliano, kwa mujibu wake alisema ni zawadi ambayo Mungu ametupatia, wanadamu walioumbwa kwa mfano wake, kuwa na uhusiano kati yetu, kujenga jumuiya na kusuka ushirika kati yetu. Na kwa njia  hiyo ni maono ambayo mtindo hupitia.

DK RUFFINI AKIWA NA ASKOFU MKUU MSTAAFU WA LAGOS KARD.ANTHONY OKOGIE
DK RUFFINI AKIWA NA ASKOFU MKUU MSTAAFU WA LAGOS KARD.ANTHONY OKOGIE

Roho hiyo inatokana na Mtaguso II wa Vatican

Ni katika tukio la kuadhimisha Jubilei yamiaka 50 ya Cepacs,iliyooanzishwa mnamo mwaka 1973 kwa ajili ya kuwafunza wanataaluma wa vyombo vya habari barani Afrika, na kwa hiyo ni wakati wa uchunguzi wa jinsi gani ubora wa Habari Njema, Injili, unavyokuwa habari kulingana na mtiririko na mbinu za leo hii.  Dk. Ruffini, alizungumza  katika Kanisa Kuu la Msalaba Mtakatifu, huku akikumbuka kwamba miaka 10 hasa kabla ya Cepacs,  Mtaguso Mkuu II wa Vatican  ulikuwa umeona uchapishaji kama hati za kwanza za kikanisa za Mtagususo( Sacrosanctum Concilium)kuhusu liturujia  na Hati ya(Inter Mirifica)juu ya mawasiliano ya kijamii. Pamoja na Papa  Paulo VI, akisisitiza kwamba "mawasiliano ya kijamii yanathibitisha kwa uwazi kwamba Kanisa linafurahia uwezo wa kuunganisha maisha ya nje na maisha ya ndani, kutenda kwa kutafakari, utume na sala."

DK RUFFINI KATIKA AFLA YA MIAKA 50 YA CEPACS
DK RUFFINI KATIKA AFLA YA MIAKA 50 YA CEPACS

Vyombo vya habari na hekima ya moyo na kudumisha njia ya Pentekoste sio Babeli

Kattika haya maendeleo ya haraka yaliyorekodiwa na sekta  hiyo na kwa pamoja na lengo la jubilei ya Cepacs  kwa hiyo ndiyo ilikuwa ni motisha wa Dk.Ruffini  kwamba ni kutafuta, wote kwa pamoja, njia ya kuelekea kwenye mtindo zaidi wa mawasiliano ya Kikristo. Dk. Ruffini ali sema mawasiliano kiukweli ni zawadi ya Mungu ambayo hutuwezesha kuweka sawa kile tulicho nacho mioyoni mwetu. Pamoja na Ujumbe wake wa mwisho kwa Siku ya Mawasiliano Duniani, Baba Mtakatifu Francisko ametualika kuzingatia mioyo yetu: kusikiliza kwa sikio la moyo, kusema kwa moyo ambayo  ikuwa ni kauli mbiu za miaka miwili iliyopita. Pia, katika Siku ya 58 ya Mawasiliano duniani  kwa mwaka 2024, mada iliyochaguliwa na Papa Francisko inaunganishwa na moyo isemayo: "Akili bandia na hekima ya moyo: kwa mawasiliano kamili ya binadamu". 

Kushuhudia umoja

Mawasiliano kamili ya kibinadamu yanahitaji utunzaji! Methali moja ya Kiafrika, iliyonukuliwa katika hati ya Sinodi ya Kiafrika, inasema, “Mazao yanapaswa kupandwa, lakini magugu hukua yenyewe.” Njia ya sinodi ya kuwa Kanisa inahitaji kukuzwa. Mawasiliano yetu yanahitaji kukuzwa ili kuwa kweli katika huduma ya Kanisa, Familia ya Mungu. Kwa hiyo, Dk. Ruffini aliwahimiza kusaidiana na kupanua ufahamu kwa ajili ya utunzaji wa zawadi hii ambayo Mungu alitupatia ili kujenga mahusiano. Kwa pamoja, tunaweza kushuhudia kuwa kwetu Umoja, kuwa "viungo vya kila mmoja wetu".

NEMBO YA JUBILEI YA CEPACS
NEMBO YA JUBILEI YA CEPACS

Kwa pamoja, kupitia radio, kwa njia ya mtandao,na kupitia mitandao ya kijamii, tunaweza kujenga mfumo wenye dhamira ya kulisha neno la kweli, kwa kuzingatia uzoefu wa Pentekoste iliyounganishwa na roho ya kushiriki badala ya ile ya Babeli. Tuwashirikishe vijana wetu katika mfumo wetu wa mawasiliano. Dk. Ruffini aliomba kuwa ujumbe usafiri kutoka kwa mtu hadi mtu kama kitu kizuri kwa sababu ni kweli. Ni mzuri kwa sababu ni uzoefu wa kibinafsi. Unapendeza kwa sababu unasimulia uzuri wa Mungu na wa wanadamu.  Aliwaomba wavumbue au kubaini njia mpya za mawasiliano kati ya rika na rika ambazo msingi wake ni ushirika badala ya utengano: ushirika kati yetu, ushirika wa Watu wa Mungu, ushirika wa Familia ya Mungu Barani Afrika! Alihitimisha.

UJUMBE WA DK. RUFFINI KWA CEPACS
20 November 2023, 10:37