Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Vincent Frederick Mwakhwawa wa Jimbo kuu la Lilongwe, nchini Malawi kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Lilongwe. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Vincent Frederick Mwakhwawa wa Jimbo kuu la Lilongwe, nchini Malawi kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Lilongwe.  

Askofu Msaidizi Vincent Frederick Mwakhwawa Jimbo Kuu la Lilongwe, Malawi

Askofu mteule Vincent Frederick Mwakhwawa alikuwa ni Makamu wa Askofu Jimbo kuu la Lilongwe nchini Malawi na Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, PMS, na kwamba alizaliwa tarehe 20 Novemba 1975 huko Salima, Jimbo kuu la Lilongwe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 12 Julai 2003 akapewa daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo kuu la Lilongwe. Amewahi kuwa Paroko-usu, Paroko, Katibu muhtasi, Jaalimu na Mkurugenzi wa PMS.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Monsinyo Vincent Frederick Mwakhwawa wa Jimbo kuu la Lilongwe, nchini Malawi kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Lilongwe. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Vincent Frederick Mwakhwawa alikuwa ni Makamu wa Askofu Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi na Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, PMS, na kwamba alizaliwa tarehe 20 Novemba 1975 huko Salima, Jimbo kuu la Lilongwe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 12 Julai 2003 akapewa daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo kuu la Lilongwe.

Askofu Msaidizi Vincent Fredrick Mwakwawa Jimbo kuu Lilongwe
Askofu Msaidizi Vincent Fredrick Mwakwawa Jimbo kuu Lilongwe

Tangu wakati huo amewahi kuwa Paroko-usu na hatimaye Paroko. Aliteuliwa kuwa Katibu muhtasi wa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe kati ya mwaka 2006-2007 na Paroko wa Parokia ya St. Patrick kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2010. Baadaye alitumwa na Jimbo kuu la Lilongwe kujiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye kujipatia shahada ya Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki na Kati, CUEA, kilichoko Jijini Nairobi, Kenya kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2012. Baada ya masomo alitumwa kufundisha pamoja na kuwa ni mlezi wa Seminari kuu ya Kachebere, Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari, PMS, Mlezi wa Halmashauri ya Walei Taifa, Mshauri na tangu mwaka 2023 aliteuliwa kuwa Makamu Askofu Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi.

Jimbo kuu la Lilongwe

 

16 November 2023, 14:55