Warsha ya uchumi wa kidugu kwa maendeleo endelevu mjini Vatican
Vatican News
Uchanganuzi wa jukumu la mtaji wa kifedha wa kibinafsi, wa hisani na mchanganyiko wa umma na kibinafsi katika kuunda uchumi wa kidugu na endelevu. Haya ndiyo yaliyopendekezwa na mkutano wa pili uliokuwa na mada:“Programu ya Uchumi wa Kidugu” kuhusu ufadhili wa maendeleo endelevu, uliohamasishwa na Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii kwa siku mbili tarehe 26-27 Oktoba 2023 kwenye ukumbi wa Casina Pio IV, mjini Vatican. Wakati wa kikao cha kwanza kilichofanyika mnamo tarehe 26 na 27 Juni 2023 kwa kushirikishana na Shirika la Fedha la Kimataifa, Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa, mjadala ulijikita zaidi kuhusu nafasi ya taasisi za fedha za maendeleo katika kujenga uchumi wa kidugu na endelevu.
Kwa namna ya pekee, mnamo Juni Idermit Gill, mwanauchumi mkuu wa Benki ya Dunia, alijitolea kwa jukumu la baadaye la Benki ya Dunia katika kukuza Malengo ya Maendeleo Endelevu na malengo ya hali ya Tabianchi kimataifa. Pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa, walibanisha kuwa waliakisi kutafuta suluhu za kuongeza ufadhili wa muda mrefu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na kushughulikia mizigo ya sasa ya huduma ya deni kubwa.
Kukamilisha kazi
Madhumuni ya Warsha ya pili kuhusu uchumi wa kidugu uliofanyika mjini Vatican kwa siku mbili ulikuwa ni kukamilisha kazi iliyofanyika wakati wa kiangazi na kujadili kuongeza uwajibikaji wa fedha za sekta binafsi ili kuunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu na hatua za tabianchi katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Mbali na kundi kuu, wawakilishi wakuu kutoka benki za kimataifa, mifuko ya pensheni, wasimamizi wa mali, mashirika ya ukadiriaji (kama vile Moody's), viongozi wa ESG (mazingira, kijamii, utawala), wataalamu wa Umoja wa Mataifa na maafisa wanaohusika katika mchakato wa G20 walishiriki.
Kati ya G20 na COP28
Kazi hiyo ilifanyika wakati wa msukosuko mkubwa kufuatia tamko muhimu la viongozi wa G20 huko New Delhi ambalo linashughulikia mageuzi ya usanifu wa kifedha wa kimataifa, pamoja na jukumu la mtaji wa kibinafsi. Kufuatia mkutano wa kilele uliofanyika nchini India kati ya tarehe 9 na 10 Septemba 2023, Umoja wa Afrika ulikaribishwa kuwa mwanachama wa 21 wa kundi hilo. Zaidi ya hayo, macho yote sasa yanatazama Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ambako COP28 ya Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi itafanyika. Katika hali hii, mwanzoni mwa Desemba urais wa G20 utapita kutoka India hadi Brazil, ambayo imeahidi kuzingatia mageuzi ya kifedha duniani.
Warsha ya Uchumi wa Kidugu kwa hiyo imefanyika wakati muhimu wa tafakari na mazungumzo ya kimataifa, kwa lengo la kuchangia mjadala kwa kuzingatia mafundisho ya kijamii ya Kanisa na ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika waraka Laudato Si' (Kuhusu Utunzanji Bora wa mazingira nyumba yetu ya Pamoja na Fratelli Tutti yaani Ndugu wote kuishi kwa amani na usalama kijamii.