Vatican:Takwimu za Kanisa Katoliki 2023 katika fursa ya Siku ya Kimisionari duniani
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, katika muktadha wa kuelekea kilele cha Siku ya 97 Kimisionari duniani limechapisha takwimu za Kanisa Katoliki kwa mwaka 2023. Takwimu hizo zimechukuliwa kutoka katika takwimu za hivi karibuni katika “Kitabu cha Mwaka cha Takwimu za Kanisa” kilichochapishwa (na kusasishwa tarehe 31 Desemba 2021) na kinahusu washiriki wa Kanisa, miundo ya kichungaji, shughuli katika nyanja za afya, ustawi na elimu. Hatimaye, muhtasari wa mada za kikanisa zilizokabidhiwa kwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji zinaoripotiwa. Kwa hiyo kufikia tarehe 31 Desemba 2021, idadi ya watu duniani ilikuwa watu 7,785,769,000, ongezeko la vitengo 118,633,000 ikilinganishwa na mwaka 2021. Ongezeko hilo la kimataifa pia linajumuisha mabara yote mwaka huu, isipokuwa Ulaya.
Katika tarehe hiyo hiyo ya 31 Desemba 2021, idadi ya Wakatoliki ilikuwa sawa na watu 1,375,852,000 na ongezeko la jumla la Wakatoliki 16,240,000 ikilinganishwa na mwaka uliookuwa umepita. Ongezeko hilo linaathiri mabara yote, isipokuwa Ulaya (-244,000). Kama ilivyokuwa hapo awali, kuna mabadiliko mengi zaidi barani Afrika (+8,312,000) na Amerika (+6,629,000), ikifuatiwa na Asia (+1,488,000) na Visiwa vya Australia (+55,000). Asilimia ya kimataifa ya Wakatoliki ilipungua kidogo (-0.06) ikilinganishwa na mwaka uliopita, na ni sawa na 17.67%. Kuhusu mabara, tofauti ni ndogo. Jumla ya idadi ya Maaskofu duniani ilipungua kutoka vitengo 23, na kufikia 5,340. Idadi ya maaskofu wa majimbo (-1) na maaskofu watawa (-22) ilipungua. Maaskofu wa majimbo ni 4,155, huku Maaskofu Watawa ni 1,185.
Idadi ya mapadre ulimwenguni ilipungua, na kufikia 407,872 (-2,347). Ulaya kwa mara nyingine tena ilirekodi upungufu mkubwa (-3,632), kuongeza Amerika (-963). Ongezeko hilo limerekodiwa barani Afrika (+1,518), Asia (+719) na Visiwa vya Oceania na Australia (+11). Mapadre wa Majimbo duniani walipungua duniani kote kwa vitengo 911, na kufikia idadi ya 279,610. Mapadre watawa, walipungua jumla kwa vitengo 1,436 hadi kufikia128,262. Mashemasi wa kudumu duniani wanaendelea kuongezeka, mwaka huu kwa vitengo 541, na kufikia idadi ya 49,176. Ongezeko hilo lilitokea katika mabara yote: Afrika (+59), Amerika (+147), Asia (+58), Ulaya (+268) na Oceania (+9).
Mabruda walipungua kwa vitengo 795, na kufikia idadi ya 49,774. Upungufu huo ulirekodiwa Amerika (-311), Ulaya (-599) na Oceania (-115). Wanaongezeka katika Afrika (+205) na Asia (+25). Mwenendo huo wa kupungua kwa watawa duniani ambao umekuwa ukiendelea kwa muda umethibitishwa, wakati huu ukifikia idadi ya vitengo 10,588 ikilinganishwa na utafiti wa mwaka uliopita. Kuna jumla ya watawa wa kike 608,958. Ongezeko limeandikwa, kwa mara nyingine tena, katika Afrika (+2,275) na Asia (+366), na kupungua Ulaya (-7,804), Amerika (-5,185) na Oceania (-240).
Idadi ya waseminari katika Seminari Kuu za majimbo na za kitawa, ilipungua kwa ujumla katika vitengo 1,960 mwaka huu, na kufikia idadi ya 109,895. Ongezeko hilo limerekodiwa barani Afrika tu (+187), na kupungua Amerika (-744), Asia (-514), Ulaya (-888) na Oceania (-1). Kwa hiyo jumla ya waseminari Ndogo za majimbo na za kitawa waliongezeka kwa vitengo 316, na kufikia idadi ya 95,714. Walipungua katika bara la: Amerika (-372), Asia (-1,216), Ulaya (-144) na Oceania na visiwa vyake (-5), wakati kuna ongezeko kubwa pekee lilirekodiwa katika bara la Afrika (+2,053).
Katika nyanja ya elimu, Kanisa linasimamia shule za chekechea (Awali) 74,368 duniani kote zinazohudhuriwa na wanafunzi 7,565,095; shule za msingi 100,939 kwa wanafunzi 34,699,835; Shule za sekondari 49,868 kwa wanafunzi 19,485,023. Zaidi ya hayo, inafuatia wanafunzi 2,483,406 wa shule ya High School na wanafunzi 3,925,325 wa vyuo vikuu.
Taasisi za afya, upendo na misaada zinazosimamiwa na Kanisa Katoliki duniani ni pamoja na: hospitali 5,405, zahanati 14,205, hospitali za watu wenye ukoma 567, nyumba za wazee 15,276, wagonjwa wa kudumu na walemavu, vituo 9,703 vya watoto yatima, 10,567, vituo vya ushauri na ndoa 10. Vituo 3,287 vya elimu ya jamii au elimu mpya na taasisi za kijamii 35,529 za aina nyinginezo. Mamlaka za kikanisa zinazotegemea Baraza la Kipapa la Uinjilishaji (Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya hasa) ni 1,121 kwa ujumla, kulingana na mabadiliko ya hivi karibuni yaliyorekodiwa. Nyaraka nyingi za kikanisa zilizokabidhiwa kwa Baraza la Kipapa Afrika ni (523) na Asia (481),Amerika (71) na Oceania/ visiwa vyake (46) wanafuata.