Tarehe 25 Oktoba,“Barua kwa Watu wa Mungu”itachapishwa!
Vatican News
Usomaji wa rasimu ya Barua kwa Watu wa Mungu ulipokelewa kupigiwa makofi na kusanyiko la Jumatatu asubuhi tarehe 23 Oktoba 2023. Kwa mwaliko wa Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu Kardinali Mario Grech, “mapendekezo madogo ya mabadiliko na nyongeza kwenye maandishi yalipendekezwa na kukubaliwa, hasa kuhusiana na tafsiri katika lugha mbalimbali.” Barua hiyo itaidhinishwa na kuchapishwa Jumatano,tarehe 25 Oktoba 2023 kama alivyotangaza Dk Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari.
Misa na kazi ya Jumatatu Oktoba 23
Siku ya Jumatatu 23 Oktoba ilifunguliwa saa 2:45 asubuhi kwa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican iliyoongozwa na Kardinali Charles Maung Bo, Askofu Mkuu wa Yangon nchini Myanmar. Baada ya misa hiyo, washiriki waliingia katika Mkutano Mkuu wa 16, ulioratibiwa na mjumbe wa rais, Padre Giuseppe Bonfrate, mbele ya Papa Francisko na washiriki 350,waliokuwapo. Padre Timothy Radcliffe, Dominikani, mtawa wa Kibenediktini Sr Maria Ignazia Angelini, na Mtaalimungu wa Australia Padre Ormond Rush walitoa tafakari, kabla Barua ya Watu wa Mungu haijawasilishwa na kujadiliwa.
Kardinali Schönborn: imani, matumaini na mapendo katika ushirika
Kardinali Christoph Schönborn, Askofu Mkuu wa Vienna, na mjumbe wa Baraza la Kawaida la Sekretarieti ya Sinodi, pamoja na uzoefu wake alioupata wakati wa sinodi zilizopita, alishirikisha kumbukumbu tangu mwaka 1965, mwishoni mwa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican, alipokuwa na umri wa miaka 20 na alikuwa mwanafunzi wa Taalimungu. Kardinali alikuwa amesikiliza hotuba ya Karl Rahner na sentensi ya mwisho ya mzungumzaji ikabaki moyoni mwake kuwa: “Ikiwa Baraza hili halitasababisha ukuaji wa imani, matumaini na mapendo, kila kitu kitakuwa bure.” Hii ndiyo sababu, aliongeza Kardinali kuwa: “Ningesema jambo lile lile kuhusu Sinodi hii.” Akiwa mtaalimungu, Kardinali Christoph Schönborn pia alishiriki mwaka 1985 katika Sinodi maalum iliyoitishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II miaka ishirini baada ya kuhitimishwa kwa Mtaguso wa II wa Vatican. Kuhusu dhana ya msingi ya Ushirika, alisema alikuwa na maoni kwamba “kile tunachofanya sasa, baada ya kumbukumbu ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Sinodi”, kwa usahihi tunajiuliza “ jinsi ya kuishi ushirika katika 'Kanisa.
Ushirika wa imani, ushirika na Mungu mmoja wa Utatu, ushirika kati ya waaminifu na ushirika ulio wazi kwa watu wote." Je ni jinsi gani ya kuishi hivyo? Kwa kujibu Kardinali Schönborn amesema: “Sinodi ndiyo njia bora zaidi.” Ni suala la kufikiria upya maono ya Lumen gentium, ambapo ni swali la fumbo kuu la Kanisa. Kanisa ni fumbo, ni watu wa Mungu, na hapo ndipo tunaweza kushughulikia suala la katiba ya washiriki wake. Kadinali huyo pia aliikosoa Ulaya “ambayo alisema sio tena kituo kikuu cha Kanisa.” Amerika ya Kusini, Asia, Afrika na mikutano yao ya kibara inaongoza, wakati uaskofu wa Bara la Ulaya haujaweza kutumia uwezo ulioendelezwa, kwa mfano, na (Fabc) Asia (Secam) Afrika na (Celam) Amerika ya Kusini. Katika bara la kale yaani la Ulaya alisisitiza kuwa, “tumebaki nyuma kidogo katika sinodi yenye uzoefu. Kwa njia hiyo: “Msukumo unahitajika.” Alitumia mfano wa ukweli kwamba, Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya hayajawahi kuwa na msimamo mmoja kuhusu maafa ya wahamiaji. Askofu mkuu wa Austria anamalizia kwa kurejea Makanisa ya Mashariki ambayo daima yamepitia sinodi isiyoweza kutenganishwa na liturujia. Hivyo ametoa mwaliko wa kuenzi imani ambayo huadhimishwa kabla ya kujadiliwa.
Kadinali Aguiar Retes: mwendelezo wa sinodi
Kardinali Carlos Aguiar Retes, Askofu Mkuu wa Mexico, mmoja wa marais wa Baraza na mjumbe wa kuteuliwa na Papa, alikumbusha sinodi ya 2012 iliyopendekezwa na Papa Benedikto XVI juu ya uinjilishaji mpya, ambayo ilihitimishwa kwamba usambazaji wa imani ‘ulivunjika’ kwa sababu: “Familia hazikuweza tena kushughulikia vizazi vipya. Hii ndiyo sababu sinodi ya kwanza ya Papa Fransisko ilijikita juu ya familia, ambayo ni ya msingi katika suala hili. Na ni muhimu kufanya kazi nao ili kufikia vijana, ambapo sinodi kuhusu wao ilifuata mnamo 2018. Akizungumzia uzoefu wake mwenyewe na vizazi vipya katika Jimbo Kuu la Tlalnepantla, ambako alikuwa mchungaji kabla ya kuhamia mji mkuu wa Mexico, aliripoti kuwa na mikutano na vijana kutoka tamaduni mbalimbali za kijamii, kwa nia ya mazungumzo yenye lengo la kukuza urafiki nchini kote na mipaka ya kijamii. Mikutano hii ilimfanya afikiri kwamba “matamanio ya imani lazima yasambazwe na vijana wanaoishi imani.” Kardinali wa Mexico aliendelea: “Hii ndiyo sababu, Papa Francisko alimwita kushiriki katika sinodi ya Amazonia. Akitafakari juu ya umuhimu wa mabadiliko ya tabiachi na ulinzi wa kazi ya uumbaji, alitambua kwamba ni muhimu kuweza kutegemea usikivu wa kiikolojia wa wadogo zaidi: “Kwa hiyo lazima tuwasaidie kuelewa Neno la Mungu juu ya maswali haya.” Hatimaye, Kardinali alizungumza kuhusu mchakato wa sinodi katika Jimbo kuu lake la Mexico, Oktoba 2021. Uzoefu wa kutembelea hali halisi za mitaa, kwa njia inayojikita katika maelewano, mazungumzo na kusikilizana, matunda ambayo yaliakisiwa kwa pamoja ili kukidhi mahitaji ya jamii. Kwa sababu, njia ya Kanisa ni sinodi,”alihitimisha
Kardinali Aveline: kusikiliza, kimya, sala na uhuru
Kwa upande wa Kardinali Jean-Marc Aveline, Askofu Mkuu wa Marsiglia, anayehudhuria Sinodi kama mjumbe wa kuteuliwa na Papa, aliyechaguliwa kuwa katika Tume kwa ajili ya ripoti ya muhtasari, alianza kwa kueleza hisia zilizoambatana naye katika mang’amuzi yake ya kwanza ya Sinodi mjini Vatican kwake ikiwa mpya, udadisi wa kukutana na watu kutoka duniani kote, ambao kulikuwa na kubadilishana uzoefu; lakini pia wasiwasi wa habari juu ya vita iliyopokelewa tangu kuanza kwa kazi hiyo. Akikabiliana na matukio hayo yenye kustaajabisha, Kardinali Aveline alisisitiza, kuwa “Kanisa lazima lichukue jukumu la kueneza kwa nguvu hata zaidi ujumbe wa upendo wa Mungu ulimwenguni.” Askofu mkuu wa jiji la Phokaea alithibitisha kufika Roma akiwa na wasiwasi kidogo kutokana na ukweli kwamba huko Ufaransa, “si kila mtu ameingia katika mchakato wa sinodi na kwamba kuna nafasi ya maendeleo ili kuhusisha watu wengi zaidi katika safari hii ya kawaida.” Kardinali alikumbusha kwamba hii “inaibua matarajio mengi kuhusu maamuzi ya mwisho ambayo yataakisi wajibu wetu wa pamoja. Juma hili litakuwa Jula la maamuzi, ambayo tutapata uzoefu wa hatua muhimu, kujaribu kukubaliana juu ya masuala mbalimbali na kuondoa tofauti. Miezi ijayo itakuwa ni ile ambayo tutavuna matunda tuliyopanda.”
Sr. Rigon:Tufanye ulimwengu kuwa mahali pazuri zaidi
Sr Samuela Maria Rigon, mkuu wa Shirika la Masista wa Mama wa Huzuni, na profesa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, ambaye anashiriki katika sinodi kama mjumbe aliyeteuliwa na Papa, alisimulia mshangao wake wa kuitwa kwenye sinodi: “Katika sala nilikubali kama mwito kutoka kwa Mungu wa kuitwa kwenye Sinodi, kama mwanamke aliyebatizwa, Mkristo na aliyewekwa wakfu,” alisema. Na Sinodi inageuka kuwa uzoefu wa kutajirisha sana, ambao ninagusa ulimwengu wa Kanisa.” Tukio fulani nililiishi kama mwaliko wa unyenyekevu; na maoni yangu ni dirisha tu juu ya upeo wa mtazamo ambao unaweza kusaidia kujenga pambozi zuri. “Tangu jana (Dominika 22 Oktoba), nimebeba maneno matatu kutoka kwa Liturujia ya Ekaristi ambapo Mtume Paulo anatuzungumzia kuhusu imani yenye bidii, kazi ngumu katika mapendo, uthabiti katika tumaini katika Yesu Kristo.” Kama hili lingetoka nje ya Sinodi hii, tungekuwa tayari tumefanya mapinduzi chanya ya kweli,” alisisitiza mtawa huyo; kwa sababu, aliongeza, “tumepokea mbegu muhimu ambayo Mungu ataikuza ijapokuwa sisi au pamoja nasi.” Juu ya kanuni hiyo, Sr Samuela alirejea wazo la Mtakatifu Francis wa Assisi kwamba: “Leo ninaanza kuwa Mkristo tofauti tena.” Ikiwa kila mtu angeweza kuamka kila siku na wazo hilo, tungekuwa na mabadiliko.” Alisema.
Muhtasari wa hati utachapishwa Jumamosi jioni
Katika kujibu swali la mwandishi wa habari, Dk. Paolo Ruffini alionesha kuwa kura, mbinu ambazo bado hazijafafanuliwa, na usambazaji wa waraka wa muhtasari umepangwa Jumamosi 28 Oktoba jioni. Kuhusu swali la pili, iwapo katika Mkutano ujao, Sinodi ya sasa izingatiwe kwa mujibu wa maudhui na umbo, Kardinali Aguilar Retes alieleza kwamba “ikiwa yale yaliyojadiliwa na uzoefu yatatekelezwa, kutakuwa na njia ya kwenda.” Kila kitu kinategemea, juu ya kile kitakachopatikana wakati watu watakaporudi katika majimbo yao.” Swali lingine lilihusu njia ya kufanya kazi iliyopitishwa wakati wa Mkutano na uwezekano wa kuitumia katika viwango tofauti vya Kanisa, kupanua ushiriki kwa watu wa kawaida na wanawake. Kardinali Schönborn alikariri hotuba yake ya mwaka 2015 kuhusu mada ya sinodi, ambapo, kuanzia Baraza la Yerusalemu, alieleza kwamba, zaidi ya yote, mbinu ni kusikiliza, yaani kusikiliza yale ambayo Mungu anayaonyesha kupitia mang’amuzi ya safari. Hitimisho la Sinodi linatokana na usikilizaji huu na utambuzi wa kawaida.
Kardinali Schonborn aliongeza kusema kuwa tayari amezoea njia kama hiyo, inayotumika katika Jimbo Kuu la Vienna na, alikumbuka katika suala hili, kwamba kati ya 2015 na leo kumekuwa na mikutano 5 ya majimbo na washiriki 1,400, ambayo ni sehemu ya watu wote wa Mungu.” Hata kama hakukuwa na kura, kusikiliza na ushirika walikuwa na uzoefu. Jambo muhimu ni kwamba mwishowe, maamuzi lazima yafanywe.” Hakika, “Mtaguso wa Yerusalemu ulifanya uamuzi wa msingi kwa ajili ya historia ya Kanisa, na njia ya kuufikia ni ile tunayosoma katika Matendo ya Mitume. Njia hii ina sifa ya hatua tatu: kusikiliza, kimya, majadiliano. Aliunga Sr. Rigon, ambaye alisisitiza kwamba kupitia njia iliyotumika kwa Sinodi, kipengele muhimu kilibakia kusikiliza. “Kila mtu, lazima agundue upya hali hii, mahali pa kazi, katika familia, katika jumuiya za kitawa. Kila mtu lazima apate fursa ya kushiriki na kusikilizwa. Si kwa bahati kwamba amri ya kwanza ya Biblia ni “Sikilizeni Israeli.”
Asili ya Sinodi haijabadilika
Katika kujibu ukosoaji unaohoji uadilifu wa Sinodi ya Maaskofu kutokana na uwepo wa walei kati ya wajumbe wake, Kardinali Schönborn alisisitiza kwamba, kwa maoni yake, “hili halileti tatizo, kwa sababu Sinodi inabaki kuwa Askofu wa Sinodi, hata ikiwa inahusisha ushiriki wa kweli wa wasio maaskofu. Ni chombo kinachotumika kutekeleza wajibu wa pamoja. Asili yake haijabadilika, imepanuliwa tu na uzoefu ni mzuri kabisa. Kwa upande mwingine, Kadinali huyo alisema, siku zote kumekuwa na wataalam wa kawaida, na uingiliaji kati muhimu sana, lakini sasa kuna uhusiano wa karibu zaidi katika sinodi ya maaskofu na ushiriki uliopanuliwa.” Kuhusu suala la iwapo kupotea kwa sinodi kumeliingiza Kanisa katika mgawanyiko na ni kwa kiwango gani Makanisa yote yanaweza kualikwa kufuata njia ya pamoja, Kardinali huyo huyo Mdominikani alisisitiza kwamba, mgawanyiko wa Wakristo kwa hakika ni kikwazo cha ushuhuda; lakini, alisema, huku akirejea maneno ya mtawa wa Kiorthodox ya Kikoptiki kuwa: “Labda Mungu anaruhusu 'aibu' hii kwa sababu bado hatuna uwezo wa kutumia vizuri umoja kwa manufaa ya ubinadamu.”
Kardinali Aguiar Retes kisha alizungumza kuhusu uzoefu wa Baraza la Maaskofu wa Mexico, katika nchi yenye wakazi milioni 180, asilimia 80 kati yao wakiwa Wakatoliki, walioungana kuzunguka imani ya kidini ambayo imejikita katika Mama Yetu wa Guadalupe. Walakini, hali ni tofauti kati ya kaskazini, kusini na katikati mwa Mexico. Wakati wa ziara yake ya kitume mwaka 2016, Papa alitoa wito wa mchakato salama katika kukabiliana na mahitaji ya mazingira ya kijamii na kiutamaduni. Na katika hili, utofauti haupaswi kuwa kikwazo: kuna njia tofauti za uendeshaji, lakini zote zinaelekeza juhudi zao kwenye mema ya Kanisa. Kwa upande wake, Kardinali Aveline amesisitiza kuwa, wakati mkubwa wa umoja wa Sinodi ni mkesha wa sala ya kiekumeni uliokuwa na mada “Pamoja” uliofanyika tarehe 30 Septemba 2023 ambapo kila mtu alikuwepo karibu na Kristo msulubiwa, “kwa sababu hamu ya umoja inakua katika tafakari ya Kusulubiwa, udhaifu wa Kristo kuwa njia pekee ya uhakika ya umoja.
Ni Papa pekee anayeweza kufanya mabadiliko ya Katekisimu
Akijibu swali kuhusu ukweli kwamba baadhi ya watu wa Lgbtq+ wanaweza kuhisi kuumizwa na maneno ya Katekisimu ya Kanisa Katoliki inayorejea “machafuko ya kimaadili”, Kardinali Schönborn alikumbusha kwamba yeye mwenyewe alikuwa katibu wa wahariri wa Katekisimu. “Ni,kazi ya Kanisa, iliyotangazwa na Papa. Na tangu wakati huo, kumekuwa na mabadiliko tu, wakati Papa Francisko alipoingilia kati juu ya hukumu ya kifo. Ikiwa kuna mengine inategemea tu uamuzi wa papa. Kisha Kadinali akapendekeza kuwa sikuzote ni “kusoma maandiko kwa ukamilifu.” Haya ni maswali, ambayo yanaangukia chini ya taalimungu ya maadili, lakini kanuni ni kwamba “kuna utaratibu wa lengo na wanadamu. Daima wanastahili heshima, hata kama wanatenda dhambi, ambayo sisi sote tunafanya, hata mimi. Tuna haki ya kuheshimu. Tuna haki ya kukubaliwa, kama wao wanakubaliwa na Mungu.”Alisema Kardinali.
Hatimaye, kuhusu uhusiano kati ya habari za Majisterio yaani Mafundisho ya Kanisa, mchango wa wataalimungu na maana ya imani, tena Kardinali Schönborn aliyeeleza kwamba ni lazima tusome tena kile ambacho Mtakatifu Yohane XXIII alisema mwanzoni mwa Mtaguso wa II wa Vatican juu ya kutobadilika kwa mafundisho na jinsi yanavyowasilishwa. Kardinali aliongeza kuwa: “Kuna maendeleo makubwa katika kiwango cha ufahamu, lakini pia kuna kutobadilika kwa imani: hatuwezi kubadili fundisho la Utatu, Umwilisho au taasisi ya Ekaristi. Huu ndio msingi wa kanuni ya imani ambayo ni halali duniani kote, na hata kama tamaduni zinatofautiana, kiini cha imani hakiwezi kubadilishwa, hata kama imebadilika sana tangu wakati wa mitume.