Sr.Maria Antonia(Mama Antula)atatangazwa Mtakatifu
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Maria Antonia wa Matakatifu Yosefu, anayejulikana zaidi kwa jina la Mama Antula, kutoka Argentina,aliyetangazwa kuwa mwenyeheri mnamo tarehe 27 Agosti 2016, atatangazwa kuwa Mtakatifu. Wakati wa Mkutano wa alasiri tarehe 24 Oktoba 2023 kati ya Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu, Baba Mtakatifu Francisko aliidhinisha kwa amri kutangazwa kwake kutokana na muujiza unaohusishwa na maombezi ya mwanzilishi wa Nyumba za Mafungo ya Kiroho za tasaufi ya Mtakatifu Iginatius wa Loyola huko Buenos Aires nchini Argentina. Kwa hiyo Mama Antula atakuwa Mtakatifu kwa sababu muujiza wa ajabu wa kupona kwa mwanamume aliyekuwa anasumbuliwa na kiharusi katika maeneo mengi, na kuingia koma, mshtuko sugu, na kushindwa kufanya kazi viungo vingi katika hospitalini ya Mtakatifu Fe, nchini Argentina.
Mtu mwenye ugonjwa wa kiharusi alipona kwa maombezi ya mama Antula
Hapakuwapo na nafasi ya kubaki maisha ya kawaida kwa sababu ya uharibifu usioweza kurekebishwa wa ubongo. Kwa hiyo Mtu huyo aliitwa Claudio, na walikuwa wakisali ili kumwombea kupitia maombezi ya Mwenyeheri Maria Antonia wa Mtakatifu Giuseppe, familia nzima, marafiki na watu wengine ambapo kiajabu mtu huyo alipata kupona. Baada ya siku chache maboresho makubwa yalibainika. Kufuatia miezi michache ya kitaalumu ya viungo (physiotherapy), Claudio alirudi kuwa huru katika maisha ya kila siku na aliweza kufanya kazi ya kawaida ya mwongozo.
Huduma ya wagonjwa na misaada kwa maskini
Antonia de Paz y Figueroa, Mama Antula alizaliwa mnamo mwaka wa 1730 huko Silipica, Santiago del Estero, katika familia tajiri. Alipata elimu nzuri ya kidini, kiroho na kiutamaduni na alipokuwa bado mdogo alikutana na tasaufi ya Mtakatifu Ignatius. Mnamo 1745 alivaa nguo ya Kijesuit za “Mwenyeheri” mjesuit na alifunga nadhiri za faragha, yaani binafsi na akaanza kuishi maisha ya kijumuiya pamoja na wanawake wengine waliowekwa wakfu. Chini ya uongozi wa Padre Mjesuit Gaspar Juárez, alijitolea kwa ajili ya elimu ya watoto, huduma ya wagonjwa na misaada ya maskini, kisha, mnamo mwaka wa 1767, Charles III wa Hispania aliamua kuwafukuza Wajeuit kutoka Amerika kwenye maeneo ya Ufalme wa Hispania, Maria Antonia aliendeleza nia ya kuendeleza utume wa mazoezi ya kiroho na wazo la kufungua nyumba. Kwa idhini kamili ya muungamishi wake na Askofu wa Santiago ya Nchi za Nje alitekeleza mpango wake.
Zaidi ya watu 80 elfu walinufaika na mafundisho yake
Alisafiri sana kueneza hali ya kiroho ya Mtakatifu Ignatius na kufungua nyumba mpya za mafungo. Shauku yake ya kwenda mahali ambapo Mungu hakujulikana ilimpeleka hadi Uruguay, Cologne na Montevideo. Huko Buenos Aires alijenga Nyumba za Mafungo. Alikufa mnmo tarehe 7 Machi 1799 akiwa na umri wa miaka 69 tu. Inakadiriwa kwamba wakati wa kuwepo kwake duniani karibu watu 80,000 walinufaika kutokana na uzoefu wa mazoezi ya kiroho ya Mtakatifu Ignatius wa Loyola. Mabaki yake leo yamepumzika katika Kanisa la Mama Yetu wa Huruma huko Buenos Aires nchini Argentina. Mwaka 1905 Maaskofu walileta mchakato wa a kutangazwa mwenyeheri kwa Maria Antonia mjini Vatican. Alitangazwa kuwa Mwenyeheri tarehe 27 Agosti 2016 katika bustani ya Francisko ya Aguirre huko Santiago del Estero, kwa kuongozwa na Kardinali Angelo Amato kama mjumbe wa Baba Mtakatifu katika maadhimisho hayo.
Sala kwa Mwenyeheri Antula ili tangazwe kuwa Mtakatifu
Mungu na Baba yetu, ulimchagua Mtumishi wako Maria Antonia wa Mtakatifu Yosefu kuwa chombo cha Uinjilishaji kwa njia ya Mafungo ya Kiroho, ukimpatia karama za Imani tendaji, kuongoa mioyo na matumaini thabiti, ili asikatishwe tamaa katika shida na upendo mkubwa wa umama kwa wanaoteseka, hasa maskini zaidi. Kwetu sisi tunaoheshimu kumbukumbu yake iliyohifadhiwa na Mabinti zake wa kiroho, utujalie tuweze kumwiga na kwa maombezi yake neema hii tunayokuomba kwa ujasiri...( kwa bidii omba neema unayotaka...).
Na umwinue mapema karibuni kama Mtakatifu pamoja na Mtakatifu Ignatius wa Loyola, Baba yake na mwalimu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Inafuata sala ya (Baba Yetu, Salamu, Atukuzwe Baba...