Sinodi,wajumbe wa Tume za Muhtasari wa Ripoti na Habari waliochaguliwa
Vatican News
Katika kikao cha alasiri cha Baraza Kuu la Sinodi Jumatatu tarehe 9 Oktoba 2023,upigaji kura ulifanyika kwa ajili ya uchaguzi wa wajumbe wa Tume ya Ripoti ya Sinodi na wale wa Tume ya Habari. Tume ya Ripoti ya Muhtasari ina kazi si ya kuandika tu, bali ya kusimamia mara kwa mara, kurekebisha na kuidhinisha kazi ya maandalizi ya rasimu ya Ripoti ya Muhtasari kwa kuzingatia uwasilishaji wake kwenye Mkutano wa Sinodi. Kwa upande mwingine, Tume ya Habari ina jukumu la kuhakikisha mawasiliano yanafanyika kwa maendeleo ya Mkutano wa Sinodi kwa mujibu wa Ibara ya 24 § 1 ya Kanuni katika makubaliano na Baraz ala Kipapa la Mawasiliano na Sekretarieti kuu ya Sinodi, ambayo husaidiana na wafanyakazi wao.
Uchaguzi ulifanyika kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizooneshwa katika Kanuni, hasa kifungu cha ibara ya 11, § 2-4; na 14 na 15.
Wajumbe wa Tume ya Ripoti ya Muunganisho
Kwa hiyo, kwa mujibu wa Kanuni, Tume ya Ripoti ya Muhtasari inaundwa na rais, Kadinali Jean-Claude Hollerich, Msemaji mkuu wa Sinodi.
Wajumbe ni:
Kardinali Mario Grech, Katibu mkuu wa Sinodi;
Padre Riccardo Battocchio, katibu maalum.
Wajumbe waliochaguliwa na Mkutano ni:
Kadinali Fridolin Ambongo Besungu (Afrika - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo); Kardinali Jean-Marc Aveline (Ulaya - Ufaransa); Kardinali Gérald Cyprien Lacroix (Amerika Kaskazini - Canada); Askofu José Luis José Luis Azuaje Ayala (Amerika ya Kusini - Venezuela); Askofu Anthony Mackinlay (Oceania - Australia); Askofu Mounir Khairallah (Makanisa Katoliki ya Mashariki - Lebanon); Padre Clarence Sandanaraj Davedassan (Asia - Malaysia).
Wajumbe wa uteuzi wa Kipapa ni:
Kardinali George Marengo, I.M.C. Sr. Patricia MURRAY, I.B.V.M.,
Padre Giuseppe Bonfrate
Wajumbe wa Tume ya Habari
Kwa mujibu wa Kanuni, Tume ya Habari inaundwa na Rais Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano aliyeteuliwa na mamlaka ya kipapa na katibu Sheila Leocádia Pires, aliyeteuliwa na mamlaka ya kipapa.
Wajumbe wa zamani (rej. ibara ya 11 § 2) ni:
Kardinali Jean-Claude Hollerich S.J., Msemaji Mkuu; Kardinali Mario Grech, katibu mkuu wa Sekretarieti kuu ya Sinodi; Monsinyo Luis Marín de San Martín, O.S.A., Naibu Katibu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi; Sr. Nathalie Becquart, X.M.C.J., Naibu Katibu wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi; Padre Giacomo Costa S.J., katibu maalum; Padre Riccardo BATTOCCHIO, katibu maalum; Matteo Bruni, Msemaji Mkuu wa Vyombo vya Habari Vatican; Thierry Bonaventura, meneja mawasiliano wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi.
Wajumbe waliochaguliwa na Mkutano Mkuu ni:
Kardinali Víctor Manuel Fernandez (Amerika ya Kusini - Argentina/Vatican); Kadinali Joseph William Tobin, C.SS.R. (Amerika ya Kaskazini-Marekani); Monsinyo Andrew Nkea Fuanya (Afrika -Cameroon); Askofu Pablo Virgilio S. David (Asia - Ufilipino); Askofu Anthony Randazzo (Oceania - Australia); Padre Antonio SPADARO, S.I. (Ulaya - Italia); Padre Khalil ALWAN, M.L. (Makanisa Katoliki ya Mashariki - Lebanon).