Sinodi,sio fedha bali wingi wa karama ni utajiri wa Kanisa!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ushirika ni neno la kwanza na la mwisho la mchakato wa sinodi, asili na maana ya kutembea pamoja. Anna Rowlands, profesa wa Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Durham huko Uingereza, alisema hayo asubuhi tarehe 9 Oktoba 2023, wakati wa kukutana kwa mara nne tangu kuanza kwa Sinodi hiyo. Profesa aliwaambia washiriki wa Sinodi kuhusu mawazo ya kitaalimungu ya sinodi katika tafakari ya mada ya "Ushirika unaong'aa au kumeremeta. Tunawezaje kuwa ishara na chombo kikamilifu zaidi cha muungano na Mungu na umoja wa wanadamu?" katikati ya sehehu ya Pili ya kifungu cha Instrumentum laboris, au kitendea kazi kilicho na mada kuu za mkusanyiko huo. Ushirika hai unahitaji ujasiri yaani, "ujasiri wa kutazama ukweli usoni kwa jinsi ulivyo". Utajiri wa Kanisa si fedha, bali ni wingi wa karama, yaani karama na neema ambazo Mungu anazimimina na kuzisambaza katika jumuiya ya waamini na ambazo tumeitwa kuzitambua, kama wabatizwa wote.” Kwa mujibu wa maoni ya Anna Rowlands, ushirika kwa hiyo ni "kitendo chetu na hadhi yetu, ni njia ambayo tunaelewa mpango mkuu wa Mungu kwa wanadamu wote wa kufanya upya uso wa dunia."
Kila mtu wa Kanisa atafute Ushirika wa uzuri usio wa kidunia
Uzuri wa utofauti katika umoja unaelezea ushirika, kulingana na mwalimu: "Katika ulimwengu wa kisasa ambao unaelekea kwenye mfananisho na kugawanyika wakati huo huo, ushirika ni lugha ya uzuri, maelewano ya umoja na wingi". Unyenyekevu na huduma ni sifa ya ushirika kwa maoni ya Rowland, katika mantiki iliyo kinyume na ile ya ulimwengu ambayo nguvu ya ushindani na milki inashinda mahusiano. Kwa hiyo "Mungu hutuvuta katika ushirika wa unyenyekevu na huduma". Kwa hakika, Utatu huangaza ushirika usio na ushindani na kila mtu katika Kanisa anaitwa kutafuta uzuri huo usio wa ulimwengu.
Vipmo vya Ushirika vinakutana
Kwa hiyo washiriki wa Sinodi katika mkao huo wanaalikwa kutafakari pamoja na wanyonge, wanaoteseka na udhaifu wa Kanisa. Kwa maneno mengine jinsi ya kujiweka karibu zaidi na maskini zaidi, wenye uwezo zaidi wa kusindikiza na wabatizwa wote katika kanisa wa hali mbalimbali za kibinadamu." Tamasha la hajabu la hali ya binadamu ni mahali ambapo Kanisa linazaliwa na kuishi, alieleza Profesa wa Chuo Kikuu cha Durham. Kama katika karamu, Mungu anatualika "kuonja na kuona, kuchukua na kula", anavutia hisia zetu. Ni kweli katika Ekaristi kwamba vipimo mbalimbali vya ushirika vinakutana. “Ufafanuzi wa Biblia wa siku kuu hiyo ni picha inayopotosha ile inayoonwa kuwa utaratibu wa asili wa mambo. Katika karamu, wale ambao hawana nguvu, waliodharauliwa na wanaoteseka watakuwa wa kwanza" kutokana na ukaribu wa Mungu, alisisitiza.
Daima kuna ukweli zaidi wa kujua
Kuhusiana na hilo Profesa Rowlands alitoa mifano miwili ya maisha halisi. Kwanza alizungumza juu ya mtu aliyenusurika kuteswa na Padre ambaye katika mkesha wa Sinodi alimwandikia kuwa "asiogope kusisitiza juu ya hitaji la uponyaji" kwa sababu "ni Ekaristi inayookoa." Pili, alishirikisha uzoefu wake katika kituo cha mapokezi kilichounganishwa na Kanisa Katoliki huko London ambako, tofauti na vituo vingine, wakimbizi walimweleza siri kwamba walijisikia kukaribishwa kwa sababu waliitwa kwa majina. Mwaliko wake kwa hiyi siyo kumtenga mtu yeyote. Kwa sababu, "Kukaribisha ukweli kunamaanisha kuwa kuna ukweli zaidi wa kujua," Alibainisha profesa.
Shuhuda, Sinodi isiwe ya muda bali mazoezi ya Kanisa
Hotuba ya Profesa Anna Rowlands ilifuatiwa, baada ya kipindi cha ukimya na shuhuda nne. Katika ishara ya matumaini kulikuwa na uingiliaji kati wa Sōnia Gomes de Oliveira wa Baraza la Kitaifa la Walei nchini Brazil ambaye alishirikisha wasikilizaji uzoefu wake kama mfanyakazi wa kijamii kati ya walio wadogo na furaha ya kuishi mchakato wa kisinodi katika Kanisa la nchi yake. Kwa upande wake alisema "Walei wengi wamegundua kwamba wanawajibika pamoja kwa ajili ya utume wa Kanisa. Sinodi, kuanzia sasa na kuendelea haipaswi kuwa ya muda tu, lakini iwe mazoezi ya Kanisa, lazima tuwe uwepo wa Yesu, uwazi kwa kusikiliza na kukaribisha katika maeneo yenye maumivu na mateso, hata katika wale tusioweza kuwafikia miongoni mwa watu walioacha Kanisa na kuwa na mioyo iliyojeruhiwa na kwa hiyo miongoni mwa wanawake wahanga wa dhuluma na chuki na pia miongoni mwa maskini na watu wa kiasili.“
Ishara ya matumaini kati ya walio wa mwisho
Bi Gomes de Oliveira baadaye alisimulia wakati alipomwendea kahaba ili kumshirikisha katika mchakato wa sinodi. Mwanamke huyo, akiwa ameshinda hali ya kutokuwa na imani naye hapo awali, alijibu: “Sasa ninaelewa, Kanisa na Papa Francisko wanataka kujua jinsi nilivyo na ninafikiri nini kuhusu uwepo wa Kanisa. Nitazungumza, labda kitu kitabadilika." Ndivyo ilivyotokea kwa mfungwa ambaye mwisho wa mkutano aliomba rozari kutoka kwa Maria, "Mama ambaye hawaachi." Na mtu huyo alisema "Labda sitatoka gerezani lakini wewe huko nje unaweza kusaidia familia yangu."
Kuingilia kati kwa mjumbe ndugu
Mara baada ya hapo, mmoja wa wajumbe ndugu, Job Getcha, kutoka mji mkuu wa Pisidia, wa Upatriaki wa Kiekumeni, na rais mwenza wa Tume ya Kimataifa ya Mazungumzo ya kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox ambaye alionesha tofauti katika tafsiri ya Kanisa. Alizungumzia juu ya dhana ya Kisinodi na Kiorthodox. Sinodi ya Kanisa na Kiorthodox “ni mkutano wa kimakusudi wa maaskofu, si mkutano wa mashauriano wa makasisi wa kawaida” ambamo “mapatano yaonesha fumbo la Utatu la uhai wa kimungu.” Kisha Mkuu huyo alitaja hali fulani za kihistoria ambazo Kanisa la Kiorthodox lilihusisha makasisi na waamini katika mchakato wa sinodi.
Sauti kutoka bara la Asia
Katika ishara ya mazungumzo ya kidini, ushuhuda wa padre Clarence Davedassan wa Malaysia barani Asia, bara lenye watu bilioni 4 ambapo asilimia 3.31% ndiyo Wakatoliki. "Msisitizo wa Waasia juu ya kuwa na uhusiano na Mungu, binafsi na wanadamu wengine na ulimwengu ni tabia ya Kanisa la Kisinodi na inaongoza kwenye umoja wa familia ya wanadamu na umoja wa watu wa Asia." Akiendelea alisema "Kanisa sio watu la wachache wasio na maana, lakini katika ni lenye sehemu nyingi ambamo ni katika huduma ya maendeleo fungamani ya binadamu na manufaa ya wote na zaidi linataka kueneza ujumbe wake ambao ni wa kiinjili licha ya changamoto." Padre huyo alisisitiza na kuonya dhidi ya hatari ya kujirejea, kwani hii "ni tabia ya Kanisa barani Asia linalokabiliana na changamoto za ujenzi wa madaraja na hali ya kuongezeka ya kutovumiliana kwa dini na kijamii". Pia kutoka Asia, hotuba ya Siu Wai Vanessa Cheng ilisikika katika chumba hicho cha Mkutano. Kwa upande wake alisema "Kusikiliza kunamaanisha heshima", alisisitiza, huku akikumbuka hitaji la kuzingatia wale wanaokaa kimya kwa kuogopa kutokubaliwa au kuchukuliwa kuwa hawaheshimu mamlaka. "Sinodi inaleta matumaini kwa watu," aliendelea, akitoa mfano wa Kanisa huko Hong Kong ambalo lilisaidiwa na mchakato wa sinodi kuanza tena baada ya miaka miwili ya machafuko ya kijamii.