Papa amemteua Sr.Silvana Piro, F.M.G.B,kuwa Katibu msaidizi utawala na urithi wa Kitume
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi 14 Oktoba 2023 amemteua Katibu msaizidi wa Sughuli za Utawala wa Urithi, Makao Makuu ya Kitume Sr. Silvana Piro, F.M.G.B., ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mwasibu Mkuu wa Taasisi yake ya Shirika la Masisita Wamisionari Wafransiskani wa Gesu’ Bambino.
Wasifu wake
Sr. Silvana Piro alizaliwa tarehe 6 Novemba 1972 huko Torre del Greco, Wilaya ya Napoli(Italia). Baada ya shahada ya Uchumi wa Viwanda katika Chuo Kikuu cha Pisa na alipata shahada ya uzamili ya Uzamili katika Usimamizi wa Ubunifu huko Pisa. Mnamo 2008 aliendelea na Shahada ya Kwanza ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Kisalesian jijini Roma. Na mnamo tarehe 7 Desemba 2009 alifunga nadhiri za daima katika Shirika la Wamisionari Wafransiskani wa Gesù Bambino. Na tangia 2008 hadi 2012 alikuwa mhudumu wa Uchungaji wa Vijana katika Jimbo Kuu la Perugia-Mji wa Pieve. Wakati huo huo kuanzisha 2012 hadi uteuzi wake wamekuwa Mwasibu Mkuu katika Shirika lake.