Papa amemteua Padre Simeon Okezuo Nwobi, C.M.kuwa Askofu wa Ahira
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mpya wa Jimbo katoliki la Ahiara nchini Nigeria ambalo hadi sasa halikuwa na Askofu, kwa huyo Mhs. Padre Simeon Okezuo Nwobi, C.M.F., kwa kumkabidhi makao yake huko Rusgunie.
Wasifu wake
Padre Simeon Okezuo Nwobi, C.M.F., alizaliwa tarehe 25 Machi 1960 huko Eziama Oparanadim Ekwereazu, katika Jimbo la Ahiara. Baada ya kujiunga na Shirika la Wamisionari wa Moyo Safi wa Maria (Waklareti), aliendelea na mafunzo ya Falsafa katika Taasisi ya Falsafa ya Claretian huko Maryland, Nedeke, na baadaye, ya Taalimungu katika Seminari ya Kumbukumbu ya Bigard huko Enugu. Alifunga nadhiri zake za daima mnamo tarehe 11 Septemba 1988 na akapewa daraja la Upadre mnamo tarehe 21 Julai 1990 kwa ajili ya Shirika lake. Alipata Diploma ya Uzamili katika Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jimbo la Enugu huko Enugu, Leseni ya Misiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma na Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu Huria cha Kitaifa nchini Nigeria.
Ameshika nyadhifa zifuatazo:
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Antoni huko Igbo-Ora (1990-1992); kufundisha katika Chuo cha Waclaretian cha Taalimungu huko Enugu (1992-1997); Mkurugenzi wa Idara ya Kiroho katika Taasisi ya Claretian ya Falsafa Maryland, Nedeke (1999-2000); Profesa katika Seminari ya Kumbu kumbu ya Bigard huko Enugu (2000-2009); Mkuu wa Utume katika Shirika la WaClaretian Kanda ya Owerri (2005-2010); Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Paulo huko Nekede (2006-2010); Mkuu wa Kanda ya Mashairiki ya Nigeria ya Wamisionari wa Moyo Safi wa Maria (2010-2022).