Katika Sinodi,Sala kwa ajili ya amani:wanadamu waunde familia moja isiyo na vita!
Vatican News.
Sala kwa ajili ya amani duniani, hasa kwa maeneo ya dunia ambayo yamekumbwa na migogoro ya sasa, ndiyo yamesikika asubuhi tarehe 12 Oktoba 2023 kutoka katika Ukumbi wa Paulo VI kabla ya kuanza kazi ya Sinodi. Aliyeongoza sala ya asubuhi hiyo alikuwa Kadinali Louis Raphaël Sako, Patriarki wa Baghdad ya Wakaldayo, ambaye aliwaalika wote waliohudhuria "kuombea amani duniani, hasa katika Nchi Takatifu, lakini pia katika Ukraine. Vurugu nchini Iraqi, Iran na Lebanon. "Watu wanangoja kwa matumaini makubwa kuishi kwa heshima na udugu na sio kila wakati kwa hofu na wasiwasi. Mshikamano pia unamaanisha mshikamano na wale wote wanaoogopa na wanaoteseka," Kardinali Sako alibainisha.
Maombi ya Margaret Karram
Kwa upande wa Margaret Karram, Mpalestina na rais wa Harakati ya Wafocolari, alisali sala nyingine. "Bwana, tunaomba kwa ajili ya Ardhi Takatifu, kwa ajili ya wakazi wa Israeli na Palestina ambao wako chini ya mtego wa ghasia zisizo na kifani, kwa ajili ya waathirika, hasa watoto, kwa waliojeruhiwa, kwa wale wanaoshikiliwa mateka, kwa ajili ya waliopotea na familia zao." Karram alisema, "katika saa hizi za uchungu na kusimamishwa", mwaliko ni kujiunga na sauti yako na ile ya Papa na wale ambao ulimwenguni kote wanasihi amani".
Karram pia alikumbuka nchi nyingine zote za Mashariki ya Kati ambazo "zinaishi kwa hofu na uharibifu". Kwa hiyo alisema Bwana, utusaidie kujitolea kujenga ulimwengu wa kidugu ili watu hawa na wale walio katika hali sawa za migogoro, ukosefu wa utulivu na vurugu wapate njia ya kuheshimu haki za binadamu ambapo haki, mazungumzo na upatanisho ni nyenzo muhimu ili kujenga amani.”
Maombi ya mwisho
Hatimaye, Baraka na sala ya mwisho ya Patriaki Sako kwa Mungu ni kwa: "Ubinadamu wote ... ili uunde familia moja, bila vurugu, bila vita vya kipuuzi na kwa roho ya kidugu, ya kuishi kwa umoja na amani".