Tafuta

Mhutasari wa Sinodi inayoendelea  na mada nyingi zimzeungumziwa. Mhutasari wa Sinodi inayoendelea na mada nyingi zimzeungumziwa. 

Muhtasari wa Sinodi:Sinodi ni jinsi Kanisa linaweza kutembea ulimwenguni

Muhtasari wa Sinodi Jumanne umeakisi masuala kadhaa ya wajumbe wa Sinodi ambayo ni pamoja na huduma ya maaskofu,wanawake,marekebisho ya Sheria ya Kanisa inayowezekana na michango ya waamini.Mshiriki wa kike alisema,suala la ukuhani wa kike ni kwa sasa haliakisi mahitaji ya wanawake leo hii.

Vatican News.

Muhtasari wa Sinodi Jumanne unameakisi masuala yaliyojadiliwa na wajumbe wa Sinodi, ikiwa ni pamoja na huduma ya maaskofu, nafasi ya wanawake, marekebisho yanayowezekana ya Sheria ya Kanisa, na michango ya waamini, huku mshiriki mwanamke akisema suala la ukuhani wa kike ni “suala lisilo na maana, kwa sababu haliakisi mahitaji ya wanawake leo hii.” Kama kawaida ufunguzi ulianza  na kuombea amani ya Mashariki ya Kati, kwa kuitikia ombi la Patriaki Pierbattista Pizzaballa. Kwa njia hiyo  Dk. Paolo Ruffini, Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi, alitoa taarifa kuhusu kazi za makadinali, maaskofu, mapadre, watawa wa kike na na  kiume, na waamini walei, waliokusanyika tangu tarehe 4 Oktoba katika meza 35 za miduara katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican , katika mkutano wa kila siku asubuhi na jioni.  

Akiwakilisha katika Ofisi ya Waandishi wa Habari wa  Vatican, alisema katika Mkutano Mkuu wa Sinodi Jumanne  17 Oktoba 2023 uliendelea na mijadala yake ya mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nafasi ya wanawake, huduma ya maaskofu, mchango wa kanisa,  walei, na mageuzi yanayowezekana ya Sheria ya Kanoni.   Pembeni mwake kwenye meza walikuwapo wageni wanne: Askofu Mkuu wa Rabat, Kardinali Cristobal Lopéz Romero; Askofu Anthony Randazzo, Askofu wa Broken Bay, Australia, na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Australia; na Profesa Renée Köhler-Ryan na Mjesuit wa Nigeria Agbonkhianmeghe Emmanuel Orobator, miongoni mwa wataalimungu wanaojulikana sana katika ngazi ya kimataifa. Wote wanne wanahudhuria Sinodi yao ya kwanza na walisema walikuwa na furaha na wametajirishwa na uzoefu huo wa kusikiliza na kujifunza.

Marekebisho ya Sheria ya Kanoni ya Sheria

Mwanzoni mwa mkutano huo na waandishi wa habari Dk. Ruffini alizungumza kuhusu mchakato wa safari ya washiriki wa Mkutano Mkuu, wa Sinodi ambapo Jumanne walipokea nakala ya Waraka wa Kitume wa Papa  Francisko wa "C'est la confiance" Kuhusu Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu na kwa hiyo Mwenyekiti wa Baraza la  Kipapa la Mawasiliano alisema Siku ya Jumatatu na Jumanne, washiriki walijadili mada zilizotabiriwa na Kipengele cha B2 ya "Instrumentum laboris” Kuhusu “kuwajibika kwa ushirikiano katika Utume. “Wajibu wa pamoja” ni neno linalopendekezwa kuanzishwa ili kuchukua nafasi ya “ushirikiano” katika Sheria ya Kanoni, ambayo “marekebisho” yake yameombwa. Marekebisho sio mapinduzi, lakini mageuzi. "Sheria yenyewe bila shaka inaweza kubadilika wakati mahitaji ya Kanisa ambayo yametayarishwa kwa mabadiliko,” alisisitiza Askofu Randazzo, ambaye mwenyewe ni  mwanasheria wa kanoni. Kwa hiyo alisema kuwa baadhi ya vipengele vya sheria “vinaweza kubadilishwa kulingana na mahitaji ya jumuiya na hali na hali fulani.”

Shemasi wa kike na nafasi ya wanawake

Katika suala la mageuzi, Mkutano Mkuu wa washiriki ulijadili uwezekano wa kufungua Ushemasi kwa wanawake, kwanza ilikuwa ni kufafanua "asili yenyewe ya ushemasi". Kuhusu nafasi ya wanawake katika Kanisa, Dk. Ruffini alisema kwamba “ilikumbukwa kwamba Yesu alihusisha wanawake na wafuasi Wake” na “swali liliibuliwa kama isingewezekana kufikiria kwamba wanawake, ambao walitoa tangazo la kwanza la Ufufuko, hawawezi pia kutoa mahubiri.” “Ilisemekana pia kwamba wanawake wanapokuwa kwenye mabaraza ya wachungaji, maamuzi yanakuwa ya vitendo zaidi na kwa jamii  ni wabunifu zaidi,” Dk. Ruffini aliendelea, huku akinukuu methali iliyotajwa ukumbini kuwa: “Unapotaka kuongelewa, fanya kusanyiko la wanaume, lakini mkitaka kufanya jambo, fanyeni mkutano wa wanawake.” Hata hivyo, ingawa jukumu la wanawake katika Kanisa lilikuwa lengo kuu la mjadala huo, kwa hakika halikuwa la kipekee au hata kuwa kuu, kama hata suala la ukuhani wa wanawake halijakuwa kubwa hadi sasa. Profesa Köhler-Ryan alieleza maswali kama hayo kuwa “suala la kawaida” ambalo halioneshi kuwa mahitaji halisi ya wanawake leo hii. “Nadhani kuna msisitizo mkubwa sana uliowekwa kwenye swali hili [la kuwekwa wakfu kwa wanawake katika ukuhani),” alisema. “Na kinachotokea tunapokazia sana suala  hili ni kwamba tunasahau kile ambacho wanawake, katika sehemu kubwa, wanahitaji ulimwenguni pote,” kukaa ndani nyumba, kuandaa chakula, mavazi, na wakati ujao wa watoto wao.” Lakini, “Ninataka kwa hiyo wawe wa wakati ujao, na wakati ujao ambapo wanakaribishwa katika Kanisa na kila mtu wanayemjua na kumpenda anakaribishwa Kanisani.”

Walei, mapadre, maaskofu

Ripoti za vikundi kazi na uingiliaji kati wa mtu binafsi pia zililenga katika masuala mengine kama vile : umuhimu wa parokia (“ambayo si kituo cha huduma tu bali ni mahali pa ushirika”) na wa jumuiya; huduma za walei, ambazo “si vizuizi kwa ajili ya ukosefu wa mapadre” na “hazipaswi kufanyiwa ukiritimba wa ukasisi”; na huduma zinazofanywa na mapadre, ambao jumuiya ya waliobatizwa haiwezi kufanya bila kuwa nayo.” Uangalifu kama huo ulitolewa Jumanne hiyo asubuhi kwa huduma ya askofu, ambaye anaweza kuonekana kama mtu,  baba anayewasindikiza  waamini na kuonesha upendo, utunzaji, na kujali, kulingana na Sheila Pires, Katibu wa Tume ya habari. Askofu anapaswa kukuza mazungumzo ya kidini na kiekumeni, anapaswa kusimamia fedha, nyanja za kiuchumi na kisheria na, hasa ili asilemewe na masuala kama hayo, Bi. Pires alisema, ilipendekezwa kwamba, katika "mtindo wa sinodi" angeweza kupokea msaada kutoka kwa washirika na wataalam. “Askofu anapaswa kuelewa kwamba yeye peke yake sio Jimbo. Hawezi kufanya kila kitu peke yake, na kwamba anahitaji msaada, "aliongeza. Baraza pia lilitazama suala la  malezi yanayoendelea ya maaskofu, na uhusiano kati ya maaskofu na mapadre, na maaskofu wapya, na kusisitiza ukweli kwamba maaskofu hawapaswi kuepuka kusikiliza waathirika wa dhuluma. Badala yake, lazima kuwe na wakati na nafasi kwa aina hii ya kusikiliza, alisisitiza Bi. Pires.

Kadinali Lopéz Romero:tuko katikati ya safari

Hoja nyingi, kwa hivyo, na mada nyingi zilishughulikiwa. Walakini, Mkutano huo  haujafikia hitimisho juu ya masuala haya, angalau sio katika awamu hii ya kwanza, ambayo, Kadinali López Romero alifafanua, ni nusu tu ya safari iliyoanza Oktoba 2021 na itaendelea hadi  2024. "Tunachopitia hapa Roma sio Sinodi," Kardinali alisema, akikumbusha maelfu ya mikutano iliyofanyika katika miaka miwili iliyopita kati ya parokia, majimbo na jumuiya za kitawa duniani kote. "Ilikuwa na thamani yake", alisema. "Kiukweli tulifanikiwa kufanya kazi na majivu ili mwali mpya uweze kuwashwa. Katika hatua hii, hatupaswi kutarajia mapendekezo. Bado tuna angalau mwaka wa kazi, na nina hakika kwamba tutakuwa na kazi ya nyumbani ya kufanya. Kisha tutafanya hitimisho ili kufikia mapendekezo thabiti zaidi.”

Mtazamo wa Uòlimwengu

Profesa Köhler-Ryan pia alizungumzia "wakati wa kuvutia", kwa hakika "wa kusisimua sana", wa maisha ya Kanisa. "Nadhani kinachotokea sasa hivi katika Sinodi hii ni kwamba tuna fursa kama Kanisa la ulimwengu wote kusikia kutoka katika sauti nyingi tofauti na kwamba mkazo wa kusikiliza pamoja kwa njia ya maombi umekuwa muhimu sana," alisema, akiongeza kuwa anafikiri kuhusika kwa waamini ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi kuhusu Sinodi hii." Kwa mujibu wa Profesa Köhler-Ryan alisema Sinodi ni "fursa kubwa ya kuwa na hisia ya mahali tulipo kama Kanisa la ulimwengu wote, na kuwa na hisia ya jinsi ilivyo kwamba kwa njia fulani sisi ni sawa sana, duniani kote. Tuna mafundisho ya ulimwengu wote, na kiukweli tunajaribu kwa njia nyingi tofauti kuwafikia wale ambao huenda hawajui kuhusu Kristo na Mama Yake na Kanisa letu,” alisema. Na tunajaribu kufanya hivi kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupitia teknolojia ya kidijitali, huku akitambua kuwa kuna watu ambao bado hawawezi kuzifikia.

Askofu Randazzo alishikilia mada kuwa: “Tunapozungumza kuhusu mawasiliano ya kidijitali na sinodi ya ulimwengu wa kidijitali tunapaswa kukumbuka kwamba kunaweza kuwa na kisiwa ambacho meli hupita mara kwa mara ikiwa na mafuta. Meli isipofika, haina mafuta, jenereta zao hazifanyi kazi, haziwezi kuunganisha kompyuta ikiwa nazo zinatengwa.” Askofu, kwa hiyo, aliwataka watu wasiangalie mambo “kwa njia ya Kizungu”, yaani, kuchukulia kuwa kila mtu ana tax na treni za kutoka sehemu moja hadi nyingine au, kwa mfano, kwenda parokiani . Tunazungumza kuhusu jamii hata katika eneo moja ambalo linaweza kuwa umbali wa kilomita elfu moja. Askofu Randazzo alisema, “Mojawapo ya matukio ya ajabu ninayopata kwenye Sinodi ni kukaa mezani na kushiriki kahawa ya hapa na pale na watu wanaokuja kutoka sehemu mbalimbali za dunia, ambao sio tu kutoka Ulaya, ambapo wanatoka katika jumuiya za kiutamaduni za Kanisa za Ulaya.” “Inasikika kama sinodi kubwa kwangu,” alisema. “Na ninadhani mojawapo ya fikra za Baba Mtakatifu,Francisko, ni kwamba hii si kitu ambacho huzaliwa katika (Vaccum) ombwe.”

Utajiri wa mchakato

Padre Orobator alikubaliana na Askofu Randazzo, akitania kwamba tukio hili la Kanisa ni mojawapo ya mambo ambayo wataalimungu “wanaishi”, yaani kuwa sehemu ya mchakato wa kupata rasilimali. “Ninasalia na hakika kwamba mchakato huo labda utakuwa muhimu zaidi kuliko matokeo," alisema. Padre  Orobator aliongeza, “Ninaamini kwamba hii ni aina ya mfumo na utaratibu ambao utatuongoza kama jumuiya inayoitwa Kanisa kupata uzoefu wa namna mpya ya kuwa ndani, ambapo watu, bila kujali wao ni nani, bila kujali hali zao au kituo au hali,  katika Kanisa, wanaweza kuwa sehemu ya mchakato ambapo si tu kwamba hawasikilizwi, lakini wanaweza pia kuchangia katika mchakato wa utambuzi.” Wakati huohuo, alitoa ushuhuda wa “tofauti za Kanisa na kuchota kutoka kwa hekima ambayo imejikita katika utofauti huu, kupata kutoka katika umairi na karama za kipekee ambazo utofauti huu hulitolea Kanisa.”

Hakuna uadui wala migongano

Tofauti, basi, inaweza kuonekana kama fadhila. Kuna “tofauti” nyingi, kwa hakika, zinazojitokeza miongoni mwa washiriki wa Sinodi, lakini, Kadinali Lopéz Romero alifafanua, kuwa, “Kamwe si migongano kati ya makundi” na hata si uadui.  Mantiki ni mazungumzo, sio "kujibu mwingine". Wala haihusishi kujibu waandishi wa habari: “Sinodi haijakusudiwa kujibu maswali ya mwanahabari mmoja au mwingine, bali imeundwa kwa ajili ya utambuzi wa Kanisa unaotokana na mchakato,” alisema Dk. Ruffini huku akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari. Yaani, inahusu utambuzi “juu ya jinsi gani Kanisa linavyoweza kutembea ulimwenguni.”

Mkutano  na vyombo vya habari

Akizungumzia kwa usahihi uhusiano kati ya mkutano na habari, mwandishi wa habari katika chumba hicho alisisitiza ukweli kwamba baadhi ya masuala, kwanza kabisa ya wanawake na mapokezi ya LGBT+, hayapaswi kuainishwa kama ujenzi wa waandishi wa habari tu, lakini masuala ambayo ni karibu kwa mioyo ya watu wengi wanaoamini ambao "wamewekeza" muda na nguvu wakati wa awamu ya mashauriano ya mchakato wa sinodi kwa usahihi ili kuwa na tafakari ya kina juu ya mada hizi  za  watu ambao sasa wanasubiri majibu. Katika suala hili, Dk. Ruffini aliweka wazi kwamba masuala haya "ni mada ya mazungumzo". Alisema,  wao Sinodi kwa hakika si tu “meza ya pande zote” na kwa hakika si “onesho la mazungumzo”, bali “mazungumzo katika Roho.” Alibainisha kuwa Mkutano Mkuu utatoa "ripoti ya awali ambayo itarudishwa kwa Watu wa Mungu na kisha kutakuwa na Mkutano mwingine." Bado ni mchakato mrefu ambao, kama Kadinali Lopéz Romero alisema, unahitaji "uvumilivu na matumaini".

Mhutasari wa Sinodi 17 Oktoba
18 October 2023, 11:10