Tafuta

Nembo ya COP28 UAE itakayoongoza Mkutano wa Umoja wa Mataifa huko Dubai, Novemba 2023. Nembo ya COP28 UAE itakayoongoza Mkutano wa Umoja wa Mataifa huko Dubai, Novemba 2023. 

Laudate Deum na COP28

Tunachapisha makala ya Osservatore Romano kuhusu Waraka wa hivi karibuni wa Papa na kuhusu Mkutano wa UN juu ya mabadiliko ya tabianchi unaotarajiwa kufanyika Novemba huko Dubai

Osservatore Romano

"Miaka minane imepita tangu nilipochapisha Waraka wa Laudato si', nilipotaka kushiriki nanyi nyote, kaka na dada zangu wa sayari yetu inayoteseka, mahangaiko yangu ya kutoka moyoni kuhusu utunzaji wa nyumba yetu ya kawaida ya pamoja. Hata hivyo, kadiri muda unavyosonga, ndivyo nimegundua kwamba majibu yetu hayajatosheleza, wakati ulimwengu tunamoishi unaporomoka na huenda unakaribia kuvunjika. Mbali na uwezekano huo, ni jambo lisilopingika kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi zitazidi kuathiri maisha na familia za watu wengi. Tutahisi athari zake katika maeneo ya huduma za afya, vyanzo vya ajira, upatikanaji wa rasilimali, makazi, uhamiaji wa kulazimishwa, nk. (2). Katika maneno haya tunapata kwa uwazi sababu zilizomfanya Baba Mtakatifu Francisko, kupitia Waraka wake wa kitume Laudate Deum, kuwasihi “watu wote wenye mapenzi mema” kuzingatia ipasavyo “hali ya mgogoro wa tabianchi”. Katika hati fupi lakini yenye makali ya upapa, vifungu vingi vinarejea Mkutano ujao wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (Cop 28), ambao utafanyika huko  Dubai kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 12 Desemba 2023. Nchi 198 zimejiandikisha. Mkutano huo, ikiwa ni pamoja na Vatican. Leo  tarehe 11 Oktoba, Rais Mteule wa Cop 28, Mheshimiwa Dk. Sultan Ahmed Al Jaber, amekutana na Baba Mtakatifu.

"Ikiwa tuna uhakika katika uwezo wa binadamu wa kuvuka maslahi yao madogo na kufikiria kwa undani zaidi, tunaweza kuendelea kutumaini kwamba COP28 itaruhusu uharakishaji madhubuti wa mpito wa nishati, na ahadi zenye ufanisi chini ya ufuatiliaji unaoendelea. Mkutano huo unaweza kuwakilisha mabadiliko ya mwelekeo, kuonesha kwamba kila kitu kilichofanywa tangu 1992 kiukweli kilikuwa kikubwa na chenye thamani ya juhudi, au sivyo itakuwa tamaa kubwa na kuhatarisha chochote kilicho kizuri ambacho kimepatikana hadi sasa(54). Kuepuka "tamaa" hii ni wasiwasi wa kila mtu: ni mchakato unaotia shaka "wadau" wengi, ambao wametajwa moja kwa moja au kidogo katika Waraka wa Laudate Deum, kwa matumaini kwamba mwingiliano wao unaweza kuhakikisha kwamba "maadili yatashinda" masilahi ya ndani au ya kawaida (39) na kujibu "kushindwa kwa dhamiri na uwajibikaji" iliyoshutumiwa na Waraka wa Laudato Si' (169).

Mmoja wa wadau hawa ni jumuiya ya kisayansi, iliyojitolea kumulikoa wazi kile ambacho sura ya kwanza ya Laudato si’ inakumbusha kuwa: "Ni nini kinatokea katika nyumba yetu ya kawaida". Baada ya miaka minane ya maandishi haya ya "kinabii", Laudate Deum inaonesha kwamba "haiwezekani tena kutilia shaka asili ya mabadiliko ya tabianchi ya mwanadamu" (11) na kwamba, kwa bahati mbaya, "sasa hatuwezi kusitisha uharibifu mkubwa ambao tumesababisha. Hatuna wakati wa kuzuia uharibifu mbaya zaidi "(16). Tukikabiliwa na uchunguzi huu wa kutia wasiwasi, hatuwezi kubaki bila shughuli au kutojali, lakini kuwa na mtazamo mpana unahitajika kwa haraka, ambao unaweza kutuwezesha kuthamini maajabu ya maendeleo, lakini pia kuzingatia kwa umakini athari zingine ambazo labda hazikuweza kufikiria karne moja iliyopita(18).

Hapa ndipo mdau mwingine anapotokea: ulimwengu wa ujasiriamali, ambao una jukumu muhimu la kuitikia kwa vitendo hisia hii ya dharura kutoka katika Jumuiya ya wanasayansi na kuendeleza kwa akili mageuzi ya haraka, kutunza nyumba yetu ya kawaida ya pamoja. Kulingana Waraka wa Laudato si’ biashara ni wito adhimu, unaolenga katika kuzalisha mali na kuboresha ulimwengu wetu. Inaweza kuwa chanzo chenye matunda ya ustawi kwa maeneo inakofanyia kazi, hasa ikiwa inaona uundaji wa nafasi za kazi kama sehemu muhimu ya huduma yake kwa manufaa ya wote(129); katika mtazamo huuo, Laudate Deum inasisitiza kwamba mara nyingi inasikika pia kwamba juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya tabianchi ya kupunguza matumizi ya nishati ya mafuta na kuendeleza vyanzo vya nishati safi itasababisha kupungua kwa idadi ya kazi. Kinachotokea ni kwamba mamilioni ya watu wanapoteza kazi zao kutokana na athari tofauti za mabadiliko ya tabianchi: kupanda kwa kina cha bahari, ukame na matukio mengine yanayoathiri sayari yamewaacha watu wengi. Kinyume chake, mpito wa aina za nishati mbadala, zinazosimamiwa ipasavyo,pamoja na juhudi za kukabiliana na uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabiachi, zina uwezo wa kutoa kazi nyingi katika sekta tofauti. Hii inadai kwamba wanasiasa na viongozi wa biashara wanapaswa hata sasa kujishughulisha nayo (10).

Hii inaweza tu kuwa na matokeo chanya kwa mdau wa tatu: vijana na vizazi vipya. Ni rahisi kutambua kwamba njama iliyoelezewa ya Laudate Deum inawageukia: "Kinachoulizwa kwetu sio chochote Zaidi isipokuwa jukumu fulani la urithi ambao tutauacha, mara tu tunapopita kutoka katika ulimwengu huu" (18). Hotuba ya Papa Francisko kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu wakati wa Siku ya Vijana Ulimwenguni huko Lisbon mnamo tarehe 3 Agosti 2023 inakuja akilini kwamba: "Kwa hivyo, fanyeni kazi kuleta "tamasha" jipya, ambalo linaheshimu "ngoma" ya maisha ya kumweka mwanadamu katika Maisha na kitovu  hicho. […] Mzee huyu sasa anazungumza nanyi - kwa maana mimi ni mzee! - pia ndoto yenu kwamba itakuwa kizazi cha walimu! Walimu wa ubinadamu. Walimu wa huruma. Walimu wa fursa mpya kwa sayari yetu na wenyeji wake. Walimu wa matumaini. Na waalimu wanaotetea maisha ya sayari yetu, ambayo leo hii inatishiwa na uharibifu mkubwa wa kiikolojia. Hapa ni kwamba hali ya elimu na mafunzo inakuwa kiwezeshaji muhimu.

Mashirika ya kiraia ni mdau  wa nne. Akirejea maneno ya Waraka wa  Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu, kwamba "makundi na mashirika mengi ndani ya jumuiya ya kiraia husaidia kufidia mapungufu ya jumuiya ya kimataifa, ukosefu wake wa uratibu katika hali ngumu, ukosefu wake wa kuzingatia haki za msingi za binadamu" (175), katika Laudate Deum anasisitiza kwamba "katika muda wa kati, utandawazi unapendelea maingiliano ya kiutamaduni ya moja kwa moja, maarifa zaidi ya pamoja na michakato ya ujumuishaji wa watu, ambayo mwishowe huchochea umoja wa pande nyingi "kutoka chini" na sio ule tu unaoamuliwa na wasomi wa nguvu. Madai yanayoinuka kutoka chini duniani kote, ambapo wanaharakati kutoka nchi tofauti sana husaidia na kusaidiana, yanaweza kuishia kushinikiza vyanzo vya mamlaka. Hivyo hii inatarajiwa kuwa itatokea kwa heshima na shida ya hali tabianchi ” (38).

Mdau wa tano anawakilishwa na serikali. COP 28 itaandaliwa na kuongozwa na Umoja wa Falme za Kiarabu. Nchi, ambayo ni msafirishaji mkubwa wa nishati ya mafuta, imekuwa ikipitia mabadiliko ya nishati kwa karibu miaka 20. Kama Urais wa COP28, ilianzisha Ajenda ya Utekelezaji yenye nguzo nne muhimu: kufuatilia kwa haraka mpito wa nishati wenye haki na utaratibu, kurekebisha fedha za tabianchi, kulenga watu, asili, maisha na riziki, na kutegemeza kila kitu kwa ushirikishwaji kamili. Nguvu zinazoibuka zinazidi kuwa muhimu na kiukweli zina uwezo wa kupata matokeo muhimu katika utatuzi wa shida thabiti […]. Ukweli ni kwamba majibu ya shida yanaweza kutoka katika nchi yoyote, hata kidogo, huishia kuwasilisha umoja kama mchakato usioepukika ” (40). Papa Francisko kwa hiyo anahimiza kila mtu kuwa na matumaini katika matokeo chanya ya COP28.

Kwa hakika, Cop 28  mbele yake ina fursa muhimu ya kutoa msukumo wa kweli kuelekea mpito unaozingatia manufaa ya wote na mustakabali wa watoto wetu: “suluhisho la ufanisi zaidi halitokani na juhudi za mtu binafsi pekee, bali zaidi ya yote maamuzi makubwa ya kisiasa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa(69).” Ni mchakato mgumu, lakini wa lazima, kwa wanadamu leo na kesho, ambao unahitaji ushiriki wa kila mtu, katika ufahamu kwamba "Kila kitu kimeunganishwa" na "Hakuna anayeokolewa peke yake" (19) na kwamba "hakuna mabadiliko ya kudumu" bila mabadiliko ya kiutamaduni, bila kukomaa kwa mitindo ya maisha na imani ndani ya jamii, na hakuna mabadiliko ya kiutamaduni bila mabadiliko ya kibinafsi(70). "Kwani wanadamu wanapodai kushika nafasi ya Mwenyezi Mungu, wanakuwa maadui wao wakubwa." (73).

11 October 2023, 16:47