Tafuta

2023.03.15 Uwakilishi wa Mtumbwi wa Mtakatifu Pietro" ambao kuanzia tarehe 10 Oktoba unaweza kutazamwa na mahujaji na watalii katika Jumba la Makumbusho. 2023.03.15 Uwakilishi wa Mtumbwi wa Mtakatifu Pietro" ambao kuanzia tarehe 10 Oktoba unaweza kutazamwa na mahujaji na watalii katika Jumba la Makumbusho.  (Vatican Media)

Kazi ya Mtumbwi wa Petro kwenye Makumbusho ya Vatican kuanzia 10 Oktoba

Papa alipokea mfano wa mtumbwi mkubwa wenye urefu karibu mita 9 x 2,ambao unapata nafasi ya kimaadili na maalum kwenye msingi wa njia panda ya kisasa katika maonesho ya kudumu kwa ajili ya mahujaji wote kutoka ulimwenguni kote katika Jumba la Makumbusho Vatican.Kuanzia Oktoba 10 utaonekana.

Na Angella Rwezaula, Vatican

Papa alipewa kazi ya bure ya sanaa iliyoundwa na Aprea, walimu wa meli kutoka peninsula ya Sorrento, nchini Italia kwa ushirikiano na Taasisi ya Kimataifa ya Kidiplomasia. Zawadi ni ya mfano wa mtumbwi wa thamani, kutoka  familia ya kihistoria ya wamiliki wa meli ya Aponte, iliyoabrikiwa na Papa mnamo tarehe 15 Machi 2023 kama ilivyoripotiwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Makumbusho ya Kipapa.

Siku ya kubariki sanaa ya mtumbwi wa Petro
Siku ya kubariki sanaa ya mtumbwi wa Petro

Mtumbwi huo ni nakala ya uaminifu wa Navicella di Pietro, yaani wa Meli  ya Petro  ya zamani na ya asili iliyopatikana mnamo 1986 chini ya Ziwa Tiberias na leo iliyohifadhiwa katika jumba la makumbusho la Yigal Allon huko Ginosar, huko Galilaya. Kwa hiyo kuanzia Jumanne tarehe 10 Oktoba 2023, Mtumbwi huo mkubwa, wenye urefu wa karibu mita 9 x 2, utapata eneo lake la kimaadili na dhahiri kwenye lango la Makumbusho ya Vatican, iliyo kwenye msingi wa njia panda ya kisasa ya helical inayoitwa Via del Mare, au njia ya Bahari ambapo  mtumbwi huo utakuwa ni katika maonesho ya kudumu kwa mahujaji na watalii wote kutoka ulimwenguni wanaofika mjini Vatican.

08 October 2023, 15:54