Kardinali Parolin anapinga kuongezeka kwa vita Mashariki ya Kati
Vatican News
Watu wawili, majimbo mawili. Hii imekuwa daima na inaendelea kuwa msimamo wa Vatican kwa Israel na Palestina, pamoja na suluhisho pekee linaloweza kuhakikisha mustakabali wa amani na ukaribu wa utulivu, kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili . Hayo yalisemwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, anayeiomba dunia kuwatazama hasa watoto wahanga wa mgogoro huu mpya: kwamba: “Tunawafikiria watoto waliosambaratishwa na Hamas, lakini pia watoto wengi wanaofariki dunia chini ya mabomu Gaza. Wito wake ni zaidi ya yote kwao, kuzingatia kutokuwa na hatia, maisha yao ya baadaye.
Vatican inapatikana kufanya kila linalowezekana
Kardinali huyo alizungumza hayo tarehe 27 Oktoba 2023 katika hafla maalum ya Kadinali Achille Silvestrini huko Mlimani Campidoglio, Jijini Roma. Kando ya afla hiyo Kardinali aliohojiwa na waandishi wa habari, ambapo alisisitiza uwepo kamili wa Vaticanmahali hapo ili kuchangia katika suluhisho la amani ya Mashariki ya Kati iyyogubikwa na mivutano na ghasia. Kardinali amesema: “Tutafanya kila tuwezalo, Papa anajitokeza sana kuhusu hili.” Kupitia maikrofoni na Camera kwa hivyo alizindua wito mpya iliyosisitizwa mara kadhaa na Papa Francisko katika wakati huu wa vita.
Wito ambao ni, kwamba sababu za amani zinaweza kushinda ghasia na vita na pia wito wa kuachiliwa kwa mateka na kisha kwa mgogoro wa kibinadamu huko Gaza. Haya ni mambo mawili ambayo hatua za Vatican inazingatia, alisisitiza Kardinali Parolin, akielezea kwamba kwa sasa hakuna ‘nafasi kubwa’ ya upatanishi na Vatican. Walakini, kuna uwezekano mahali kwa uwepo wa Kanisa la mahalia, kupitia Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu na kwamba kunaweza kuwa na kuingiliana kati na kubadilishana ujumbe. Na zaidi kwa upande huo kwamba tunajaribu kufanya kitu.
Mkutano unaowezekana kati ya Papa na familia za mateka unachunguzwa
Kuhusu uwezekano wa uvamizi wa ardhi katika Ukanda wa Gaza, Kadinali alielezea matumaini kwamba hakuna hali mbaya zaidi na kwamba inaweza kutatuliwa vinginevyo. “Ninaamini kwamba suala hilo linahusiana sana na suala la kuachiliwa kwa mateka, ikiwa shida ya mateka inaweza kutatuliwa pengine kungekuwa na uharaka mdogo wa kuchukua hatua za msingi. “ Kuhusu mateka wa Israel, Kardinali Parolin – alijibu swali kuhusu mkutano wa Papa na familia za watu waliotekwa nyara – kwamba: "Tunafikiria juu ya hili, tumeona kwamba wako hapa na wamepokelewa kwa kiwango cha juu kwa taasisi nchini Italia, kwetu bado Uamuzi wa mwisho haujafanywa lakini naamini utafanyika kufikia leo.”
Mawasiliano na Marekani
Hakuna taarifa kutoka kwa kadinali kwenye simu iliyopigwa kwa Rais wa Uturuki Erdogan kwenda kwa Papa (Sifahamu yaliyomo); alipokuwa kwenye mazungumzo ya simu ya Oktoba 22 kati ya Papa Francisko na Rais wa Marekani Joe Biden, alisema: “Tunafikiri kwamba Marekani inaweza kuchukua jukumu muhimu katika kesi hii pia. Papa alirudia msimamo wa Vatican kuelekea Biden, akipata sikio la kusikiliza kwa sababu Biden mwenyewe kutokana na kile nilichoelewa ana wasiwasi juu ya uwezekano wa kuongezeka vita na anatumaini kuwa mambo hayatakuwa mabaya zaidi. Mawasiliano mengine na viongozi wengine wa kimataifa hayajatengwa: “Itatathminiwa siku baada ya siku kulingana na jinsi hali inavyoendelea.” Alisema kardiali Parolin
Janga la Ukraine
Hatimaye, Kardinali Parolin hakusahau Ukraine na janga la idadi ya watu ambalo limekuwa kwenye vita kwa takriban miaka miwili. “Sasa Ukraine imetoka nje ya uangalizi kidogo, lakini kwa hakika tunaendelea kulifanyia kazi hilo pia,” alihakikishia. “Tunaendelea kufanya kazi zaidi ya yote katika nyanja ya kibinadamu, mkutano wa washauri wa kisiasa kwenye jukwaa la amani la Rais Zelensky unaendelea huko Malta. Kutakuwa na ushiriki wa nuncio. Nilitengeneza video jana kusema kwamba tunaendelea kutilia maanani mkasa wa Ukraine na hitaji la kutuhusisha sote kutafuta suluhu."