Kardinali Parolin atembelea Ubalozi wa Israel mjini Vatican
Kardinali Pietro Parolin alitembelea Ubalozi wa Israel unaowakiisha nchi yake mjini Vatican na kueleza mshikamano wake kutokana na shambulizi la Jumamosi iliyopita dhidi ya Israel na kujali maisha ya raia wa Israel na Palestina hasa wale wa Gaza.
Vatican News
Siku ya Ijumaa asubuhi, tarehe 13 Oktoba 2023, Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin alitembelea Ubalozi wa Israel unaowakilisha Nchi hiyo mjini Vatican ili kuwasilisha mshikamano na msaada wa kiroho kwa Balozi Raphael Schutz kutokana na shambulio la kusikitisha lililotokea Jumamosi iliyopita tarehe 7 Oktoba 2023.
Katika muktadha huo, Kardinali Parolin alionesha wasiwasi wake kwa ajili ya ustawi wa raia, Waisraeli na Wapalestina, hasa walioko Gaza, huku kukiwa na mzozo unaoendelea.
13 October 2023, 16:32